Tuesday, May 31, 2011

NISAIDIENI JAMANI, MAMA MKWE WANGU AKIJA TU! AMANI NDANI INATOWEKA-NATAMANI HATA KUACHIKANisaidieni mwenzenu, niliolewa miaka 5 iliyiopita, ila mama mkwe wangu hakunipenda toka mwanzo, kwakuwa alikuwa ameshamuandalia mwanae mke wa kuoa, lakini mwanae akaforce kunioa mimi kwakuwa tulipenda sana, 

Sasa toka nimeolewa, mama hanipendi mimi wala kizazi changu, yani anachukia wanangu kiasi kwamba akifika watoto wananywea kabisa, na hawataki hata kulala nae, nilijaribu sana kujiweka karibu nae, lakini wapi!

Some times huwa anasusa hata kula,  anaweza  akashinda hata njaa, sasa mimi hali hii sijazowea, natamani kupatana na mkwe wangu kama ambavyo wengine wanapatana nao, lakini huyu wangu aliwahi kunitamkia kabisa kuwa sitakuja kukupenda mpaka nakufa,
Nilimueleza mume wangu, akasema wewe si unajua tatizo mama hakupendi toka mwanzo? ila mimi nakupenda sana, wewe tulia,  muache tu! Akae akichoka ataondoka, 
sasa nishaurini wapendwa, maisha  haya yananipa ugumu sana maana niko nyumbani muda mwingi, nashinda nae, nakosa raha kabisa, mara anitangaze nimemroga mwanae, wakati hata mganga simjui, mara mimi mchawi ndio maana mwanae haoni, wala haelewi, tena maneno haya anatamka kwa housegirl wangu, sasa kweli ni halali hii? na akija anakaa mwezi mzima, 

mwenyewe anadai amekuja kupumzika, lakini mbona hapumziki ila analeta matatizo tu! Nifanyaje??? Akifika tu! Amani ndani inatoweka. Sometimes huwa nahisi labda yeye ndio ana mambo ya kishirikina, maana kuna siku mwanae (mr wangu) alimlazimisha kulala na mwanangu wa kike ana umri wa miaka 4, 

mtoto usiku alilia sana, nilipoenda  kumchukuwa mama akawa mkali, cha ajabu hata kumbembeleza hambembelezi, anasema mmezowea kudekeza watoto, akilia tu mnambeba ukiangali ni usiku wa manane,  ilibidi nimchukuwe mtoto, nilivyomfikisha kwangu tu! Akalala, wakati siku zote huwa analala kule chumbani kwao pamoja na housegirl na wala hasumbuhi

Hali hii isikie kwa mwenzio tu! Ikikukuta unaweza kutamani hata kuacha mume ambae unampenda, nishaurini jamani

5 comments:

 1. Dada sali sana. Ukishasikia mama mkwe anakuhisi unamlogea mwanae ujue inawezekana anakuja kuwatembelea huku amefungasha mahirizi. Haijawahi kunikuta ila dada yangu alikuwa na similar challenge. Yaani ndugu za mumewe walikuwa wanaweka madawa kwenye msosi wao. Alipowagundua aliwatolea uvivu wakabaki ooh bibi katutuma ili familia yenu iwe na upendo. Akawauliza kwa nini mnafanya bila ruhusa yangu. Well ni long story, ila ikibidi mpekuege huyo mama mkwe akija kukutembelea. Usimwache mmeo pigana kike, utaacha wangapi?

  ReplyDelete
 2. Pole sana kwa hilo. Dawa yake muambia unaweza kumuamchia mwanaa, na ukaenda kuolewa na mwanamme mwingine, kwani mwanamme ni yeye tu dunia hii. Muombe mungu. kama mkristo nenda kanisani, kuwa mtu wa mungu, utashinda. Kama muslam anza kuswali, muombe mungu utashinda. Tumia muda wako kuenda nyumba ya mungu kila siku, au akija karibisha nawe wazazi wako, au sister zako. Nazani utajiskia amani. Muache kama alivo. muambie, wewe unaweza kumuacha m

