Friday, March 18, 2011

ANASEMA NIACHE KAZI - NA KAMA SITAKI BASI TUACHANE NAE- HELP ME PLEASE


Habari yako Violet, mimi huwa ni mpitaji mzuri kwenye blogu yako, japo huwa sichangii kutokana na ubusy nilionao . lakini leo yamenikuta naomba msaada wa mawazo,

Mimi ni muhasibu Company moja hivi ya clearing and forwading hapa Dar es salaam,  nimeolewa na mfanya biashara , ndoa yetu ya kiislamu ilifanyika mwaka jana  mwanzoni na tunamtoto mmoja wa kiume,

Mume wangu alinikuta nafanya kazi, sasa baada ya kujifungua mkwe wangu (mama yake ) aliniletea housegirl, nikawa namwachia mtoto, siku moja baba yake akaniambia yeye hataki mwanae alelewe na housegirl, nikamwambia mbona namuacha mtoto katika hali nzuri na nikirudi jioni huwa namuhudumia vizuri, akakataa,

Nikawa naenda kazini kwa kuforce, kuna siku asubuhi mimi naoga, akachukuwa nguo zangu nilizoaandaa akazificha pamoja na pochi yenye pesa zangu , nikamuuliza akasema hataki nifanye kazi, tukazozana sana, hata kazini sikwenda

Sasa nisaidieni wapendwa nimepewa mwezi huu tu! Nikishapokea mshahara niache kazi, anadai atakuwa ananilipa hiyo hela kila mwezi kama haiwezekani basi nirudi kwetu nimuache mwanae

KINACHONIUMA
1.   Mimi ndie msaada nyumbani kwetu, wazazi wangu wananitegemea mimi katika baadhi ya mambo
2.   Nikikaa nyumbani nitasahau ujuzi wangu, kwa wale maacountant wanaelewa namaanisha nini
3.   Kazini kuna posho nyingi, not only that lakini pia tunapata huduma ya hospitali mimi na familia yangu, so baadhi ya gharama zinapungua,
Nisaidieni mwenzenu, kazi naitaka na mume namtaka

14 comments:

 1. ACHANA NAE, USIACHE KAZI, KAZI NDIO MUMEO WA KWELI

  ReplyDelete
 2. Achana nae huyo, tena wewe muislamu dini yako inakuruhusu kutaliki. Ingekuwa kina sie ndo kulia na kusaga meno. Achana na huyo mume hakupendi kabisa na ni mbinafsi. Hata kama ana pesa kazi ni zaidi ya pesa, utakaa nyumbani ufe kwa presure

  ReplyDelete
 3. Pole dada angu lakini kuhacha kazi husikubali kuacha. Fuata fikra zako dada, wanaume wa siku hizi sio wa kuwaamini, na wala sio wa kuwategemea. Ukifuata mawazo yake na fikra zake, mwisho utajuta.

  1)Washirikishe wazazi wako, usikie watasemaje.

  2) Ama Chukua chako ondoka bibie, tena mchukue na mwanao maana haki ya tz mpaka atimize miaka 7 ndio anaweza kuishi na baba. Hawezi kukuzuia husimchukue mtoto wako, mtoto ni wa mama wakati wote, wewe ndio unajua uchungu wa kumtoa mtoto nje ya tumbo na sio yeye.

  Husimuogope hata kidogo bwana, anakutishia tu, ili ufanye kama anavotaka. Mie nazani ukiondoka atakuja mwenyewe kukuomba urudi home. Na hata kama hasije kukuomba mrudiane, hachana nae, fuata msimamo wako wa kimaisha, husimuache mtu yeyote akuyumbishe.

  Faham, nia na mathumuni ya mumeo ni
  kukuharibia maisha yako,ili akumiliki. Nia yake haswa hakupige chini, akukandamize kimaisha ili aku controll, akitoka hapo atakufanyia vituko vya ajabu na kukutesa sababu unamtegemea. Huyo ni muaribifu wa maisha yako, hapendi maendeleo yako... mnafki tu basi.

  Lingine la kufikiria, ya mungu mengi akiaga dunia kabla yako, atakulipa akiwa huko kabulini pia? samahani kwa kusema hivo, ila mtu lazma uwe unangalia future pia, sio ya sasa tu. Wazazi wawili wakiwa na elim na wote wakiwa wanafanya kazi ni picha nzuri sana kwa mtoto. Nikipata muda nitaongeza kuandika ngoja nikalale kwanza nimechoka, mie nina watoto 2 na nimeolewa pia, na napiga kazi toka asubuhi hadi jioni, hamna kurudishana nyuma kimaisha songa mbele. Hata mie simsikilizi mume wangu hata kidogo, akija na mawazo yake yasio jenga kwangu.... tunagombana na kutengana time ingine, ndoa ndoano, ukifuata msimamo wako mume atakuheshm sana na atakuona unazo akili na yeye mwenyewe atajilaumu baadae.......

