Sunday, January 24, 2010

MACHOZI NI SULUHISHO LA MATATIZO YA MWANAMKE????


Wanawake wengi sana tumekuwa tukilia pindi tunapopata matatizo, tumeshindwa kuvumilia yale yanayotupata, mfano hai ni mimi mwenyewe, hadi wengine huniambia nina machozi ya promotion, hii pia nimeiona kwa wanawake wengi, unalia weeeeeeee, ukinyamaza unaona kama umeshatua mzigo kwa kiasi fulani, kama ni hasira basi unaona imepungua kwa sehemu,


utakuta mtu anatafuta na private place, anajifungia kama ni chumbani peke yake, analia kwa uchungu sana, na anaweza kuchukuwa muda mrefu sana kwa kulia,


but problem inabaki pale pale


hali hii humfanya mwanamke kuwa mpweke sana kwa muda mrefu,

mwingine hataki kubembelezwa hata kidogo, yani ukimbembeleza ni kama umemwambia azidi kulia


Mwingine akitoka kulia huwa na hasira sana, atapiga watoto, usimsemeshe, anaweza kukupa jibu moja tu, ukanyanyua mikono juu. Lakini tatizo linakuwa palepale, sasa hebu tusaidiane kushauriana juu ya hili, je inawezekana mtu kuiacha hali hii??? na utaiachaje? ili ukipata tatizo usilie tena???

11 comments:

  1. mh! bora kama tupo wengi, mimi nilijuwa mliaji ni peke yangu, aisee kulia kunasaidia sana kupunguza hasira, kuto kulia, kunamfanya mtu aujaze moyo uchungu, na moyo ukishajaa ndio ile pressure haziishi,mara moyo unaenda mbio, yani shida tu!
    ila mtu kama mimi nikiumizwa nalia weeeeeeee, nikinyamaza nimeshamliza naweza hata nisikuulize chochote wewe ulinikosea, ila nisipolia ujuwe kila nikikuona naanzisha ugomvi mkubwa tu!
    hivyo kama hasira zako unamaliza kwa kulia, bora ulie tu! sema issue ni kama ulivosema kwamba tatizo linakuwa pale pale but some how utakuwa umeshajipunguzia hasira kama ukilia.
    hahaaaaa nimecheka sana eti wanakutania una machozi ya promotion.

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ni kweli huwa mnahisi kulia kunawasaidia coz hata my ex alikuwa analia hata kwenye vitu vidogo...ila sometimes inaboa

    Soggy

    ReplyDelete
  3. we soggy wewe, hujatulia wewe, tena nyie wanaume ndio mnaopenda kutuliza, mnatuumiza sana, mwanamke ni wa machozi, ndio maana hata yesu alipopigiliwa msalabani wanawake ndio waliomlilia? Dada Violet, hii hali huwezi kuiondoa kwani ipo kwa kila mwanamke, wengine huwa ni majasiri, toka utotoni, hawatoi machozi, but most of them ndio kina sie, kulia sana. machozi mimi naona yanasaidia sana kupunguza hasira, ndio maana hata msibani, wanawake hulia sana kuliko wanaume,
    huwezi kuiepuka kwani ni kama alivyosema mchangiaji wa kwanza, kwamba ukinyamaza, basi ujuwe kabisa kuwa pressure itashuka, sababu moyo hautakuwa na uvumilivu.
    asante
    JOYS

    ReplyDelete
  4. Soggy umeonaeee kuwa wanaboa kuwa wanalialia tu hata kama ni jambo dogo. Unajua wanawake wanakosea jambo lakujipa nafasi ya kupenda na kufanya kazi. Sikumbuki ni kitabu gani kwenye Bible, kuna maneno kama haya " Mwanamke atazaa kwa uchungu na Mwanaume atakula kwa jasho" na kama haitoshi "Mke muheshimu mume na Mume mpende mke" Kwa maneno haya MUNGU alijua kuwa mwanamke hatoweza kukabiliana na challenge za dunia kwa ujumla wake. Hawezi kuvumilia challange za kutafuta pesa kwakuwa atakutana na watu wa aina mbalimbali watamkwaza na ataumia moyo wake. Na kwenye kupenda pia hawakutakiwa kupenda kwakuwa hawana moyo wa kuvumilia kero za kupenda, wao walitakiwa kuheshimu tu na maumivu ya Kupenda akabiliane nayo mwanaume kwakuwa ni shupavu. Kesi za kimapenzi hukuwa sana na kuzagaaa sana mpaka kwa wazee kama mwanamke amegundua mume ana mwanamke mwingine, ila mwanaume inachelewa au isifike kabisa kwakuwa anaweza kuvumilia.
    So acha walie kwakuwa wamekiuka maagizo ya MUNGU na kubadirika haitawezekana tena. Kikubwa tuwasapoti tu kwa kila jitihada za maendeleo ya kutafuta pesa na hata kujaribu kupenda.