  ReplyDelete
 3. pole sana dada hayo ndio majaribio ukisikia majaribu ndio hayo mume mnapendana mama mkwe ambaye ni kama mama yako ambaye angetakiwa yeye ndiye azidishe upendo ndani ya nyumba kwakukupenda wewe na wajukuu zake imekuwa nikinyume dada nikuambie kitu mimi sijui wewe ni dini gani unajua shetani hatakikuona watu wakipatana au wakipendana unajua hakuna linalomshinda Mungu alimradi tu umwamini na kumtegemea kwakilakitu kama wewe ni mkirsto funga na kusalihata washirikishe watumishi wa mungu piga magoti mlilie Mungu wako atasikia kilio chako na atarekebisha ndao yako itakuwa na Amani maana shetani amepitia mahali pabaya na unapoendelea kumwomba Mungu usijekumchukia mama mkwe wako zidisha mapenzi kwake hata kama yeye anakuchukia usijibishanenaye hatakidogo na kuhusu uchawi yoote muachie mungu maana kama mungu hakupanga hata kama ni mshirikina au mchawi hakufanyi kitu na wala watoto hawezi kuwafanya kitu mtegemee mungu atakushindania na kukuepusha na mabaya narudia tena usije kuonyesha chuki yeyote kwa mama mkwe wako japo ni ngumu lakini kwa Mungu yote yawezekana usilipize ubaya kwa ubaya bali ushinde ubaya kwa uzuri laiti kama ungefuata haya ninayokushauri siku moja ungerudi hapa kutoa ushuhuda kwamba umefanikiwa good luck

  ReplyDelete
 4. Pole sana ndugu yangu! Hii ishu huzikuta familia nyingi sana kwa sababu ya wivu ambao hauna hata maana! Hivi huyo Mr wako baba yake bado yupo hai? Maana pia inawezekana huyo mama kamchukulia mtoto wake kama mume wake yani anaona wivu wa Mr kukupenda wewe na pia anataka kuwa in control. Ila pia inaweza ikawa ni historia inajirudia, labda na yeye alifanyiwa hivyo na mama mkwe wake. Yani kiini cha kukuchukia wewe lazima kinazidi tu kutaka mtoto wake amuoe huyo msichana mwingine.
  Mimi sijaolewa ila pia naelewa umuhimu wa familia kupendana. Kumbuka uliapa ni kifo tu ndicho kitawatenganisha wewe na mume wako naomba usikate tamaa. Na ni kweli kama alivyosema hapo juu mtu mmoja kuwa utaacha wangapi? Na pia inabidi uwaze na watoto wako, kulelewa na baba yao ni muhimu sana.
  Hakuna binadamu anayeweza kukusaidia kwa hili, ila tu ni Mungu! Unajua hakuna kitu chema kama mama kumcha Mungu. Kuna mengi utapigana nayo ila matunda yataonekana. Hapa naongea from experience, yani familia yenye mama anayemcha Mungu bwana we acha tu! Kila familia ina matatizo yake na ndoa pia, na hayataisha ila tuna Mungu anayeelewa yanayotutokea. Hakuna binadamu aliyekamilika, kwahiyo ni Mungu tu wa kumkimbilia. Tafuta wanawake au kina mama ambao unaweza kujiunga nao katika maswala ya maombi. I mean serious people, kusali na watu nako ni kuzuri maana nguvu inaongezeka. Usipoteze muda kumfurahisha binadamu maana it's vanity. You can never please a man enough. Una kila sababu ya kufurahia maisha yako. Mungu akulinde na familia yako pia. Kila la kheri.

  ReplyDelete
 5. pole sana dada, mimi nimeolewa nna mwaka wa 12 sasa, mimi ninavyo amini sio lazima mama mkwe akupende au wewe umpende! unajua wewe ndo uliependana na mumeo mpaka mkaoana so sio lazima wa kwao(his family) ikupende! wala sio lazima wewe uwapende kumbuka uliempenda ni mumeo tu mlipokutana, kutokupendwa na yy isikuumize kichwa kabisa coz mie naamini mama mkwe angepewa chance ya kumchagulia mwanae mke angemtafutia msichana ANAEMPENDA yeye, wifi zako vilevile!so sio lazima upendwe nao!ofcoz ukiolewa unatakiwa kuwapenda ndugu wa mimeo kama wako but kama haijawork dont force it!wee chakufanya waheshimu, tambua uwepo wa mama mkwe akija kukutembelea maswala ya kutaka ukaribu nae achana huko!kumbuka mama mkwe will NEVER be like your mama!
  Mwombe Mungu atakusaidia, achana na mawazo ya kutaka kuacha mume kisa mama mkwe!embu asikupe shida tena shukuru upo hme muda mwingi you can watch your kids wasifanyiwe vibaya ungekuwa kazini je? kama wtt ni wakubwa like hyo wa 4yrs mwambie asikubali kufanyiwa kitu kibaya/asichopenda na bibi yake na kama bb atalazimisha aje kuripot kwako!na wewe simama kwa wtt wako hata kama ni bb lakini kumbuka mtt akipata tatizo ni wewe utakaehangaika nae milele, ndugu huwaga wanaishia kukupa pole tu.

  ReplyDelete