  ReplyDelete
 4. Kaza buti kwa kumaanisha dada unajua mimi nimejifunza sana kutoka kwa mama yangu dada mama yangu alikuwa nesi baba alikuwa POlice kila siku baba alikuwa anamwambia aache kazi wanagombana kila siku mama akamwambia siachi siku moja akachukua nguo za kazi akachoma moto kesi ikaja kwa babu kijijini, lakini mama alijenga masimamo sana ikatokea akatutekeza akatafuta nyumba ndogo akapotelea kabisa tulilelewa na mshahara wa mama wa nesi tukasoma alirudi akatukuta tumekuwa watu wazima na mshahara wa nesi umetusomesha na mama amejenga nyumba kwa mshahara huo wa nesi. Sasa basi angemsikiliza kipindi hicho aache kazi angekuwa mgeni wa nani kipindi ametuacha, sasa bibi kaza buti tumia hekima yako utaishije wewe kwa mshahara kutegemea, na kasi ya maisha magumu, ilivyo unataka hata pad umuombe familia yako inakutegema usiache kazi tafuta watu wa kuongea naye, ukiacha utaijutia na kuikumbuka siku moja

  ReplyDelete
 5. haya ni majaribu sijui hata nikushauri nini maana kazi inauzito wake na mume anauzito wake jaribu kuwashirikisha wazazi wake au tafuta mtu mwenye hekima kidogo awezekumsemesha amweleze umuhimu wa kazi ni hayo tu otherwise bora umwache mume uendelee na kazi yako maana nao hawa tabiriki unaweza kuacha kazi yako na yeye akakuwacha au asikuwache lakini akakufanyia vituko ukajuta kuzaliwa

  ReplyDelete
 6. Pole mpendwa kwa hilo. Mimi nakushauri usiache kazi bali jaribu kushirikisha wazazi katika hili maana ni suala gumu sana kuacha kazi, watu wanatafuta kazi halafu wewe Mungu amekupa eti uache? Hebu fikiria ukiacha kazi halafu wazazi wako nani atakayewasaidia? Ndoa ni tamu na kazi vilevile ni muhimu, ongea na mumeo umweleze hali halisi akishindwa kuelewa washirikishe hata viongozi wako wa dini. Pia nakuomba umuombe Mungu akusimamie katika hili kwani yeye atakushindia, funga kwa maombi naye atakusaidia kwani Mungu hana upendeleo!

  ReplyDelete
 7. Dada Muhasibu,kwanza nakupa pole.Pili,naomba nitoe fundisho kwako na kwa wanawake wote wenye hali kama yako,umeeleza wazi kabisa kuwa ukiacha kazi ujuzi utapotea,matumizi pia hayatakuwepo kwani wewe unahudumia nyumbani,wazazi wako pia unawasaidia-unajua sisi wanawake tunafanya mambo makubwa lakini madogo hatuyawezi-kuzaa ni kazi kubwa-lakini kuwa na msimamo na mambo yetu hatuwezi-hivi uache kazi halafu iweje?mkikosa matumizi mumeo akioa mke wa pili tena mwenye kazi ndio awalishe wote pamoja na wewe?can u hold that?
  hujatueleza ulipopewa mwenzi mmoja ulijibu nini?kama ulikubalia basi huna budi kuacha kazi ila nitakuona mjinga sana.
  Ushauri endelea na kazi-mpe msimamo wako kuwa wewe hufanyi kazi kwaajili ya mshara tu-jamani kukaa nyumbani bila shughuli mbona ni ugonjwa?akinga'ngania mwambie sawa..akufukuze tu..kwani nini hivi unajua wanaume wanatupima misimamo yetu pia?kwakweli jibu la swali lako linategemea wewe ulijibu nini ulipopewa notice na mume wako ya mwezi ya kuacha kazi..?but stop being foolish be woman and stand up 4 ur right..jamani juzi tumetimiza miaka mia (100) ya uhuru wa wanawake..haya mambo wanawake tunayasikia kwenye redio tu bila kuyafanyia kazi?please kazi kwa kwenda mbele..akisema anakuacha mwambie sawa...kama kweli anakupenda hawezi kukuacha kwasababu unafanya kazi..

