Friday, January 29, 2010

MKE WANGU NI MCHAFU SANA, NISAIDIENI KUMSEMA

Bila shaka hujambo Violet, Mimi ninashida moja kubwa sana ambayo inaniumiza kicha na kuninyima raha, shida hii ni uchafu wa mke wangu jamani, nina mke mzuri sana, nampenda sana, tatizo ni uchafu alionao, tuna watoto wawili, na yeye anamiaka 29, si mtoto kusema kwamba ashindwe hata kuusafisha mwili wake, yani hadi sometimes naona kinyaa kula wala kulala nae,
 
anaweza asitandike chumbani hata siku tatu, kazi ni kukung'uta kitanda wakati wa kulala, nguo utakapoiacha ndipo utakapoikuta, yani hadi huwa nawaza labda na pepo, halafu cha ajabu huwa haoni hata aibu, nimesema sana, hadi tunaishia kugombana na kunijibu kama naujuwa usafi nifanye mwenyewe,

 
yani haoni aibu kabisa, huwa namtolea mifano nyumba za dada zake zilivyosafi, lakini wala hana hata mpango kabisa, nimewambia dada zake wamseme, lakini haijasaidia hata kidogo, yani mimi sielewi tatizo hasa nini nini

vyombo vinaweza kulala kwenye sink hata siku mbili na wala asishtuke, hadi huwa namuuliza pua zako zina matatizo? mbona husikii harufu ya vyakula vimeanza kuchacha, kunasiku niliamu kufanya usafi mwenyewe, nikaingia hadi jikoni, nikakuta kule stoo sufuria limefunikwa, ile nafunua, limejaa funza wengiii tena wazima,
aisee nilimtandika mabao kwa hasira, nikajuwa kuwa tumeshalishwa uchafu
niliacha kula nyumbani kwa muda wa mwezi mzima, lakini hajabadilika kabisa jamani
sikua aliyoniudhi kupita zote ni sikumoja ambayoalikuwa mwezini, imefika usiku wakati tunalala nikaona amechukuwa nepi ya mtoto kwenye beseni akavaa kama pad, sikusema chochote, asubuhi wakat naenda kazini nikamwachia pesa anunue pad, jioni wakat wa kulala akavaa matambara yake tena, nikamwambia pesa  ya pad nilikupa mke wangu, kwanini unavaa matambara? akajibu ile hela amelipia kwenye mchezo, kuna mchezo anacheza na rafiki zake, sasa violet hebu nisaidie dada yangu, kuna wanawake wa hivyo au ni huyu wangu tu???? mbona mwenzenu sina amani, sitting room utakuta nepi za mtoto hata zenye mavi zitazagaa masaa hapo, yani hadi huwa naona aibu kuja na rafiki zangu ghafla, 
kina dada, hebu nisaidieni ushauri, nampenda sana mke wangu, tatizo uchafu tu!

13 comments:

 1. hi kaka pole sana sana na hali mbaya ya tabia ya wifi yetu, kama ni mkristo hebu mpeleke katika maombi unajua labda ana pepo la uchafu kama mpaka mwili wake hauthamini anaweza kuleta magonjwa ndani mkashangaa mnatapika na kuaharisha au hata kipindupindu, na kama mna watoto ni hatari sana kwa afya, na pia labda ufahamu umefungwa na uwelewa wake ni mzito. kama amefikia umri huo ni mtu mzima sio mtoto hakuna asiloweza wala kujua.mpeleke akaombewe unajua mke sio kitandani jamani, pamoja na usafi wa nyumba kujua kupika, kuangalia familia, na mambo mengine.Ngoja nikupe mf. labda unakuta mtu anakuwa anapenda kufanya ngono na kila mwanamme au na kila mwanamke na fika anajua kuwa kuna ukimwi na anasikia na mabango anaona, ukiangalia ni mzima mtu wa hivyo? ujue anapepo la ngono. Sasa labda na mkeo naye anapepo la uchafu kaka mpeleke katika maombi na yeye mwenyewe aamue kutoka ndani moyo kuwa nataka kubadilika na kuwa msafi sitaki tena uchafu kwa kumaanisha.Na pia kama mkeo alikulia nchi za ughaibuni ni tatizo kubwa sana nchi ughaibuni utakuta wasichana ni wachafu kupindukia uzuri wake ni nje tuu akikuvalia jinz na top utapenda lakini pad mpaka mlangoni kupika hajui sasa mwanamme gani anataka kula noodle za kupasha katika microwave, halafu unataka kuolewa lazima ujiandae na kuwa na sifa za kuwa mke bora, Mithali inasema mke mwema hujenga nyumba kwa mikono yake mwenyewe bali mpumbavu hubomoa kwa mikono yake mwenyewe, sasa asibomoe ajenge nyumba bora.
  Mama Dear

