Tuesday, April 5, 2011

INAPOBIDI KUJISHUSHA KINA MAMA TUJISHUJE JAMANI- TUACHE VIBURI ILI NDOA ZETU ZIPONE


Wapendwa wangu leo nataka tuongee kidogo, pamoja na kuwa mikasa imekuwa miingi sana, nimeona ni vizuri kama tutashauriana pia ili tuone kama inawezekana kufanya hiyo mikasa kwenye ndoa zetu isitokee,

Katika mikasa mingi sana inawahusisha wanandoa, hasa wanawake,  mara mume wangu nimemfumania, mara mume wangu kiburi, mara mume wangu mchafu na mengine mengi, lakini je hatuwezi sisi kama kina mama kuangalia ni jinsi gani tunaweza kufanya ili kuzuia? na pale yanapotokea basi iwe imebidi yatokee??? lakini sisi tusiwe chanzo

Tushauriane kwa pamoja, tufanye nini ili tupunguze hii kasi ya machafuko kwa wanandoa, nina amini kabisa kama kila mtu ataplay part yake kama mama mwenye hekima basi 80% ya ndoa zetu  zitakuwa zimepona
(i) KUNUNA KUSIPITILEZE.
Kununa imo, lakini sio nongwa jamani, mtu ukinuna basi ndio lo!! Mwezi mzima, sasa tujiulize tunaponunia waume zetu mwezi mzima tunategemea nini??? Kama ana hamu na wewe si atapata nafasi ya kutoka nje? Maana akirudi home anaona kero, mama kanuna, tena wengine bila hata haya wanawambia watoto baba akija msimuamke mkalale, kha! Baba lazima ajiulize hivi kuna haja gani ya kuwahi nyumbani, bora nikae bar niliweeeeeee, matokeo yake anaanza kurudi usiku amechoka baba wa watu,  na anarudi tu! kutimiza wajibu
 
Pale inapobidi kukasirika,  yes! Show him kwamba hapa umekosea, ili nae ajuwe asikupande kichwani,  kama umeamua  kumtingisha kwa kununa basi huo mnuno wako uwe na kiasi, sio ndio kila akikusemesha umevuta mdomo, jamani tusipoangalia  tutazipoteza ndoa zetu wakati bado tunazitaka, 
pia tukumbuke katika yale mambo serios lazima tuwe serios kweli, mfano kuna mmoja alisema ameambiwa aache kazi,  dada huyu anaweza kukaa namumewe kwa upole na upendo akamwambia tu! kwanini niache kazi? asikilize hizo sababu, ili nae apate muda wa kujitetea, pengine kazi inamtia kiburi anasahau majukumu yake kama mama ? pengine baba hapati huduma inavyostahili ? pengine housegirl ndio kila kitu ? hadi kusema hivyo lazima kuna reason, tusikimbilie kusema ondoka, au achana nae,  we! usipime, mume mtamu jamani, mume anauma asikwambie mtu, ifike kipindi tujichunguze je tuna mapungufu gani sisi kina mama kwa upande wetu, kabla hatujaanza kulaumu waume zetu

 Kinamama tunapoishi na waume zetu kwenye ndoa, baada ya muda huwa  tunajenga mazowea, ambayo sometimes yanakuwa hayajengi bali yanabomoa, mazowea ya aina hii huleta kiburi ambacho kwa namna moja ama nyingine kina madhara makubwa sana, unakuta mwanamke anamdomo mchafu afadhali ya choo, anamjibu mumewe majibu machafu hata mbele za watu /watoto wao, kitu ambacho ni kibaya sana, sababu wale watu wanaowazunguka ninyi wawili watajua tofauti zenu, na mtatiana aibu sana maisha yenu yatakuwa nje, kila mtu atawaona vihoja kuanzia watoto hadi majirani, lo! tubadilike jamani.