  ReplyDelete
 8. Acha hiyo kazi uone atakavyokunyanyasa unawajua wanaume unawasikia na ndoa yenyewe ya kisislamu wewe usicheze dada usiache kazi familia yako nayo utaiweka wapi, Mimi dada yangu alijidai anataka kuacha kazi kisa mwanamme kila siku anahamishwa mikoani na yeye mikoani hamna bandari tukampa somo na mume wake mwenyewe mnyanyasaji kwa kwenda mbele siku akilewa mapombe yake katoka hamnsini elfu kwa mama mkwe ni matusi tu kuwa sisi masikini familia yetu masikini sana kaowa mtu mmoja tuu, sasa kaza buti usiiache kazi

  ReplyDelete
 9. Huo mumeo hajasoma nini mwambie ache yeye kazi akaye nyumbani kwa mwezi mmoja tuu halfu muulize anajisikisiaje asikubabaishe hapa ukishinda hilo tuu basi hatokushinda te tena,

  ReplyDelete
 10. Dada pole sana kwa yanayokusibu....! najua kwamba upo kwenye wakati mgumu sana hivi sasa, ila jambo la msimgi ninalokuomba tafadhari usiache kazi hata kama atakupiga mkwala namna gani, mume sio kila kitu. Hivi unafahamu ugumu wa kuwa gorikipa? na hao ndugu na wazazi wako nani atawasaidia!Acha kujiangalia wewe pekee, hebu angalia jinsi gani hao wazazi wako watakavyoathirika na kumbuka jinsi walivyojitahidi kukusomesha na mpaka ukafikia hapo ambapo huyo mume akapata kuvutiwa na wewe na kuwa mkewe, Leo hii eti kirahisi tu anakwambia acha kazi(haaa!),haiingii akilini hata kidogo. kuwa na msimamo dadangu shikilia kazi yako. Ni bora uendelee kubarikiwa na mungu kwa kuendelea kuwasaidia ndugu zako, kuliko kupata laana eti tu kwa kutaka kumfurahisha mume.

  ReplyDelete
 11. Alikuoa ukiwa unafanya kazi na sasa anataka uache kazi kisa hataki mtoto wake alelewe na mtu mwingine, looooooooooo, vituko. Mulize kwa nini alikuoa ikiwa akijua wewe ni mfanya kazi,na kwa nini hasikufahamishe tokea hapo mwanzo kabla ya ndoa kuwa ukizaa atataka uache kazi, maana pale ungejua kufunga nae ndoa au kuachana nae. Muulize kwanini hasioe mwanamke sio mfanya kazi ili amzalie na amlele watoto wake mpaka akaja kukuoa wewe mfanya kazi? Huyo mwanamme mwendawazim

  ReplyDelete
 12. wanaume malaya pia huwa wanatabia hiyo ya kuwaambia wake zao waache kazi kwa kusingizia hawataki watoto wao walelewe na mahousegirl, kwani anajua ukifanya kazi ukiwa unakutana na watu watakutongoza na wewe. pia kuwa makini atakunyanyasa huyo na hiyo pesa yake utaiona baada ya miezi kadhaa tu, baada ya hapo utapata joto ya jiwe... usiache kazi, kazi ni muhimu ukizingatia masiha ya sasa yamepanda yani hata matajiri wanalalamika sembuse yeye... na akifa je utaanzia wapi wewe?... acha fikira hizo fanya kazi na umshirikishe mungu pia katika hilo... wish you lucky ila keep it in mind USIACHE KAZI UTAJUTA....

  ReplyDelete
 13. USIACHE KAZI UTAJUTA MIMI MUME WANGU ALINIAMBIA NISIFANYE KAZI, KISA NI MKOANI NA YEYE BIASHARA ZAKE NI DAR ES SALAAM NIKASEMA NTAENDA POPOTE SASA NIPO MWANZA MAISHA YANAENDELEA KAMA KAWAIDA. LAKINI BAADA YA MIAKA MIWILI NIKIWA KAZINI YEYE AKAPATA MATATIZO KWENYE BIASHARA ZAKE SASA HIVI MIMI NDIO KILA KITU KWAKE NA NIMEMPA PESA ZA KUWEZA KUANZA BIASHARA UPYA, MWACHE AENDEEE KAZI NI KILA KITU MAMAA

  ReplyDelete
 14. Pole dada

  Ila mie nakushauri usiache kazi na kumbuka kwamba ww ndio wanakutegemea kwenye familia yako.

  Mie nina mfano uliohai kabisa dada yangu mume wangu alikuwa yupo Mbeya kikazi so kwa ss amerudi hapa hapa dar kule mkataba umeisha so kwa ss ana kazi na mie ndio kila kitu kwa hapa nyumbani ss je ningeacha kazi leo hii tungeenda wapi na familia yetu.so kuwa makini dada coz mie mume wangu alisema hivyo hivyo acha kazi nikamwambia itakuwa ukitaka niache na uite pande zote mbili ueleze kwamba namuacha sababu hataki kuacha kazi.

  ReplyDelete