Monday, March 21, 2011

NIKIMWAMBIA NIKAMTAMBULISHE KWETU ANASEMA NIMWACHE KWANZA- NIFANYAJE

mambo dada v mimi kijana mwenye miaka 22 nnamchumba wangu ambae nampenda sana, chaajabu anasikiliza sana maneno ya watu,

na pia kila nikimwambia kwenda kwetu nikamtambulishe analeta sababu mi nashindwa kumuelewa kabisa na nnampenda sana jamani

tuna mwaka mmoja na miezi sita sasa na kila nikimwambia kwenda home ana jibu ucjali home tutaenda lakini kuna mambo nakamilisha na ukijaribu kufatilia mambo anayosema anayakamilisha hakuna lamaana  hata moja yani jamani mi cmuelewi kabisaaaaaaaaa, hebu jamani dada angu nisaidie nimueleweje huyu mtu?5 comments:

 1. Hujatuambia uafanya kazi gani au unataka kuowa na umri huo miaka 22 years, usichanganyikiwe kaka soma kwanza uwe na maisha mazuri unamtambulisha mtu kwenu kwani unataka kuowa lini, ukishamtambulisha au. labda anaona aibu mwanamke uwe na aibu. babu
  ongea naye kwa hekima

  ReplyDelete
 2. we mtoto mdogo hivyo unataka kuoa kwa nini? watu wanalalamikia ndoa wewe unataka kuingia mapemba yote hiyo??? ah! hebu soma kwanza mdogo wangu, jipange kwanza, haya maisha ya kuoa yapo utayakuta na utayachoka sana. sawa

  ReplyDelete
 3. we kijana, tafuta maisha kwanza, achana na habari za kuoa

  ReplyDelete
 4. achana na mademu wewe bado mtoto sana umtambulishe wenzio yanatushinda wewe sahizi
  soma MR

  ReplyDelete
 5. umri sio isue,
  ninachokushauri mimi ni kimoja tu! huyo binti hakupendi, na ameshajua kuwa wewe unampenda, na utateseka sana,
  mshukuru mungu kwakuwa umejua mapema sana alivyo, kweli kaka nakwambia ukioa utakuja kujuta, achana nae, hakupendi, au ana mtu mwingine teyari, achana nae huyo hakufai, pole kwa hayo kaka

  ReplyDelete