Monday, January 25, 2010

SIELEWI NINI KINAENDELEA KATI YA MCHUMBA WANGU NA RAFIKI YANGU, NAOMBENI USHAURI


 Dada Violet, kwanza nashukuru kwa kufungua blog ambayo naamini itatusaidia sana katika mambo mengi, na hata ushauri pia, mkasa huu ulionipata naomba uuweke ili nishauriwe kwani hadi sasa sijui la kufanya.
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27, nafanya kazi katika Company moja ya simu, nina mchumba wangu ambae tumekuwa na uhusiano wa miaka minne sasa, nateyari ameshanivalisha pete, kwao nafahamika nae kwetu anafahamika, lakini siku za hapa karibuni nimekuwa siwaelewi yeye na rafiki yangu mimi, nina huyu rafiki yangu ambae nampenda sana, na namshirikisha mambo mengi, hadi kwa mchumba wangu nimemtambulisha na anamfahamu vizuri, miezi miwili iliyo pita mchumba wangu alikuwa na graduation, Basi kwakuwa aliniambia baada ya kutoka chuoni kutakuwa na part ya kumpongeza mahali fulani, basi nami sikusita kumfata rafiki yangu kumualika, cha ajabu nilipokuwa nikimuelezea alidakia na kunieleza kila kitu, kwamba mbona shem alishaniambia, siku nyinigi? wakat mimi ndio nimetoka kuambiwa, iliniuma lakini nilitake easy, basi ikafika siku ya tukio, nikampitia rafiki yangu kwao, sikumkuta isipokuwa nilikuta wadogo zake na nikakuta box kubwa sana la zawadi, nilipouliza wakasema amefunga zawadi ametoka kidogo, wewe tangulia tu! tukafika ukumbini, tumekaa kidogo nae rafiki yangu akaingia akiwa na box lake la zawadi, kitu nilichonote pale nikwamba rafiki yangu na mchumba wangu walikuwa wamebadilika sana, kila mtu ananijibu dry kwa chochote nitakachouliza, nikawa nimekosa amani kabisa, kabla ya party kuisha nilitangulia kwenye gari ya mchumba wangu, nikaanza kulia, sababu sikuwa nikijisikia vizuri, party ilipoisha walikuja hadi kwenye gari, mchumba wangu na rafiki yangu, akaniambia, kwanini uko huku? nikamwambia najisikia vibaya, wala hakuonyesha kujali, akaniuliza tunaenda wote nyumbani? nikamwambia ndio, akasema ngoja tukamshushe kwanza rafiki yako kwao ndio twende, nikamwambia sawa, bas hata wakati tuko kwenye gari, walikuwa wakipiga story wao, mimi wamenitenga kabisa, hata wakiongea nikichangia wanapotezea ile mada na kuleta ingine, inaniuma sana, kwani nampenda sana mchumba wangu, tulipomfikisha kwao tukarudi kwa mchumba wangu, tukaanza kufungua zawadi, nilikuwa nina hamu ya kujua ndani ya box la rafiki yangu kuna nini, nilipofungua sikutaka kuamini nilichokiona, nikakuta amemuwekea chupi za dazani moja, boxer dazani moja, kondom box zima, vest, viwembe, tauro,na mashuka, na picha yake, nikamuuliza mchumba wangu, imekuwaje? akasema unaniuliza mimi? muulize rafiki yako, nililia sana, nikampigia rafiki yangu simu, cha ajabu hakuonyesha kushtuka kabisa, ndio kwanza akaanza kucheka akasema mimi nilifikiri umekuta bastola au bomu, kumbe umekuta zawadi za kawaida tu! niache nilale bwana, akakata simu,
nilitoka usiku uleule hadi nyumbani, nilililia sana, kesho yake nikawanampigia simu mchumba wangu akawa hapokei na hata rafiki yangu pia akawa hapokei,  nikaenda nyumbani kwa wazazi wa mchumba wangu nikawaeleza wakakasirika sana, wakamuita, walimsema na pale pale baba yake akamuuliza unampango gani na binti wa watu, jibu hapahapa, yeye akasema ananipenda na bado anataka kunioa, lakini toka tutoke kwenye kikao kile, nimekuwa simuelewi kabisa, ananishushua hovyo, ananikaripia tu hata mbele za watu, hataki kutoka na mimi kama zamani,
hali hii inanipa shida sana, nashindwa hata kufanya kazi zangu kwa ufanisi, inaniuma sana yani. naomba mnisaidie dada violet na wadau wengine, nimepoteza muelekeo wa maisha kabisa,
bado nampenda sana mchumba wangu,