Mume anataka kuheshimiwa, ili na watoto wajifunze heshima kupitia kwa mama yao, lakini utakuta mtu akiudhiwa anaropoka hovyo maneno makali ambayo baada ya ugomvi wao kuisha inageuka kuwa aibu kwake,

                                  (ii) (MALIZENI TOFAUTI ZENU CHUMBANI KWENU )
Turejee mafundisho ambayo wengi wetu huwa tunapewa kwenye Kitchen Party zetu, malizeni chumbani migogoro yenu, au hata ukimnunia  basi watoto wasijue, au majirani, mwingine akinuna basi ahata kama ni maji ya kuoga haweki, kama ni  Chupi ndio hatafua tena, kama ni chakula ndio hatamuandalia tena, jamani jamani, tujitahidi

wanaume ni kama watoto wadogo, utakavyompenda mwanao na kumuweka karibu na wewe ndio atakupenda sana, lakini mtoto ukimfokea fokea tu atakuogopa na kukuchukia, ndio kama waume zetu, tukiwaweka karibu watakuwa marafiki kabisa,

NDOA TAMU jamani asikwambie mtu, tusifikiri ndoa inaweza kuvunjika kwa urahisi. Sometimes mkikosana, jaribu kukumbuka mmetokea wapi?? Kumbuka siku yako ya harusi, kumbuka mapenzi mliyo kuwanayo kipindi kileeee, halafu uya apply kwenye ndoa yako sasa,  ndoa ina heshima yake kama mtaheshimiana, na hata kama mtapishana basi mmoja lazima akubali kushuka, ukijishusha mwanamke hutoonekana mjinga kama wengi tunavyofikiria, bali utaonekana mke mwenye busara asiyetaka kuibomoa nyumba yake kwa mikono mikono yake, KUJISHUSHA ni dawa moja nzuri sana,  hata kama hujakosea, kwani ukikaa kimya au kama unamueleza ukweli yeye haelewi, no need kupigizana kelele weeeee, NI KUJISHUSHA TU ndio dawa pekeee,

Kwenu wadau wangu, leteni maneno yenu yenye hakma, tusaidianae nami nitayapost faster.
nawapenda sana na ninatamani kama ndoa zetu wooooote zingekuwa za upendo na furaha ili hata vizazi vyetu (watoto wetu) viwe vimerithi tabia njemba toka kwetu 7 comments:

 1. Habari dada, jambo la msingi katika ndoa ni hilo coz wanaume is like a child vile unavyomtreat mwenza wako atakavyo yeye ndivyo mapenzi yazidivyo, hata katika maisha ya kawaida kujishusha ni jambo moja jema sana linaloepusha mambo mengi. ndoa ni tamu sana pia kumpa nafasi ya kumsikiliza akisemacho hata kama amekosea kisha unashauri kwa upole pia ni dawa sio kila kitu wajua wewe.....ndoa ni masikilizano, sio magombano, ndoa ni mashauriano sio majibizano, ndoa ni mpango kamili wa Mungu kwa wanadamu ili wakamilishe furaha yao duniani......pia huu u busy kupita kiasi tulionao wamama unachangia sana kudhoofisha ndoa jamani tujue kuna wakati wa baba na mama na watoto na wakati special wa mke & mume tu hata kama tuna mambo mengi tujitahdi kutenga muda. sio tusubiri mpaka baba aamue yeye. kila kitu inawezekana na utafurahia ndoa yako. tujitahdi kujenga paradiso katika ndoa zetu.

  ReplyDelete
 2. kweli kujishusha ni dawa kubwa sana sana katika ndoa mimi nimejifunza sana mume wangu ni mpele mno unaweza muuliza kitu leo atakupa jibu weekmbili zijazo atakwambia subiri nakumbuka, na huwa akimake dision ndiyo hivyohivyo na huwa akisema kitu kwa ukali namsikiliza saa nyingine namchunia masaa machache halafu naona huu ujinga aa nachilia mabli nasonga mbele na pia nimejifunza mume wangu ni rafiki yangu wa karibu sana sana, kuliko kitu chochote kile kwa hiyo utanuna usiku mko kitanda kimoja, haina faida sasa na mnageukiana upande mmoja, kwa kushuka ni jambo jema mno na ndoa ni tamu jamani

  ReplyDelete
 3. Naomba msikilize hii country. Inaelezea jinsi gani mazingira tunayoyatengeneza nyumbani yanasababisha watu kutoka nje ya ndoa
  http://www.youtube.com/watch?v=6-_7biygy3c&feature=player_detailpage

  ReplyDelete
 4. Kwakuongezea...
  Iwapo mwenzako ana hasira, basi chochote atakachoongea wakati yyuko na hasira, wewe msikilize tu aongee weeeeeee mpk amalize.....Then ukiona hasira zimepungua kdg ndio unamvutia kwa kitanda unaongea nae kwa utaratibu na kwa mapenzi makubwa, unamuelewesha then mambo yanaisha.... si vizuri sana kujibishana na mmeo na kupigizana kelele ambazo zinaweza kuwapa watu cha kusema..Ni mtazamo tuu....

