Sunday, March 6, 2011

ANAFANYA UMALAYA HADHARANI BILA HATA KUNIOGOPA-NIMFANYAJE AACHENisaidieni mwenzenu jamani, nina watoto wawili, miaka 6 na miaka 4, wote wanasoma.

sikuhizi mume wangu amebadilika sana, kiasi kwamba hata ada za watoto wake hatoi, hadi tugombane sana ndio anatoa ada, mapenzi pia yamekwisha, anafanya mambo ya aibu hadharani huku watu wakiona,

Kuna siku moja alikuwa na wanawake bar, amewanunulia pombe, huku wanamshika shika, dada mmoja akiwa pale bar ananifahamu akanipigia simu niende nikamuone, nikaenda nikajionea, wanamnyonya, wanamshikashika sana, ndio maana akirudi nyumbani anakuwa hana hamu na mimi,

basi siku hiyo nilipata ujasiri nikamfata pale pale, nikawambia jamani, tafuteni nyumba ya wageni, msitie aibu hapa, wale wadada walikimbia, mume wangu nae akaanza kunikimbiza nipige huku kashika chupa mkononi, 

nikajificha mahali, nilipoona amerudi bar, nikarudi nyumbani nikachukuwa nguo nikaondoka, nikakaa kwetu mwezi mzima, badae akaja kuomba msamaha, nikarudi, sasa ujinga ule umeanza tena, anaweza hata kunitukana mbele ya watoto wangu, naumia sana
Mimi sina kazi, nikiondoka tu hata watoto hatawasomesha tena, sasa nifanyaje jamani, niliwahi kufungua biashara ya salon, akanifanyia fujo na kunifanya nifunge, hataki nifanye chochote kile,

Naomba ushauri please, sijielewi kabisa, ukizingatia mtaa mzima wameshajua tabia yake, naona hata aibu kutoka ndani
No comments:

Post a Comment