  ReplyDelete
 2. pole sana kaka angu yani kaka matatizo yako yapo kama ya kaka angu nae ameowa mke mchafu jamani hajui kujisafi kwa chochote.akiongea mdomo unavyotoa harufu hutatamani kumsemesha tena.ameonge we na kumpaa mfano hebu angalia nyumba za wenzetu labda kwa fulani au fulani,ndugu wifi alikuwa akiambiwa hivyo anamtukana kaka na kumwambia kama unaona hao ni wasafi si uwende ukalalenao hata akifananisha kwa dada zake yaani mimi au mama,anamwambia kamchukue basi huyo mama ako au dada ako anayejua usafi aje akufanyie na umlale tumetukanwa sisi bila makosa.mwisho kaka akaona isiwe tabu akampa likizo kwanza ludi kwenu mama sikutaki niache na nyumba yangu na wanangu acha hapa si wezi kuishi na wewe mchafu sana mwanzo alileta jeuri alitukana akaondoka kweli kaka alipobaki peke yake tukamuwekea house boy watoto mimi na mama tukawachukua eee bwana we nyumba ilikuwa safi hiyo mpaka kaka akabadilika kanenepa unajua ukiwa wakelwa na kitu hata afya haiji yule bibi cha kwanza kumludisha watoto mbona alipokuwa anakuja kwake mwenyewe alikuwa anaona aibu tena sana coz na sisi kwa kusudi akisema nakuja kuona mtoto tunampeleka kule kwa kaka ili aende kwake akaone.nakwambia alilia huyo kaomba msamaha sura imemshuka aibu kibao.kaludishwa ndani ni msafi huyo jamani huwezi amini kawa masafi tena sana yani tena yeye ndo kawa to much wanamtoto wa pili sasa mchanga yani tulienda kumuona anamwambia house boy kaka wawekee maji ya uvuguvugu kwenye sink kina mama wanawe wamshike mtoto.kaujua usafi kuliko maelezo.so na wewe mpe likizo mkeo mshenzi anakela mno

  ReplyDelete
 3. mpetalaka aende kwao akajifunze usafi hata hivyo kaka unamoyo wa kuvumilia mimi siwezi. mwambie kabisa bibi weeee naomba uende ukapumnzike kwenu kwanza nimechoka na uchafu wako nukta muondoe ila watoto mwambie marufuku hakuna kubeba.aweza kulisha mavi huyo sidhani hata kama akitoka kwa choo ananawa vyema ndo anaendelea na kazi zake aku babu muache mpe likizo kwanza

  ReplyDelete
 4. Huyu mwanamke huo uchafu kauanza kwenye kipindi cha kati au tangu mwanzo? Maana chanzo cha tatizo na lini limeanza ndio linatakiwa ili kutafuta njia ya kulitatua. Kama limeanza kwenye kipindi cha kati, basi atakuwa na tatizo la pepo la Uchafu, kwani pia kwa wadadisi wa mambo wanasema kuna pepo la uchafu na la usafi. Mtakiona mtu kapita tu ndani hata kama hajachafua yeye anaweza fagia au kukusafisha kochi au kiti. Mwingine hata uingie na matope ndani haoni shida. Kwahiyo ni swala la kulitibu kiroho kwakuwa kimwili limeshindikana, Kama umepiga na kumsemea kwa dada zake na hajabadilika. Kabidhi kwa Mungu tatizo lake.

  BABA MKUBWA

  ReplyDelete
 5. pole kaka yangu, huyo dawa yake mpe likizo aende kwao, halafu wewe weka houseboy, mbona atanyooka, mi mwenyewe nilikuwa mchafu haifai,mume wangu akanirudisha kwetu, ye akaleta houseboy, jamani mwenyewe niliona aibu, hta nilivyorudi kwa mume wangu alikuwa hatki nimwandalie chakula wala nini, kila kitu houseboy, mbona nilikoma lakini asaivi ni msafi mimi mpaka mume wangu ana raha, analetea marafiki zake, yan tuna amani, mrudishe kwao huyo hata c wa kumchekea.

  vivian

  ReplyDelete
 6. peleka kwao akajifundwe upya, mwanamke mazingira bwana au kama huwezi kukaa mbali na mkeo tafuta msaidizi wa ndani coz inawezekana pia majukumu hapo home yanamshinda tafuta msaidizi uinusuru ndoa yako. nihayotu kwa leo.