  ReplyDelete
 5. kwanza nikupongeze mdogo wangu kwa ubunifu huu uliouleta ambao utakuwa msaada kwa wengi, real nimependa sana, WHAT I WANT TO ADD HERE NI KWAMBA, KAMA ILIVYOELEZWA NA VIOLET, NDOA NI TAMU JAMANI, TENA MARA NYINGI WANAOSHAURI '' ACHANA NAE, ATAKUUWA SIJUI NINI, HAO NI WAONGO NA WENGI WAO NDOA ZIMEWASHINDA AU HAWAJAOLEWA, WATU WANAENDA KWA WAGANGA KUTAFUTA NDOA, WEWE UWAACHIE KIULAINI HIVYO,
  POINT YA VIOLET NI NZURI SANA, TUJISHUSHE JAMANI HATUTAKUWA WAJINGA, MUNGU ATATUWEKA JUU, PIA NAKANDAMIZIA TUSISAHAU MAJUKUMU YETU NYUMBANI, KAMA NI KUMNYOA MR, MAENEO YA KATI, BASI HAKIKISHA ANAKUWA VIZURI, NI WAJIBU WETU PIA KUCHUNGUZA LEO BABA ANAVAA CHUPI GANI, KWAPA LA BABA LIKOJE LEO,
  Mkikosana ombaneni msamaha mapema, kama mwenzi wako ni mgumu kusema sory, basi wewe sema sory, HAUTAKUWA MJINGA JAMANI, kwanza yeye mwenyewe atashangaa,
  NIMALIZE KWA KUSEMA VIOLET UMEPENDEZA MWENYEWE, NAKUPENDA NA ASANTE KWA BUSARA ZAKO NZURI MAMA,
  MAMA MDOGO MERCY

  ReplyDelete
 6. violet nina mkasa wangu nahitaji ushauri naomba email address yako pssssss, au tunakutumiaje???

  ReplyDelete
 7. Hi Violet

  Ni kweli katika maisha ya ndoa inatupasa tushuke katika kugombana kwetu na hata watoto wasijue lakini kwa upande mwingine hata kina baba nao hawawezi kuongea taratibu na kwa ustaraabu je mtu km huyo umfanye nn then na anakwambia kwann unijibu incase umekaa kimya coz utaki kubishana nae so na usikose pia kuandika mada juu ya wao sio kila sie tu ndio wakushuka kwao.

  Na kitu kingine kweli tuna jisahau utamkuta mama anamuuliza msichana wa kazi kwann ujafua nguo za baba kwani msichana wa kazi ni jukumu lake kufua nguo za mumeo au ww mwanamke?

  pia tuwe macho katika kuwapangia mavazi gani wanataka kuvaa kabla ya kwenda job coz kuna wengine hawafanyi kazi so ni jukumu lako ww mwanamke kumpangia nguo mumeo ujue anavaa nn mpaka soksi maana ipo siku atakujia na chupi ya kike then waanza jiuliza mh km yangu vile or sijui sikumbuki kumbe katoka nayo huko nje kwa mwanamke mwingine.So ni wajibu wetu kufundishana kila kinachowezekana km wanandoa ndani ya nyumba ila kuna wanaume wengine awakubali kunyolewa ila km yy hataki mwambie ninyoe mie basi na hakuna raha km kunyolewa na mwenza wako jamaniiiiiii.

  So tujitahidi muda tunao hata km tunafanya kazi ila tunaporudi jioni majumbani kwetu tuwe macho na yale yalibaki kwa muda ule mpaka saa ya kwenda kulala.

  Frm Halima.

  ReplyDelete