    Ni hayo tu
    BABA MKUBWA

    ReplyDelete
  5. mh!
    mbona kulia ni poa tu! wanawake ambao hawalii ni wachache sana, hapa tu ninapoandika jana usiku nimeliaaaaa, hapa nilipo macho yamevimba??? na mtu akiniuliza nalilia nini tu! basi kilio kinaanza, yani hali hii inakuja yenyewe tu! sijui kwanini. baba .....aliniudhi sana jana, nililia sana, lakini sasa hivi nimeshamsamehe, kwakuwa nimeshatoa machozi,
    mwanamke kulia ni kawaida, haina haja ya kushangaa,
    mdau original

    ReplyDelete
  6. kwa mtazamo wangu mimi, kulia sio kutatua matatizo bali kutoa machungu, mimi huwa naliaaa, napata ahueni fulani hivi, thn ndo naanza kufikiria wat to do?? ila kunawanaolia tuuuu, hamna jingine zaidi ya kulia, hiyo sasa inakua ujinga, mwanamke lia nt unyamaze ukae chini ufukirie jinsi ya kutatua hilo tatizo.

    ReplyDelete
  7. mh!
    kulia kitu gani,
    no kulia hapa, tunabanana tu! yeye anamwaga ugali mimi namwaga mboga, ulie kitu gani? kwanza kulia ni dalili kubwa ya kushindwa, yanini ulie ujipunguzie maisha duniani,
    chakufanya violet na wote wanaolia kama nyie,
    kataeni roho ya kulia,
    pili jaribuni kudharau yale yanakuja kama makwazo kwenu kwani hata biblia inasema makwazo hayana budi kuja, tatu jipeni nafasi ndani ya moyo, hata aliekukosea asipotubu wewe msamehe tu! wanaume wenyewe ni kama hivyo, wanasema bora tuendelee kulia, cha msingi ni kudharau tu! yote utaona smooth kabisa.
    kwanini ulie, na mtu akigundua unapenda kulia lia, basi atakutesa sana, atakusumbua mno. kitu kidogo atataka ulie, acheni kulia, yani hata tatizo likuuma vipi, wewe dharau tu! usionyeshe kama limekuuma.
    jaribuni mtakuja kuniambia
    Violet nina mkasa wangu mmoja nimekutumia kwenye email yako, naomba uutoe ili nipate ushauri
    TUNAKUPENDA

    ReplyDelete
  8. Afadhali jamani mimi huwa nalia mno mpaka najionea huruma kitu chochote kile kikinitokea solution ni kulia naona ni afadhali nilie ndiyo napata nafuu kubwa tuu hata nikiumwa saa nyingine nalia huwa saa nyingine nasema mimi naona kama siko timamu vile. lakini ndivyo nilivyo wapendwa.
    mama Dear

    ReplyDelete
  9. mmh jamani wengi tunalia..mimi nikiudhiwa kitu cha kwanza ni kulia...ila nakua mwenyewe nitalia mpaka nikitoka hapo utanionea huruma...nahisi ni njia ya kuondoa maumivu ya moyo..ila kuna wakati naona kama nitakuja kupatwa ugonjwa kwa sabb ya kulia...nalia...na najua kulia .kuna wakati nilijipa ujasiri kwamba kwanini nilie..ila nilishindwa hali iko pale pale..KULIA tu !maana mambo yanayoniumiza moyo wangu ni mengi hata siwezi kuelezea kila nikiyakumbuka nalia..

    ReplyDelete
  10. Kulia kwa mwanamke ni kuondoa machungu tu ambayo yanakuumiza lakini sio njia ya kutatua hayo matatizo,inabidi tujikaze ili kukabiliana na hali hii.

    ReplyDelete
  11. Mbona kulia ni kawaida sana kwa mwanamke coz hata bible inathibisha hilo! lakin mie naona bora kulia kwa sababu machozi hutoa kinyongo moyoni! HUO NI MTAZAMO WANGU!!

    Priss

    ReplyDelete