Monday, May 2, 2011

ALINIDHARIRISHA SANA- SASA ANATAKA TURUDIANE, ANANIFAA KWELI????

Mimi ni mdada ambae sijaolewa, ila nina mpenzi wangu ambae tunapendana sana, yeye kwa sasa hana kazi, mimi ndio huwa namsaidia akiniomba msaada wa hela nampa, cha ajabu dada yangu, ilikuwa jmosi moja alikuwa anakunywa na rafiki zake, akaniita niende, nilikuwa nimebanwa na kazi lakini nilijitahidi nikaenda,

Baada ya kumaliza akaniambia tukaenda hadi kwao kwanza. akasema lazima nilale nae, nikamwambia haitawezekana maana nilikuwa tight sana, alikataa, nikataka kuondoka kwa nguvu, kinachonishangaza akabadilika gafla na kuanza kuongea kwa sauti, " umekula hela yangu nilipe nilipe, nikamuuliza Tshs ngapi?, akasema elfu 20,000, nikaona hali inakuwa mbaya maana alikuwa anaongea kwa sauti kiasi kwamba watu wakaanza kukusanyika, ikabidi nitoe 20,000 nikampa, wakati sijala pesa yake yeye ndioa anakula za kwangu,

akasema bado ingine, na kama simpi nimuachie simu yangu yenye thamani ya 250,000, akaanza kuropoka mbele ya wazazi wake, anongea kwa fujo sana, na vitisho  

anasema " leo nakukata panga kama ujatoa hela yangu", Mama yake na Baba  wakasikitika sana alivyokua ananifanyia Kijana wao, mama yake akaniambia niondoke,

 baada ya wiki 1 akanipigia simu akiniomba msamaha, ukweli moyo wangu unawoga nae sana dada. najiuliza ipo siku atanifanyia kama alivyonidhalilisha, Je mtuu huyu ana mapenzi na mimi, kweli?, naomba ushauri wenu Ndugu zangu.

Samahani dada Violet kwa ujumbe mrefu,  Naomba jina langu liwe kapuni, , Kazi njema Dada.

11 comments:

 1. Hiv unahaja hata ya kujiuliza hapo! hakuna mapenzi hapo, pesa na mwili wako ndo anavihitaji, kimbiaaaaaaaaaaaaa!!!!

  ReplyDelete
 2. we dada, mimi naakushauri achana kabisa na huyo mwendawazimu, hakupendi hata kidogo, shauri yako, wewe nenda tutasikia umepigwa panga la ukweli, maisha yako ni bora sana, huyo hakufai kabisa, achana nae msamaha wake ni wa kinafki, na akija tena mtemee na makohozi mshezi huyo
  ANITA

  ReplyDelete
 3. au alikuwa amelewa?kama alikuwa amelewa maybe ni pombe,ila kama alikuwa hajanywa huyo si mwanamme,atakutu use mpaka utajuta,angalia usipoteze muda wako mwa mtu ambe hajui thamani ya mapenzi

  ReplyDelete
 4. jamani duniani kuna mambo, kimbiaaaaaaaaaaaa shoga

  ReplyDelete
 5. USIMKUBALIE MPUUZI HUYO, MPIGE CHINI

  ReplyDelete
 6. wala unahaja kuomba ushauri wewe mwenyewe ungeamua huyo hakufaii hata mara moja asizingizie ulevi maana hiyo pombe sijui kama ataacha mwache mara moja emekudhalilisha sana mbele ya wazazi wake wala hii kitu usifikirie hata mara mbili tafuta ustaarabu mwingi ukirudiana naye siku nyingine atakuua kabisa aseme pombe tafuta mchumba mwingine maana wanaume hawajaisha duniani tena huyo anaonekana ni mshamba sana hajui maana ya penzi

  ReplyDelete
 7. Mh! Pole sana dada, kama walivyokushauri hao waliopita mpendwa usikubali kurudiana nae hata iweje, jali maisha yako, kuna watu wengi sana wanakutegemea wakiwemo wazazi na ndungu zako.
  Kama mwanaume utampata tena mume wa maisha yako ambaye atakujali na kulithamini penzi lako, piga goti muombe mungu wako kila kitu kitakuwa sawa. Hata kama ni kumpenda utamsahau tu kwani ni wangapi wameachana na marafiki zao wa kiume na wanaishi tena kwa raha???
  Asije akakulaghai eti alikuwa amelewa, mlevi anajijua asikwambie mtu, na mara nyingi mlevi anayetukana mtu anakuwa amedhamiria kabla ya kunywa kwahiyo anakuwa amekunywea au zinakuwa ndio tabia zake vinginevyo mlevi wa ukweli huwa hatukani, akilewa analala zake kama gogo.
  Pole sana, usijali hiyo elf 20 haitampeleka popote sanasana nayo ilishaisha isha kwa kunywea, fanya kazi yako, angalia maisha yako na mungu atakupa mwanaume wa maisha yako.

  Amanda

  ReplyDelete
 8. Dada poleh ,vijan wa type hiyo ni wengi mjini wanataka mteremko wadada wa mujini wanaita Slope km anashuka mlima ,Yuko kifedha zaidi na hna penzy la dhati na kukupa uchafu wake basi midume ya hivyo kujidai na miwivu mamdogo tambaa utakuwa huna maendeleo kulisha jitu mmekutana ukubwani Eboooh

  ReplyDelete
 9. Yaani unafikiria kabisa kulisamehe hilo lishorobaro. Kwanza nadhani ni mtoto wa mama maana anakaa kwao. Wa nini? Chapa lapa hilo ni jambazi tu.

  ReplyDelete
 10. HUYO HAKUFAI HATA KIDOGO TENA HANA HESHIMA MBELE YA WAZAZI?

  ReplyDelete
 11. pole mpenzi achana na huyo mwanaume ndio tabia yake hiyo asije akakudanganya ni ulevi.mi yalishanikuta hayo nikasamehe lakini baada ya muda hali inarudi upya.mr.right mbona wapo wengi tulia omba Mungu mr.right anakuja utakula raha mpaka utamuuliza alikuwa wapi kipindi unapata shida.

  ReplyDelete