26 comments:

 1. pole sana mpenzi wangu, kwakuwa umeweka na unahitaji ushauri, basi naomba nikushauri, pia kuna wengine watakushauri, ninachoamini walipowengi hapaharibiki kitu, utapata ushauri wa maana kabisa.
  Hadi sasa, ninachokiona mimi ni kwamba huyu mchumba wako hakupendi, ila ameona haya tu kusema mble ya wazazi wake, labda kwa kutowavunjia heshima wao, lazima ujiulize, huyo rafiki yako hakuona zawadi zingine za kununua hadi anunue chupi? anunue boxer? bado haitosho aweke na kondomu? haya na picha yake ameiweka ya nini? kusema ukweli uko katika wakati mgumu sana, huyo rafiki yako hafai hata kidogo, na vunja urafiki nae kabisa, watu wa hivyo wako wengi sana dear, hata mimi kuna rafiki yangu mmoja alishawahi kutaka kuanza upuuzi kwangu, nashukuru baba Tracy alikuwa muwazi na tulishirikiana nae kukemea tabia hiyo. ila huyo mchumba wako wewe ni wazi kwamba kuna kitu kinaendelea kati ya hao wawili, wewe chunguza tu kwa makini utagundua, kwanini uingie kwenye ndoa ambayo imeshaanza kkukupa mateso kabla? kwanini? wakati maisha ya ndoa ya wawili inatakiwa amani ili uifeel ndoa? mimi ningekuwa wewe, ningemwita rafiki yangu pamoja na mchumba wangu na kuwaomba waniweke wazi, wasinifiche, na wakionekana kujing'atang'ata kweli tena nisingeendelea nae ningemwachia pete yake ningekamata hamsini zangu. kkukuvalisha pete isiwe sababu ya kukufanyia upuuzi, na huyo rafiki yako hafai kabisa.
  nisimalize yote naomba na wengine pia wakushauri,
  pole najaribu kuhisi unavyojisikia, hasa kwa mtu unaempenda.

  ReplyDelete
 2. ah! mbona vitu vingine havihitaji hata ushaauri?? sasa hadi hapo wewe unaona bado unapendwa???
  achana nae hakupendi na atakupotezea muda wawako tu, shauri yako

  ReplyDelete
 3. huelewi nini wakati kinachoendelea hapo kinaeleweka??
  NI MAPENZI NDIO YAPO HAPO
  Achana nae, njoo kwangu nitakuoa, unaonekana ni mstaarabu

  ReplyDelete
 4. Inawezekana!
  Kweli kabisa lazima uumie mrembo, rafiki yako na mpenzi wako wooote wanamakosa ya kushirikiana kukuangamiza wewe kwenye mapenzi. Kikubwa nataka kusema,jifunze kupuuza, jifunze "kufungulia mbwa" nikiwa na maana waache wafanye mambo yao kwa kiwango wanachoweza utajua kila kitu wazi wazi, kwakuwa sasa wanaibana na kufanya kwa kificho ndio maana wanakutesa sana. Ila ukiwaacha huru haitachukua muda watachokana na utaona mbwa wako atarudi nyumbani mkia matakoni. Naongea hivi nikiwa mimi nimepractice jambo hilo. Sasa akirudi utaona anavyojisemesha na kujaribu kufanya mambo ya kukufurahisha, kwakuwa alishajishusha dhamani kwa muda uliopita hata mambo atakayoyafanya kwako yatakuwa hayana dhamani pia. Itamuuma sana na atahangaika sana. Pia elewa kitu chochote kikiwa kinazuiliwa mara zote mwanadamu hupenda kukifanya. Eg Gongo, Rushwa, Madawa ya kulevya, basi hata mapenzi ya usaliti ni haramu lakini watu wanapenda kufanya hata kwa nguvu.
  Kama umenielewa hapo juu itakuwa vyema sana, chakufanya shusha moyo wa wivu, kuwa busy sana na kazi yako au jambo lolote la msingi. Ukitaka kujua ukweli zaidi na kuwatenganisha utakula muda wako pasipo malipo. Tulia tu kimya sana, najua kwa sasa unaumia kwakuwa unampenda ila jifunze kupotezea utaona hawaiendi mbali.
  Mimi najua mwisho wa mapenzi ya namna hiyo, hayawezi kudumu kama ulivyokuwa wewe na yeye.
  Natamani ningekuwa nakueleza kwa kuongea kwa sauti ningesema mengi sana na ningefurahi kuona umenielewa. Mungu akipenda tunaweza wasiliana.
  Ok kazi njema