  ReplyDelete
 7. hhehehe mtafutie mwenzie huyo, utaona atakavobadilika, au weka kfanyakazi wa ndani, hlf uwe unampa favours, ataona donge na yy ataanza kuwajibika...kaaah inaudhi kwa kweli. pole kaka

  ReplyDelete
 8. mh pole sana kaka angu hadi unatia huruma ndoa ishamshinda mie sijaolewa ila mh anatisha sasa hata tatizo si kuchoka hadi pad inamshinda kuvaa huu si muda wa kuvaa matambara jamani mwambie aende kwao kwa muda akajifunze usafi tena maambie na ndugu zake pia wazazi wake utajakula visivyoliwa ukaumwa tumbo bure sasa hao watoto wakiota meno inakuwaje na wanvoendeshaga si ni mashaka kabisa rudisha kwao akajifuzne usafi

  ReplyDelete
 9. pole sana kaka na tabia ya huyo mkeo, binadamu kila mtu anakasoro zake lakini nyingine zinazidi we unaweka matambala aibu, kaka muombee hata mimi nina msalaba mkubwa tu ngoja niombe ushari wadau mnisaidie. jamani haya mambo sijui yakoje mimi mume wangu akioga asubuhi basi tena mpaka kesho tena, kibaya zaidi anataka tufanye mapenzi atakaporudi na harufu ya pombe na kikwapa cha siku nzima ndoa za siku hizi ni shida tupu watu tunavumilia, nywele hanyoi hata ukimwambia nikunyoe anakwambia siku nikiamua ntazitoa hiyo harufu unaisikia wewe mimi mbona siisikii, hakuna cha deodarat wala nini vyote havitaki mtu wa hivi unamfanya nini, mpaka nafikia hatua ya kutaka kutafuta bwana njee kwa sababu ninapolala naye namsikia akinuka jasho la asubuhi mpaka mchana, na ninapokuwa nimesafiri nakuta chupi zinataka kuwa rangi nyeusi madai yake hawezi kufua wala kusafisha bafuni tunapotumia watu wawili mpaka likizo nikitaka kuchukua huwa nawaza itakuwaje maana njoo nakikuta kina rangi pembeni nyeusiiiii, yeye ni kufrashi tu, chupi hivyo hivyo, hata sijui watu wa sample hii wanafanywa kitu gani maana sielewi mimi nahisi ndoa imenishinda siwezi kukaa na mwanaume mchafu mpaka kwenye mwili wake.
  Jack

  ReplyDelete
 10. pole sana Jacque,
  kitu ambacho naweza kushauri hapa ni kwamba huyo mumeo kinachomfanya awe mchafu ni hizo pombe zake,
  muombee tu! wanaume kama wamerogwa
  ah!

  ReplyDelete
 11. pole kaka ndo kubwa huo,cha muhim hapo usikate tamaa na wala usichoke kuongea na mkeo mweleze kwa utaratibu na mapenz jins unavyojisikia kuokana nahiyo hali yake ya uchafu,naamini kama utongea nae vizuri n kwa mapenz atakuelewa.

  ReplyDelete
 12. Pole sana Kaka,mimi naona kabla ya kuamua chochote,wewe jifanye kama mjinga,hizo kazi zake zote za usafi zifanye wewe,hata kama umechoka,kuwa kama kichaa vile.Tandika chumba vizuriosha vyombo,safisha nyumba,yaani kila kitu bila kumlaumu wala nini,fanya hivyo kwa kipindi cha wiki kama mbili hivi,ninahakika nyumba itabadilika gafla.Sasa basi lazima atajifunza kitu utaona anafavya mfundishe wewe,muonyeshe kuwa hata wewe unaweza,mtie aibu kwa njia hiyo.Mara nyingine kupiga au kuacha mke si suruhisho la matatizo,tena unaweza ukaanzisha matatizo mengine makubwa ambayo yanaweza kukukosesha amani kabisaa.Fanya hivyo hata kama ni ngumu,kweli atabadilika asipobadilika basi ujue anashida kubwa ktk ufahamu wake,hivyo hapo sasa uanze kuchukua hatua ya kumuitia watu wazima,si dada zake no! Wazee wale wenyewe,si unajua!wamfunde ki-ukwelii, asiposikia hapo,nakushauri umpeleke hospitali akachekiwe akili yake kama ni nzima.

  ReplyDelete
 13. kaka yangu pole sana ila ningekushauri umuwekee msaidizi sababu ungali unampenda na kuikoa family yako

  ReplyDelete