Wednesday, January 20, 2010

mwanamke akisuka nywele anatakiwa kukaanazo kichwani siku ngapi


Kuna wengine hadi miezi miwili au mitatu nywele ziko kichwani, zingine hadi zinatoa na harufu,

halafu pia tufahamishane je kukaa na nyweli muda mrefu kichwani hakuchangii kukatika kwa nywele kweli??
japo zinapendeza sana, na waweza kubana style yeyote ile,

9 comments:

 1. mh!
  wabongo tumezidi ubahiri
  wewe utakaaje na nywele miezi miwili mitatu jamani?? hata waseme? kwanza nywele zinaficha mambo mengi sana hadi kunuka na hata chawa waweza ingia, lo!
  mi staki
  JOYS

  ReplyDelete
 2. umejuajaje violet, mimi nina rafiki yangu ambae akisuka nyweli anakata miezi mitatu, ndio anasuka zingine, haendi salon wala nini, madai yake hela iende kihalali, mh! kazi kweli, ila kiuhalisia, style hii ya kukaa na nywele miaka, inakata nywele, kama hizi za kimasai, nyweli zinaisha kabisa, mwanamke suka nywele, wiki au wiki mbili then fumua,
  Mama Wini

  ReplyDelete
 3. jamani nywele kichwani miezi mitatu kwa mwanamke ni uchafu duh utawatia mafua wenzako usafi ni muhimu dada

  ReplyDelete
 4. Mmhhh jamani kukaa na nywele miezi miwili ni hatari na ni uchafu mkubwa sana kwa mwanamke anaejua nini usafi.

  ReplyDelete
 5. Naomba kuuliza na kutoka nje ya mada ni Hair Dressing Saloon ama Hair Dressing Salon kwani mie najua yenye double o ni ya gari, samahani kama nimekukwaza

  ReplyDelete
 6. asante kwa kuonyesha umakini wako katika kufatilia neno moja baada ya jingine, asante sana, ni kweli its a typing error, but im going to work on it.
  stay blessed

  ReplyDelete
 7. Jamani nywele kawaida ni wiki moja tu kwani nionavyo mimi mwanamke yeyote huwa anapendeza au kuonekana amependeza ikiwa tu kichwani kwake ni kuzuri yaani hair style yake awe amekata or kusuka huwa inavutia sana, ila wapo wanaokaa na nywele hadi miezi mitatu ukizingatia siku hizi kuna joto sijui hapo inakuwaje na ukija kufumua nywele zingine mpaka zinakatika kwa joto zinakuwa zimechoka.
  mimi kama mimi naona wiki moja tu inatosha
  Mama Mario

  ReplyDelete
 8. mnashangaa miezi mitatu tuuu??!! mi huu namaliza mwezi wa tano,na sina mpango wa kuzifumua! kinachotakiwa osha nywele zako kila wiki, utakuwa bomba tuu

  ReplyDelete
 9. hahahahaaaaaaaaaa
  miezi mitano? too much,
  lakini unajua madhara yake???
  ukija kufumua utakuta upara kama umetiwa wembe
  shauri yako

  ReplyDelete