  BABA MKUBWA

  ReplyDelete
 5. kwa hiyo wewe BABA MKUBWA unachomshauri aendelee kuchunguza nini wakati muda unaenda na umri unaenda? bora nyie wanaume, hata mkizeeka mnaoa, lakini sisi wanawake, tofauti na nyie,cha msingi ukishagundua kitu cha kutaka kukunyima raha, kukunyima amani ndani ya roho, ukiona mtu kama hivyo anakushushua shushua mbele yawatu, anakukaripia, hataki kutoka na wewe, sasa wanini tena?? mimi huwa nashangaa sana, eti unakuta mtu yuko ndani ya ndoa anateseka, anadharauliwa, ananyanyasika, lakini ameng'ang'ania humohumo kisa ndoa, ndoa kitu gani? ondoka ishi peke yako, lakini usiishi kama ndege mkiwa. mimi nakwambia hivi, achana nae, wanini?kwani hakuna wanaume wengine hadi yeye? kwanini ufupishe maisha yako, ACHANA NAE, huyo sio wa kuvumilia wala kuongezewa muda wa marekebisho
  JOYS

  ReplyDelete
 6. mdogo wangu, mimi naamini kabisa kwamba mtu hata awe amegeuka vipi, amebadilika vipi, still ni mwanadamu, lazima atachange tu! pengine ni jaribu lako tu mungu ameamua kukupimia, usimuache, wewe endelea kumuomba Mungu, kama aliumbwa kwa ajili yako, basi huyo ni wako na atatulia tu! watu wanakushauri na ushauri wao ni muhimu, lakini kwa suala la mapenzi hutakiwi kukurupuka, mapenzi yanatesa sana, yanaumiza sana, yanaweza hata kuua, huna haja ya kumuita rafiki yako, muite yeye tu! ongea nae kwa mapenzi, muulize kama kunamahali labda umekosea ndio maana anakufanyia vituko, akisema vipo, wewe tubu, kubali kushuka, na kama hana muulize tena anampango gani na wewe, usikurupuke tu kumuacha au kuvumilia tu bila kutake action yeyote, nakuhurumia sana mdogo wangu, mapenzi yanatesa na yanaumiza sana.

  ReplyDelete
 7. Jaman mpz wangu kwanza pole,pili huyo mtu asikusumbue jitaid kumuomba mungu akusaulishe wala usiwaonyeshe kuwa umeumia take it easy na maisha yataenda,wanaume ninavyowajua kilichokutokea wewe ndicho kitakachomtokea huyo rafiki yako verry soon,wanaume wana tamaa sana atataman mwingine na kumuacha huyo rafiki yako naye ataumia ivyoivyo huwa malipo ni hapahapa dunian,halafu ma dia cku nyingine usikubali mwanaume akaiteka akili yako ni kwel kuna kupenda but jitaidi kupenda kwa asilimia hata 80% nyingine ishirini unaziacha incase of anything unakua na uwezo wa kujicontrol,,achana nae asije akakuletea maradhi na mwanamke au mwanamme kama kabla hajaoa or kuolewa kama hujatulia kwa maana huwezi kuwa na msichana or mvulana mmoja hata ukiolewa au kuoa utakua hivyohivyo mshukuru mungu kwa kukuonyesha kabla hujaingia kwenye ndoa,pole sana my dia

