Thursday, January 28, 2010

NGUO IPI .....???????? IVALIWE WAPI?..................................

 
hebu leo tuongee kuhusu mavazi yetu hasa kina dada,
na hasa mavazi ya ofisini, na pia tuelimishane jamani, ni vazi gani la ofisini??? ni vazi gani la sherehe? ni vazi gani simple tu kwaajili ya nyumbani? na mavazi mengine meeeeeengi, TUTAKUWA TUKIANGALIA VAZI MOJA MOJA, NA LEO TUTAANGALIA JUU YA MAVAZI YA OFISINI TU!
Vazi gani hasa kwa wadada linafaa kuvaliwa ofisini???Tuambie uonavyo wewe
 
Unaweza kuvaa suti yeyote ile na ukapendeza,



si lazima suti tu, unaweza kuvaa hata kiblauzi chako simple skirt or trouser  na ukanoga tu



kama hawa huyu kavaa simple na amenoga, huyu nae suti pia amenoga



but naona kama vile suti zinapendwa sana ofisini,



unaonaeeee, mrembo huyo nimependa sana alivyovaa, BELT linakwenda na SKIRT yake, blauzi inaignia kidogo kwenye hiyo rangi ya skirt, umeona kiatu kileeeeee, (nimekipenda sana) basi pale kwa pembeni unapiga pochi black, We  inanoga hiyo, usipime!!!!!



mh! hapo sasa,!!!!!!!!!! si umeona tofauti iliyopo? si kwamba hajapendeza, kapendeza sana, lakini hii ni yakuvaa ofisini kweli?  sema na wewe, unaonaje? ofisini tuvae vipi wadada???


7 comments:

  1. jamani vai mai dia hongera mno mpenzi hongera sana,kwa ubunifu wako mai dia...yani nimeona picha yako ulivyokuwa mbonge punguza mwili huoo shost.mmmh mwaego nisikuchanganyie mada niache watu wachangie.na hilo vazi la office. rafiki yako dom sec judd.

    ReplyDelete
  2. aka mwenzangu suti inanoga we!

    ReplyDelete
  3. watu wamezoea sana suti, kwahiyo tumeshakremisha, ndio suti inapendeza its classy, hasa kama unamikutano and the rest, but pia unaweza kuvaa kigauni kifupi, kisiwe wazi sana juu, kama kko wazi kuna vikoti vizuri tu vya ofisini unaweza vaa, soo gauni pia linafaa, but a simple dress, haina makorokoko, with high heels..pia inakubalika.

    ReplyDelete
  4. hi dada,
    pole na majukumu mpz.
    lakini hata kijitenge ukikishona vizuri like suite pia inapendeza ndugu yangu, tatizo watu wanashindwa kubuni mishono mizuri, utakuta mtu kashona mtenge mikono kama popobawa then aenda nayo ofcn utafikiri huko ofisini kwao kuna mashindano ya TAARABU.

    Cheers
    Mama wa Furaha

    ReplyDelete
  5. Watu wengi kwa ujumla hawajui kutofautisha jinsi ya kuvaa nguo, za ofisini, za kwenye sherehe, za nyumbani wala za weekend. Mtu utakuta amevaa dira ofisini, kweliii jamani!!!! Tujifunze kuvaa, hata hizo suti kuna nyingine zina urembo sana mi naona unaweza kuvaa hata kwenye sherehe na si ofisioni.

    ReplyDelete

  6. Hapa ndo kwenye ngondo hasa kwa akinamama, inabidi mavazi yetu yaendane na audience. usivae nguo ya bilicanas kwenye msiba..haipendezi.
    Asanteni

    ReplyDelete
  7. Tujitahidini kwenye mavazi ya heshima hasa tuwapo mabarabarani.

    ReplyDelete