Monday, March 14, 2011

MUME KANIZUIA URAFIKI NA MKEWE- CHA AJABU MKEWE ANANIPENDA NA NAMUHURUMIA KUMTENGA, NISHAURINI JAMANI


Dears, hii ni ndefu kidogo, hata hivyo nimejaribu kuiedit ili isitupe uvivu kusoma, lakini itakuwa na fundisho ndani yake, hebu tumshauri mwanamke mwenzetu maana mh!! soma mwenyeweMimi ni mama nimejenga, naishi kwangu na mume wangu na watoto watatu, Juzi juzi hapa kahamia mama mmoja hivi, alipofika mimi ndio nilimpokea, ni jirani yangu kabisa, basi tukatokea kuelewana sana, 

Ila kwa kumuangalia tu! Utagundua ni msemaji semaji sana, lakini mimi naweza kuishi na watu wa hivyo so sikuona tabu kuzoweana nae, mumewe hatuna mazowea, na kwanza si tabia nzuri kumzowea mume wa mtu, ila huwa tukionana mara moja moja mtaani au barabarani, husalimia tu! Inshort ni watu tunaoheshimiana sana

Sasa wiki iliyopita weekend nilikuwa natoka, ile natoka nje tu! Nikakutana na huyo mama (jirani yangu) getini, akanambia nimekuja kupiga story, nikamwambia mie natoka, akasema nikusindikize maana nyumbani niko mchov sana nikiwa pekeyangu, nikamwambia, umeaga kwa mumeo? Akasema ngoja nimusms, maana yuko uwanjani kwenye mpiria nikipiga hatutaelewana,
Baada ya muda akaniambia ameruhusiwa kwenda,

basi akaunga tela safari ikaanza, mishale ya saa 2:30 usiku tukarudi, nikamshusha kwake, nami nikaingia kwangu, ile nafika tu hata sijakoga geti likagongwa, kutoka namkuta Yule jirani yangu na mumewe, keshadundwa na macho yote yamekuwa mekundu sana kwa kulia.
Mumewe akaniambia shem mimi nakusheshimu sana, akaniambia nataka uniambie ulimpeleka wapi mke wangu, nikawambia ha! Si huyu hapo muulize tulikuwa wapi?

Akasema nimekuuliza wewe, aliongea kwa ukali hadi alinichefua  ananiliza as if ni mtoto wake, nami nikaja juu, nikamwambia bwana, haya wewe na mkeo wote out, mko kwangu leteni heshima, kama kwenu hamuheshimiani wala kuaminiana basi nikwenu, naomba mtoke nje sasa hivi, ikabidi awe mpole,

Akaniambia naomba niambie, nikamuleza ukweli wote kwamba kuna shemeji yangu huko tegeta alipata ajali, ndio nilikuwa nakwenda kumuona, akaniambia kwanini uliondoka na mke wangu bila ruhusa yangu, nikamwambia wa kuomba ruhusa ni mkeo sio mimi, na alikuomba na ukamkubalia,

Akamuuliza eti uliniomba ruhusa mimi? Kabla hajajibu akalambwa vibao mbele yangu, nikasema jamani, kwani nyie mnaishije??? Yule baba akaniambia hivi,

NAPENDA UENDELEE KUHESHIMIKA , NAOMBA ACHA URAFIKI NA MKE WANGU, HUYU MIMI NDIO NAMJUA, TABIA ZAKE HUZIWEZI, NAOMBA ACHA- UKIENDELEZA URAFIKI NAE YATAKAYOKUJA KUKUPATA USINIHUSISHE,

Akamgeukia mkewe na kumuwasha vibao kadhaa mbele yangu na akamvuta kuelekea nje
Kinachonitatiza, huyu dada haishi kuja kwangu, yani nikiwepo tu! Basi anakuja, nilimwambia bwana, hebu tulia kwako wewe, akasema mume wangu namjua mimi, wala usisikilize maneno yake, yani  ametokea kunipenda sana huyu binti (maana nimemzidi umri kidogo)

Sasa nifanyaje maana huyu mkewe nishamwambia mara kibao bwana wewe mumeo hataki uongee na mimi kaa tulia kwako, lakini hakomi na wala haachi, sometimes huwa najificha kabisa akija namwamiba mschana wangu mwambieni hayupo, hivi ninavyokwambia Violet hata jana alikuwepo kwangu. Nisaidieni,

1 comment:

  1. Habari za mchana wapendwa... ngoja nikupe ushauri kidogo mpendwa...unajua kwanini mumewe alikasirika? hii inaonyesha kabisa huyu dada hakumwaga mumewe alipretend kuwa kamuaga lakini hakumuaga.. asingekuja nae pale mbele yako na kumuuliza " ETI NILIKUPA RUHUSA WEWE" Inaonekana huyu dada ni muongo na anapenda kutembea kwenye nyumba za watu.. haiwezekani hizo siku chache alizoamia hapo keshakuzoea namna hiyo hata kama ulimpokea wewe na kuanza kuja kupiga story kwako... huyo anatabia mbaya ya umbea... inawezekana mume wake ameshamchoka kwa tambia zake za umbea na kuletewa mashataka mara kwa mara nyumbani kwake... na kwanini kama ni mke mzuri akikatazwa kitu na mumewe asikubali kuacha kwani lazima aende kwa mtu ndo utaonekana jirani mwema? ujirani ni kuheshimiana, kusalimiana na kusaidiana wakati wa shida na raha sio lazima uende kwa mtu ukapige story... Na huyo mumewe alikasirika kwa kuwa hakumuaga, alafu anarudi saa mbili za usiku siyo tabia nzuri kwa mke wa mtu... na wewe ulikuwa na confidence, na uaminifu naye na ndio mana ukakaa nae mpaka saa mbili za usiku ukijua kuwa mumewe anataarifa.. huyo ni mbea na mchonganishi .. kunasiku atakuchonganisha na watu wengine hapo mtaani,,, mana inaonekana anatabia za kwenda kwa watu... sasa uwe makini kama mumewe alivyokwambia... kwani hana kazi za kufanya? mshauri akae ndani kwake. Na wewe usipende tabia za kubebana na wake za watu, especially hao uliowazidi umri utaonekana unaenda kuwatafutia mabwana na ikiwezekana na kunasiku yatakukuta ambayo hutasahu, mwambie ukweli huyo binti kuwa huwezi kufanya nae urafiki, ila muwe majirani wema tu... inatosha.. Usimkwepa wala usijifiche kwa ajili yake mpe ushauri mzuri na mwambie alinde ndoa yake...

    ReplyDelete