  ReplyDelete
 8. jaman..mimi imeniuma kama ndio nimefanyiwa mimi..ila dada yangu hapo hakuna mapenzi..tafuta muda muombe mchumba wako mtoke ..muulize taratibu kua ana mpango gani na wewe na umuuleze jinsi anavyofanya na rafiki yako..ukiona bado hajali ..basi achana nae..atakupotezea muda ..Mungu atakupa mwingine ...

  ReplyDelete
 9. JOY, umenisoma vibaya, haina haja ya kumchunguza. Akichunguza atapoteza muda wake tu. Kikuwa nilichomwambia akae kimya na aendelee na shughuli zake. Pia kama umesoma vyema nimejitolea mfano mimi mwenyewe kwa mke wangu niliongea nae sana ikawa ni majibu mabaya na ujeuri wa kupindukia, ila nikaona haina haja kumzuia naona kama namchochea. Nikaacha kumfikiria wala kumuuliza. Hivi naandika hapa wameshachokana na hata date za kwenye mabo ya ku-DO jamaa hamtaki anamwambia anakisukari kwahiyo mashine haifanyi kazi. Lakini baada ya kuona sasa hata zile out za nyama choma pia hazipo amegundua kuwa muda wake umeisha na kuna mwingine anakula nyama choma. Sasa mke anarudi kwa kasi ndani na kujaribu lile mara hili. Sasa mimi naona kama anaigiza tu kwakuwa nimeshampuuza sana kwani ananitumia kama mapumziko yake ya fujo za nje.
  Kwahiyo huyo dada wala asiwe na haraka ya umri na wala asiwe na haraka ya kwenda kwa mwanaume mwingine. Watu wanaolewa na mika 40 sembuse yeye.
  BABA MKUBWA

  ReplyDelete
 10. mbona mkasa wangu huyatumi kwenye blog wanishauri? nisaidie dada violet, nina wakati mgumu sana. nahitaji ushauri, nimetumia hiyo personal email yako, au hujaipata?
  please dada violet

  ReplyDelete
 11. kwa hiyo baba mkubwa umeamua nini hadi sasa? mimi niko ofisi moja hapa Town, niliwahi kumkuta mke wangu live na rafiki yangu wa karibu, iliniumiza sana, nilijaribu kupotezea kama unavyosema lakini haikunisaidia, moyo bado ulipata pigo, nilimdharau kupita kiasi, alijaribu kuniomba msamaha nilikataa nilimfukuza, akaenda kwao, kumbe aliondoka akiwa mjamzito, demu mwenyewe kwao mambo safi, akafika kule akajifungua, mimi nikajua yule mtoto ni wa rafiki yangu, ila kuna siku nikakutana na rafiki yake, akaniambia mtoto amefanana na mimi sana, nilichokifanya nikampa hela kidogo ili aniibie mtoto siku moja aniletee, kisha atamrudisha, ilimpa hofu sana, nilipomueleza dhamira yangu alikubali, siku alipomleta mtoto nikaenda kupima damu, iko sawa na yangu, kumbe ilikuwa mimba yangu, nilikaa peke yangu na mtoto wangu mdogo aliemuacha kwa muda wa mwaka mmoja, ilikuwa shida sana, mtoto kumuacha na housegirl, ukizingatia mke wangu bado nampenda ila nikikumbuka tu nilivyowakuta live na mke wangu, moyo unaumima sana, aisee nisikufiche mshkaji wangu, nilikonda kitambi chote kikaisha, yani nilitamani hata kujiua, of course sisi ni wakristo na tunandoa ya kanisani, nilienda kwa mchungaji kumuelezea, mchungaji akanishauri, akafungua baadhi ya vitabu akanipa maandiko, aisee nilijiona mimi ni mkosefu sana, nilichokifanya nilienda hadi kwao mimi na mchungaji, tukaita wazazi wake na wangu, tukakaa, mchungaji akaongea sana na kutaka kutuomba turudiane, nilistaajabu kipindi ambacho mimi ndio nataka nimsamehe, yeye akawa hataki kusamehewa, BABA MKUBWA usiombee ikukute hii hali, nilijuta kwanini sikumsamehe kipindi kile, alikataa kata kata, akasema yeye anataka kuolewa, basi tukaondoka, nikakaa kama wiki tu! nikafukuzwa kazi kwa madai utendaji wa kazi ni mbovu, aisee nilichanganyikiwa, lakini alienichanganya zaidi ni mke wangu, nilipiga magoti, nikaomba mungu anisamehe dhambi zote, na anipe kibali kwa mke wangu, nikaamua kumsamehe, nikaamua kusahau, nikamtumia rafiki yake kunikutanisha nae, alikataa tena, akavunja na urafiki na huyu rafiki yake, sikuchoka, nikamfata tena akiwa peke yake mahali, nilimkumbusha mbali sana tulipotoka, tuliyopitia, na nikamwambia mimi nimemsamehe na nitarudisha mapenzi kwake, uanjua alichoniuliza?
  aisee huu mkasa nitamtumia huyu dada yetu violet auweke hewani, naamini utamsaidia kila mtu, hivyo BABA MKUBWA, na wewe dada unaetaka ushauri, hakuna kitu kizuri kama kusahau lililopita na si kudharau? sahau na dharau ni vitu viwili tofauti, yeye amuite mchumba wake, amwambie anavyojisikia, amsamehe na asahau waanze upya
  ni hayo tu!

