Wednesday, January 27, 2010

UNAJUA KAMA LIMAO /NDIMU NI DAWA YA KUKATA HARUFU KWENYE KWAPA?


Wakisema watamke mwanamke mrembo hawataacha kutamka usafi ndani yake, usafi na usafi unahitajika kwa mwili wote, sasa leo tuone hiki kisehemu kidogo, lakini kikiamua kutoa harufu, kinakufukuzia mpaka marafiki, (KWAPA) Wanawake wengi tumekuwa tukioga, tunapulizia perfume kwenye makwapa kwa wale wenye uwezo, ili mwakwapa yasitoe harufu, lakini utakuta pamoja na kupulizia perfum bado sehemu ya kwapa inaacha alama ya njano, teyari inapunguza urembo wako, mtu akikuona atajua kabisa wewe ni mchafu.


wengine wansema kuwa ni Ugonjwa, uende hospitali, lakini kuna rafiki yangu anaitwa BETTY ameniomba niwafahamishe dawa simpe na ni nzuri kwa kukata harufu, ni dawa ambayo hata mtu mwenye uwezo wa chini anaweza kununua, ni LIMAO AU NDIMU,
(Nanukuu)
Mambo dear, nimeona kwenye blog yako umeelezea kuwa tutakuwa tukifundishana urembo, n.k sasa leo mimi ninafahamu jinsi ya kutoa harufu ya kwapani bila kutumia perfumu,
1. unaoga unajikausha na taulo safi hasa makwapani,
2. unachukuwa Ndimu au Limao unakamulia kwenye mkono
3. unachukuwa yale majimaji ya ndimu unaanza kupaka kwenye kwapa,
kipingi cha kutumia limao /Ndimu pekeyake, huruhusiwi kutumia perfumu yeyote ile
unafanya hivyo kutwa mara mbili, asubuhi na jioni, na kwa wale wanaotoa harufu sana, basi wafanye hata mara tatu,
USISUGUE, itakuchubua, unapaka taratibu tu! wajaribu kwa muda wa siku tatu mfurulizo wataona mabadiliko na mashati hayataweka alama ya njano tena.
tupo wote, tutazidi kushaurina sana, tuzidi kuwa warembo.
kazi njema.
(Mwisho wa kunukuu)
 
hapa hatumaanishi kwamba tusitumie perfume, maana nazo zina raha yake, zinafanya unukie vizuri sana,
ila kuna wale wenzetu ambao wanatoa jasho sana, kiasi kwamba imekuwa kero hata kwao, waweza tumia malimao kukata harufu hiyo,  then ukishajiona uko okey, basi utaendelea kutumia perfumu,
many thanks to BETTY

9 comments:

 1. kwanza naomba nikupongeze kwa kutuletea blog ambayo kusema ukweli kabisa itatusaidia sana sisi kina dada, naamini tutabadilika sana, napenda wanawake wabunifu kama wewe,
  nami pia nimshukuru BETTY kwa kutuambia dawa hii, ambayo kwakweli nimesoma nimecheka sana, ni kama vile ameniona mimi, hadi siku hizi sinunui nguo nyeupe, maana zote zina alama, ninatoa jasho masaa yote, kikweli huwa nanunua kitambaa spesho kwa ajili ya kwapa, sasa dawa hii naenda kuinza leo hii hii nikirudi nyumbani, mwambie BETTY kama itanisaidia kweli, basi nitampa zawadi, maana nimehangaika sana, nimetumia dawa nyingi za hospitali, harufu inapungua lakini inarudi tena,
  MAMA Lily

  ReplyDelete
 2. hilo halina ubishi wala mpinzani hiyo ni dawa haswa huwa mimi natumia ila sasa mimi mama Dear nilikuwa mshamba kidogo nilikuwa natumia maganda nakamua likibaki ganda la ndimu au limau nasumugua na imenisaidia kweli sina tena kikwapa wala harufu, kumbe na maji ya ndimu au limau asante kutuelimisha
  mama dear

  ReplyDelete
 3. Asante kwa blog yako inaelimisha sana big up Dawa hii ni kweli me nimejaribu kabla ya kusoma hapa na nimepata majibu na nilipaka kwa siku mbili tu japo cina asili ya kunuka kwapa sana ila jua la siku hizi linakufanya utoe jasho sana so anony hapo juu dawa hiyo kwa kuongezea pia osha kwapa na maji ya ukoko wa ugali ukishapika ugali ukimaliza loweka sufuria na maji masafi then unapoenda kuoga unaoshea kwapa jizoeshe mara nyingi utaona mabadiliko kikwapa kinakera sana
  mama enjo

  ReplyDelete
 4. hahahaaaaaaaaaaaa
  toomuch jamani
  wewe mama enjo unatudanganya wewe, yani uoshe kwapa na maji ya ugali? mh! kama hivyo bora unuke kwapa kuliko maji machafu ya ugali
  umenichekesha sn
  hivi uko serious au unatudanganya?

  ReplyDelete
 5. habari mama Tracy

  Mimi naomba dawa ya kutoa jasho sana kwenye kwapa mana unavaa nguo ukitembea kidogo tu tayari kikwapa kimelowa huwa sipendi kama unajua dawa ya kumaliza jasho la kwapa naomba nisaidie tafadhali

  ReplyDelete
 6. mpendwa wangu hapo juu,
  namshukuru Mungu hali yangu ni Nzuri,
  kuhusu jasho kutoka kwenye kwapa, pia unaweza kutumia hilo hilo limao au ndimu, unajua limao ni dogo lakini linauwezo wa kukata harufu. sasa mimi nakuomba, ujaribu kununua limao au ndimu, kisha tumia maji yake kama tulivyoshauriwa na BETTY, Paka kwa hizo siku tatu au nne tena kwa issue yako paka kutwa mara tatu. halafu utaniambia kama itaendelea, mimi nina ndugu yangu mmoja, nae alikuwa anatoka jasho sana makwapani, alichafua nguo zote nyeupe katika makwapa zikawa njano kabisa, lakini alipotumia hii kwa muda wa wiki moja tu! hali ilibadilika, ndio maana nakushauri na wewe jaribu kutumia kisha utaniambia mabadiliko yake,
  siku njema.

  ReplyDelete
 7. dada violet
  kwenye intro yako umesema tutakuwa tukisaidiana katika ushauri, sasa mbona mimi nimekutumia mkasa wangu na nahitaji ushauri lakini hujautuma?? kweli nahitaji ushauri sana
  sana tu maana nahisi kuchanganyikiwa

  ReplyDelete
 8. Hello Ndugu wapenzi.
  Kuusiana na limao, ni kweli, limao ni dawa ya makwapa, na pia kwa wale ambao wanatoa jasho makwapani, limao ndiyo dawa peke.
  Shukura nyingi kwa Betty na Mwenzake, kwa kuelimisha jamihi kuusu usafi wa mwili.
  -Limao pia ni dawa ya kufifiza makovu ya mwili,(kama mtu aliuguwa upele) kukata limao, alafu kupaka maji wake mwilini, kupaka maeneo ya mwili ambayo yana makovu, uregeza ngozi ya mwili na pia ufifiza weusi wa makovu, na kumaliza makovu mwilini. Asante

  ReplyDelete
 9. Mama HELLEN.Nashukuru kwa ushauri dada,maana nilikua najisikia vibaya kwa kikwapa.Hongera kwa kujitolea somo.

  ReplyDelete