Thursday, June 2, 2011

NINAWASHWA SANA SEHEMU ZA SIRI, MADAKTARI WAMESEMA SINA UGONJWA, NIFANYAJE

Hi dada Violet, kwanza nakupongeza kwa blog yako nzuri, blogu inayotusaidia sana, Mungu akubariki dada, pia naomba ufiche kabisa jina langu na email address yangu,

Mimi ni dada/mama mwenye umri wa miaka 20, najiita mama kwakuwa nimefunga ni mke wa mtu, ninatatizo la kuwashwa sana sehemu zangu za siri, yani dada violet huwa najikuna hadi navimba, wakati najikuna huwa nasikia rah asana, ili nikishaanza kuvimba huwa Napata maumivu makali sana,

Nilimshirikisha mume wangu juu ya tatizo langu, tukaenda hospitali, nilipima vipimo vyote nikaambiwa sina ugonjwa wowote, wakasema labda maji ninayotumia kunawa si salama,  nikawambia ninatumia maji ya bomba, na tena huwa natumia ya moto,

Hali hii inaniumiza sana mwenzenu, sina raha kabisa, kuna kipindi nilijikuna hadi damu zilitoka, naanza kuuguza jeraha, hakuna uchafu wowote unaotoka, sasa jamani wamama wenzangu nisaidieni, hili tatizo lina mwaka mmoja sasa,
Natarajia ushauri wenu sana, na mungu atawabariki wote
                                                                 

10 comments:

 1. Dada pole sana mimi nibinti mwenye umriwa miaka 20 nilipatwa na tatizo ka lako nili umia sana unavyosema nihivyohivyo ndivyo nilikuwa nikisikia ila nilipona kunadawa moja nilitumia kwa jina nimelisahu kido nakumbuka tu kuna shemu imeandikwa vagna cream ila kesho nakuahidi nitakutumia jina kamili la hiyo dawa naninaamini hata wewe itakuponesha pole sana ila fahamu kuwa tatizo lako limefika mwisho

  ReplyDelete
 2. mkazi wa g/mbotoJune 4, 2011 at 8:51 PM

  utakuwa na fungus wanaoitwa candida,hivyo unatakiwa kununua cream ujipake huko kwa bibi.Vilevile inawezekana kuna hormones zinasababisha hivyo hivyo we nenda duka la dawa kachukue hiyo cram jipake na uhakikishe uwe mkavu muda wote huko kwa bibi.

  ReplyDelete
 3. pole sana dada,... utakuwa na fungus huko chini... yawezekana ule ute wako unaotoka kuna saa ukinawa unakuwa kama maziwa ya mtindi hivi kidogo jaribu kunawa ukiwa unaingiza kidole kujisafisha utaona... lakini kama siyo hivyo, bado utakuwa na fungus tu... unachotakiwa kufanya ni kwenda pharmacy.. ulizia dawa ya fungus kwa wanawake nafikiri inaitwa viginal cream,, na pia ina vidonge vyake ambavyo utakuwa unaviingiza huko chini kwa siku sita kila siku bila kushiriki tendo la ndoa, na cream yake utakuwa unapaka juu kuanzia kwa chini huko kwa bibi,.. mpaka juu kwenye mashavu yote.. ni vizuri ukaitumia usiku hasa ile ya kuingiza ambayo ni vidonge ukiwa unaenda kulala ndio inafanya kazi vizuri mana unakuwa hutembei, .... kwa hiyo kile kidonge ulichodumbukiza kule chini hakiwezi kutoka.. utapewa na kibomba cha kutumia kuingizia kile kidonge huko chini..hakikisha usichelewe sana kulala angalau saa tatu usiku ili ukikiingiza kiweze kufanya kazi vizuri.. mana ukichelewa kukiweka asubuhi ukinawa utakuta hakijasagika vizuri.. ila cream yake unaweza kupaka kutwa mara mbili kama wewe ni mfanyakazi.. ukioga asubuhi mda wa kwenda kazini paka.. na usiku ukishaoga wakati wa kuingiza kile kidonge ndio upake na hiyo cream yake. hakikisha ukiwa unatumia uwe umeshaoga. Nakutakia kila la kheri na utapona kabisa usijali... ukiona inajirudia uwe unatumia mara kwa mara at least kila baada ya miezi 3 itaisha kabisa na utasahau...

  ReplyDelete
 4. hata mimi hiyo hali ilinipata lakini mimi ilikuwani pembeni pembeni nilikuwa nawashwa najikuna na kutoa uchafu mwingi nilinunua dawa inaitwa Dactarin imenisaidia kwa kiasi kikubwa sana.jaribu hiyo

  ReplyDelete
 5. POLE SANA DADA HIYO ITAKUA NI FANGASI JARIBU KWENDA KWA MADAKTARI WA MAGONJWA YA KINA MAMA WATAKUSAIDIA KULIKO KUTUMIA TU DAWA

  ReplyDelete
 6. Uliwahi kumuona docta bingwa wa maswala hayo? pole sana! Kwa ushauri wangu tumia hizo cream ulizoshauriwa, lakini jambo likiwa gumu, musiogope gharama, waoneni wataalamu bingwa, ikishindikana zipo dawa za kinyeji!

  Mpendwa mwenye blog hii, nafikiri ni mara ya kwanza kuingia humu, nakufagilia kwa blog yako hii nzuri, yenye kusaidia. TUPO PAMOJA DAIMA, HII NDIO KAULI MBIU YA WANABLOGS

  ReplyDelete
 7. Habari dada pole kwa kuchelewa kukutumia jina halisi ya hiyo dawa inaitwa GYNOZOL vaginal ream ninzuri na itakuponyesha nenda duka la madawa na watakupa maelekezo ya kutumia na endapo utapona naomba utufahamishe

  ReplyDelete
 8. asanteni wadau wote tulimshauri huyu dada, kwa niaba yake naomba niwashukuru sana, na amepromise kurudisha majibu kama dawa tulizomshauri zitakuwa zimemsaidia, maana tatizo hili amelichoka sana, pia nikukaribishe rasmi EMU-THREE kweny blogu yetu, kwa niaba ya wadau wa blog yangu wooote, tunakukaribisha sana,
  MBARIKIWE WOOTE,

  ReplyDelete
 9. dada uko juu naomba kukufahamu zaid unafanya kazi wapi maana nimetokea kukupenda tu. i love u sana na huo unywelw wako mhhhhhhhhhhhhhhh

  Rachel/Mama bm

  ReplyDelete
 10. Mimi ninamatatizo kama hayo nimeenda hospitali. na nimepewa dawa inaitwa CLOTRIMAZOLE CREAM ANTI -FUNGAL SKIN TREATMENT lakini niko nje ya nchi

  ReplyDelete