  ReplyDelete
 12. mimi ni mama yako, kwakuwa binti yangu wa kwanza ana miaka 30 ni mkubwa kwako, na ninakushauri kama mama yako. kwanza nikupe pole kwa lililokupata, limenisikitisha na kuivuta akili yangu sana. limenikamata hisia zangu na kunipotezea furaha niliyokuwanayo leo, nasikia uchungu sana. blog ya huyu dada ndio kwanza nimeiona leo kupitia kwa kanumba. ila nikukumbushe tu kuwa hakuna aliemkamilifu hata mmoja hapa ulimwenguni, sote ni wakosefu kwa Mungu, hata malaika walidanganya wakashushwa chini kuwa majini, itakuwaje kwetu sisi wanadamu? cha msingi nakusihi wewe dada, muite mchumba wako uongee nae na akitubu msamehe, hakuna kitu kizuri kama kusamehe na kuanza moja, msamehe mchumba wako, wanaume tabia zao hufanana, na wanawake tabia hufanana ukimuacha huyo unaweza kuja kupata mchafu kuliko huy wewe muombee na utulie
  pia nikupongeze wewe kaka ambae umeamua kumsamehe mke wako, umeamua jambo la maana sana, hata max ulizopata kwa Mungu ni nyingi, unajua tatizo la binadamu huwa wanatamka tu nimekusamehe, lakini wanalo bado moyoni, wewe liache tu! endelea kumuomba msamaha atakubali tu! pengine wakati anakuomba msamaha yeye ulimdharaku sana kama ulivyosema, ndicho kinachompa mashaka hata yeye, cha msingi naomba kama utakubali nikuelekeze nilipo uje tuende pamoja kwa huyo mke wako nitakusaidia, kwani nje ya kazi yangu, huwa ninafanya na cancelling kwa watu mbalimbali, ataelewa tu, nakuonea huruma sana mwanangu,
  MAMA IRENE

