Monday, March 28, 2011

NIMECHOKA SANA, TUNAISHI KAMA MAADUI, HAKUNA MWENYE AMANI NA MWENZIE, NIFANYAJE

Jamani maisha yangu ya ndoa yamenishinda, adui yangu wa kwanza sasa hivi ni mume wangu,  hatuna amani, kitu kidogo tu anaweza kukukasirikia hata wiki nzima, haongei wala kushirikiana na wewe chohote, watoto wako boarding so nyumbani tuna house girl tu, unakuta hata kama nipo, hanitumi mimi anamwagiza housegirl wangu, hapa nilipo nawaza kumtimua, lakini kazi kwangu ni nyingi, namimi sina muda wa kufanya kazi zooote,

Yeye anabibi nje, naamini hivyo maana hata siku tukibahatisha kufanya mapenzi,  na unakuta tumekaa hata wiki mbili bila kugusana, siku tukikutana, anaweza nifanya mimi nikapiz hata mara tano, yeye akawa bado na kama akija kupiz basi ni kidogo sana, tofauti na mwanzo, tukikaa siku nne tu, akiweka ni dk 3 anapiz na anapizi za ukweli haswa, sasa huyo bibi yake wa nje ndio anipe tabu ndani??? 

Kwanini anipige pige hovyo??? kwanini ujinga wake asiufanyie nje na akarudi ndani na heshima?Kitu kidogo makofi, ananiaibisha kwa majirani zangu, dharau ndio usisem
Nisaidieni, au nikae nae mbali sana iwe kama rikizo kwetu, baada ya muda nirudi atakuwa amejirekebisha? Ah! Nimechoka jamani, nimechoka sana na huyu mwanaume7 comments:

 1. pole mpenzi wanaume wote ni baba mmoja mama mmoja lakini cha muhimu angalia kazi yako kama una kazi usiangaike naye maana atakuumiza kichwa muombe Mungu wako akusaidie katika kazi zako mawazo yako hamishia kwenye mambo ya kukuletea faida na siyo yeye tena

  ReplyDelete
 2. Funga mkanda simama kama mwanammke mimi ni mama sasa na mtoto niko kwenye ndoa miaka 9 tatizo ambalo liko kwa wazazi wangu ya ndani hatujuia matusi ya nguoni na kumpiga makofi hadharani, imenifanya nimchukie sana baba yangu mama yangu ni mpole sana sana imefika hatua tukaona kila mtu akae kwake lakini head girl wetu akamchombeza mama wakarudiana ikawa shida kweli imefika hautua nimemripoti police imi binti na nimemwambia mama tulia kimya tuntengeneza huyo mzee ni story ndefu turudi kwenye mada

  Sasa wewe simama na mkalie koon kama anamwanamke kwa nini kukupiga hovyo na kukudhalilisha kidogo anaanza mwisho wake itakuwa atakutia kilema usichoke kutokuktuma wewe isikusumbue bbwana zaidi tafuta eneo la maombi upate amani yako kwanza na huo dem wa nje isije ikwa kafanya nguvu za giza

  ReplyDelete
 3. Pole sana mpenzi. Usichukulie hasira, hebu piga goti chini umwombe Mungu akusaidie. Maana wewe peke yako hutaweza kukabiliana na hili, Mungu peke yake ndie anayeweza kukupa jibu, Mungu anajibu maombi! Maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu, mtazame Mungu wakati wote, mwambie aiponye ndoa yako maana shetani anataka kuisambalatisha.Mwambie Bwana Yesu aingilie kati, usiache kuomba endelea kumtazama Mungu ipo siku atajibu maana yeye anasema ombeni nanyi mtapewa, bisheni hodi nanyi mtafunguliwa, usikate tamaa kwani yeye ni mwaminifu!

  ReplyDelete
 4. Ni lazima kujua ama kuzingatia kwamba wote ni binadamu wenye mapungufu mbali mbali.Kwa maana hio upungufu kwenye mahusiano yenu unaweza kuwa pande moja au zote mbili.Ni vizuri kuchunguza kitu gani kimepungua katika mahusiano yenu kwanza kabla ya kunyoosha kidole kua huyu ana haribu pale.

  Kazi ni muhimu sana lakini isifanye ukasahau ndoa yako.kuna mahali umesema unafikiria sijui umtimue au laa (hii inasema mengi zaidi na pengine baadhi mumeo amegundua kwahio ana kukomesha)

  Ushauri wangu zingatia kazi kwa sasa na mpango mzima wa kulea watoto kama ni mtu aliyekomaa kiakili atajirudi na kujiona mshamba au mjinga all together.Pia jitahidi kubadili mfumo wako wa maisha hata kama uko bize na kazi (wanaume wengi akiona huna attention nae ana assume na wewe huko kazini kuna mtu anamsaidia coz hayo mambo yapo sana).

  Ishi kawaida bila kuonyesha hasira na kujiweka vizuri na ikibidi mkifanya mapenzi tumieni kondomu kama kuna dalili ya kutoka nje ya ndoa.Itambulike kua maisha ya ndoa yana mitihani mingi lkn ukiwa na msimamo utashinda.Kwasasa mawazo zaidi yawe kufanya mambo yamaendeleo na si kufikiria ngono au yeye kanuna muda wote.Na kwanini hamuongei (mawasiliano ni kiungo muhimu sana katika mahusiano kuondoa tofauti na kujadili mipango ya maisha ikiwemo kulea watoto,miradi ya familia n.k)

  Hio ya kumtumia Housegirl kwa mambo yake wakati wewe upo inatia wasiwasi.Ni lazima mtafute suluhu si jambo la kawaida kumsusia kiasi hicho umpendaye kwa dhati.Ni hayo tu kwa leo kila lakheri!

  ReplyDelete
 5. Hivi wanawake wengine mkoje? Mbona mnakuwa ving'ang'anizi, kama anakuletea za kuleta na wewe una kazi yako, mpotezee. Halafu haya maisha ya kupeleka watoto wote boarding na kubaki nyie wenyewe kama mko kwenye fungate halafu fungate linawashinda siyo mzuri. Watoto huwaunganisha wazazi wanapokosana, kwani mtoto anaweza akaongea kitu mkajikuta wote mna-share nae na kusahau kama mlinuniana. Nyumba ni watoto!!

  ReplyDelete
 6. MWAYA POLE, HAYO MBONA KILA NDO YAPO ILA WATU WANAVUMILIA KWA SABABU HAWAHITAJI WATU WAWANYOSHEE KIDOLE, WE KAZA BUTI NA WATOTO NA KAZI PIA KINGINE JIWEKE SMART ZAIDI, UONEKANE MREMBO KILA WAKATI AKIONA HVY ATAJIBADILISHA

  ReplyDelete
 7. Mafundisho yako mazuri na kama wanawake wakiyafuata, wataokoa ndoa zao.

  ReplyDelete