  ReplyDelete
 13. Aaaah kwakweli nilichoamua mimi anipe muda tu taratiiibu nitarudisha mapenzi kwake kama zamani. Yeye awe kwenye nafasi yake ya mke inatosha ila sio kuforce mambo ili nione kama napendwa ndio maana nasema naona kama anaigiza. Kweli ilinisumbua sana mara ya kwanza kwakuwa nilimpa uhuru na kumuamini kwa kiwango kikubwa. Ilikuwa kama miezi 6 najaribu kumuweka sawa lakini haikufaa. Nikapuuza na kumsahau kama yupo, kama atarudi home sawa, kama ataamua asirudi pia sikuwa niko tayari kuumia. Kwahiyo nikawa naona naishi na dada, tufanye tendo la ndoa au tusifanye nona poa tu kwakuwa nilikuwa namuona mbwa kabisa. So ni hivyo tu ingawa watu nikiwapa mkasa wangu wanasema wewe nimtu wa aina yake ni mvumilivu wa kuwango cha juu sana. Yaani wanasema wasingeweza hata miezi 2. Nilimsimulia broo wangu mkubwa akasema wewe unaroho ngumu hata SUNAMI haiwezi kuitoa. Lakini nifanye jambo gani kwakuwa mtu anafanya akiwa na akili zake. Sio issue maisha yanaendelea ila ni full kujistukia.
  Ila pole sana mkubwa kwa mkasa wako huo ulifanya maamuzi ya kufuka kwa haraka sana. Huku mjini ndio tunasumbuliwa na hawa wanawake au watu wazinzi. Ingekuwa kijijini unaenda kwa SANGOMA unamuomba afanye mambo watu wanasiane tu. Ili kwa wanadoa wengine wajifunze. (Hili ni wazo la hasira)

  BABA MKUBWA

  ReplyDelete
 14. hivi siku mungu aamue kufunua dhambi za mwanadamu, kuna atakaesalimika? iweje wewe ushindwe kumsamehe mwenzio? na wewe kaka uliekuwa ukitupa story yako ukakatisha, tunaomba umalizie tujuwe ilikuwaje, mbona unatuacha Dilema? umeishia patamu sana, na mke wako kwanini usimforwadie hii blog ili aone ushauri wa watu wanavyomshauri, mimi naamini kama mama Irene hapojuu anaweza akafanya cancelling kupitia humu humu na wengine tukafaidika, pole kwa yaliyokupata na hongera sana kwa kuamua kusamehe, mke wako ni wako tu, tena ndoa ya kanisani, nikama mmepeana rikizo tu, lakini ni wako, atakusamehe tu!
  AMINA

  ReplyDelete
 15. Dada angu pole, i can imagine the way unavyojisikia, mengi wamesema hapo juu, ila mi ushauri wangu jaribu tu kuwa mvumilivu, najua ni ngumu maana mapenzi yana nguvu kuliko mauti, but i believe God will see you through!

  ReplyDelete
 16. vumilia tu dada yetu, mapenzi yana mikasa mingi, na mizito, nakusihi vumilia tu, kila mtu akisema auweke mkasa wake hewani kama walivyofanya hao, hatutafika kokote kule, cha msingi kama alivyosema mama Irene tu! samehe, kisha toa moyoni kwako, muanze upya,
  nakuombea sana. mm pia nina mkasa mzito naona hata hiyo iliyoandikwa hapo juu ni midogo, hakuna ambae angeweza kuvumilia, sasa mimi kwakuwa namtumaini mungu basi nilimkabidhi yeye bila kuonyesha changes yeyote ndani kwangu na hatimae nimeyamaliza, kwa intro tu!
  NILIMKUTA BABA YANGU MZAZI AKIFANYA MAPENZI NA MKE WANGU KITANDANI KWANGU, NIKASAMEHE, NIKAKUTA BABA HUYO HUYO ANAFANYA MAPENZI NA BINTI YANGU NIKASEMEHE, Mungu ameshugurika,
  nawatia moyo wote mliopata matatizo kama mimi, kama bado manapendana sameheaneni tu! dawa ya ndoa ni msamaha! lakini ukiweka moyoni yatakuumiza, binadamu tunafanya mengi machafu, tusameheane tu!
  MAMA IRENE, toa cancelling kupitia humu utasaidia watu sana.
  JACOB
  uk

  ReplyDelete
 17. DHAMBI YA ANAEIBA 10,000/= NI SAWASAWA NA YULE ANAEIBA MILIONI, INAHESABIKA NI WIZI, HALI KADHALIKA DHAMBI YA MZINZI NI SAWA SAWA NA WEWE ULIETAMANI, Nilichojifunza hapa nikwamba watu wanaona uzinzi tu ndio dhambi, sio kweli, mnataka kusema nyie hamajawai kutamani, au ni vile hatumo mawazoni mwenu??
  MSAMAHA TU NDIO CHA MSINGI, SAMEHEANENI, MSAMEHE MCHUMBA WAKO, USIMUHESABIE KOSA, MPENDE KAMA ZAMANI, HIZO OUT HATA WEWE MTOE TU! MUWEKE KARIBU ATANYOOKA, ILA NAWE UKIENDELZA KIBURI YATAKUSHINDA
  USHAURI WANGU UTAFAKARI SANA
  MDAU REAL

  ReplyDelete
 18. Jamani mbona mambo ni mazito sana sana kila anayeelezea lake ni gumu kwanza kaka J naamini wewe umemshiba yesu ndiyo maana umeshinda jaribu ni ngumu mno mno kupita kiasi, mungu aendelee kukutetea, na kaka uliyemfumania mkeo na rafiki yako mtafute mungu iko siku mungu atafanya njia jaribu halikuumbiwa wanyama wala miti wala mawe ni mimi na wewe, na hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea, kila jaribu na mlango wake wa kutokea,Sasa dada mwenye mkasa na mchumba wako watu wanakushauri uwache hasira umsamehe, mimi swali langu je atamsamehe na kumuita je kama hamtaki si kama atakuwa anajipendekeza, hebu tulia dada mtafute mungu kwanza wala hawatafika mbali hao, unajua kipimo upimacho ndicho utakachopimiwa, rafiki yako atapimiwa tuu tena chake kijaa na kusukwasukwa, tulia mtafute mungu akikupigia sawa akiwa kimya na wewe kuwa najua ni ngumu, lakini unayaweza yote katika yeye akutia nguvu, muombe mungu akutie nguvu usimtukane wala nini kaa kimya kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho na pia ikitokea kakuacha mpe mungu nafasi huwezi jua mungu kakuepusha na nini? kwani ungekuwa ndiyo uko ndani ya ndoa, ungefanya nini vituko hivyo.na pia unapokuwa unaenda katika mafanikio shetani hachezi mbali na kazi yake ni kuuwa kuiba na kuharibu, usiumie moyo japo ni ngumu mpe mungu nafasi utashinda tuu vita ni vya bwana ushindi niwetu.
  mama Dear

  ReplyDelete
 19. dada kama wewe ni mkristo, napenda kukupa mstari huu wa kukutia moyo "BWANA YESU,NDIO NGOME YAKO NA KIMBILIO LAKO,JE MWANADAMU ATAKUFANYA NINI?? pia kumbuka kuwa "VITA YETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA,BALI NI JUU YA NGUVU ZOTE ZA GIZA, nguvu za giza kama hizo alizoleta huyo rafiki yako nina hakika hata kama dada yangu utaachana na huyo mchumba wako naye akaendelea na huyo rafiki yako hawatafika popote kwa sababu inaonekana tamaa imemkaa huyo mchmumba wako.

  Pole sana
  Kaka Jems

  ReplyDelete
 20. Jamani nimeguswa pia, nilivalishwa pete kama wewe na mahari juu, alivyonichenjia huwezi amini, at the end tulikuja achana, bt niliteseka sana na vituko na kuumia. Anaomba msamaha kesho unasikia yupo na mwanamke huyohuyo.Kikao cha wazazi kilikaa pia na akakubali kubadilika, lakini baada ya kikao mambo yalikua ni yaleyale. Mi kwa experience yangu, i think tulia kama baba mkubwa alivyosema, shusha mukali, no simu, msgs wala kumfuatafuata. Kama ni wako atarudi otherwise msahau inauma sana ila utapata mwingine. Nimeolewa sasa na mwanaume mzuri kuliko yule, nina amani na furaha. Mungu ni mwema na mwaminifu, hamtupi mja wake.

  ReplyDelete
 21. Asee!Pole sana dada mtaka ushauri.
  Nimejaribu kuvaa viatu vyako na kwakweli nimeyafeel maumivu yako ndani kabisa ya moyo wangu.Narudia tena kusema POLE. Nionavyo mie huyo mchumba wako si kuwa hakupendi na ndio sababu katika kikao na wazazi wake alikiri kukupenda na kuwa suala la ndoa liko palepale. natamani kusema ni utoto tu ndio unaomsumbua ya kuwa akikuwa ataacha lakini najua kama ni ukubwa tayari anao ila sijui ni nini kipo ndani ya akili yake? Kwakuwa una mapenzi ya dhati kwake nakushauri uendelee kumpa nafasi ila isizidi,na kama akitambua makosa yake na akakiri na kuomba msamaha huna budi kumsamehe na kuendelea naye,ila upe nafasi moyo wako na kuusikiliza kama kweli unamuhitaji bado kutoka moyoni na isije kuwa ni kwakuwa amekuvisha pete na unatarajia ndoa basi ndio ujishuuushe mpaka chini. Pia sio mbaya kumwonya kuwa uhuni katika maisha ya sasa sio deal kabisa atakufa kabla ya wakati hata kabla hajazifanyia kazi degree zake zilizoleta soo kwenye zawadi ya graduu.
  Ni hayo tu,
  Mumy Jnr

  ReplyDelete
 22. mdogo wangu pole sana kwa matatizo ulio nayo real inauma sana tena sanamimi yalishanikuta kama lako mbaya zaidi mimi nikiwa tayari mjamzito bwana we acha tu, nilitamani kufa nilikuwa nalia tu whole day kazini siendi but unajua nini kunasiku nilikaa nikawaza nikasema mimi ni wathamani sana mbele za mungu binadamu hawezi nitesa kiasi hiki niliamua kukaa kimya nikaomba mungu anisaidie kusamehe na nisahau na kweli kwa ushauri wa watu mbali mbali niliweza na muda si mrefu wakashindwa mchumba akarudi na ndoa tukafunga na sasa ninanpoandika nina mtoto tayari wa mwaka mmoja na miezi5, unachotakiwa sasa hv kwanza jaribu kutafuta muda wa kuongea na mchumba wako kwa faragha tena kwa upole hapo utajua msimamo wake maana asijekuwa anasema mdomo tu then moyoni hamaanishi then akikupa msimamo na wewe toa wa kwako mwambie wewe ndio uliemtambulisha kwa huyo rafiki yako then unaomba na hupendi waendelee kuwasiliana na uonyeshe msimamo wako dada huku ukimuomba mungu naimani ukisahame na ukasahau mungu huwa yuko upande wako na mchumba wako atarudi kwako, kaa chini fikiria uamuzi ulio bora kwako, tunatakiwa tuwaombee waume/wachumba wetu kila iitwapo leo majaribu ni mengi

  ReplyDelete
 23. pole sana dada marafiki hawafai kabisa mwombe MUNGU atakusaidia kwani ametuaidi ktk maandiko matakatifu kwamba atatuacha na wala hatatupukia kabisa na kwasababu sikio lake sio zito hadi hashindwe kusikia maombi yetu dada mlilie Mungu atajibu kaa zungumza nae kama haeleweki anza maisha mapya watashindana tu sababu hakuwa wake umri si kigezo mpenzi bado una nafasi ya kupata mme mwema.gud luck sister

  ReplyDelete
 24. Pole sana mdogo wangu mungu akutie nguvu. Hata Mungu mwenyewe anajua kabisa kuwa duniani kuna dhiki tujipe moyo kwani yeye ameushinda ulimwengu na mambao yake yote. Endelea kulia miguuni pa Yesu atakusaidia
  Naendelea kukuombea najua kwa jinsi inavyouma. marafiki ni wabaya sana. kumbuka kikulacho ki nguoni mwako

  ReplyDelete
 25. pole sana my sister najua unavyojiskia maumivu nafsin mwako jambo moja la msingi ni kujiuliza je wewe hujawahi kumtenda kama uliwahi basi mwombe msamaha kwanza

  ReplyDelete
 26. Pole sana my sister try to forget and then piga kazi mungu atakusaidia

  ReplyDelete