Naombeni ushauri please,
kuna baadhi ya tabia chafu za mume wangu ambazo sikuzijua before, au sijui kwakuwa nilikuwa simchunguzi sana, sasa nimegundua baadhi ya tabia chafu anazofanya, nimelia sana na nimeumia vya kutosha kias kwamba huwa nawaza hata kumuua yeye na mimi mwenyewe nijiuwe, lakini nikiwaza watoto, moyo unaniuma kupita maelezo. Naumia sana, lakini kuondoka siwezi, na bado nampenda sana isitoshe nimezaa nae, nampenda sana.
Huwa najaribu kumuonya mimi kama mimi, na sometimes nimeshawafahamisha ndugu zake, wamemuonya, lakini sioni mabadiliko,
la kwanza, kinachoniumiza zaidi ni kwamba, hataki kuonekana kama ana mke. Hivyo huwaambia wanawake zake kuwa sijaoa, wala sijazaa, utakuta hadi usiku tumekaa nae, wanamtumia sms za mapenzi, ukicomplain anakuuliza hiyo sms ina ubaya gani. (hivi jamani, mtu asiempenzi wako anaweza kukuuliza- sweet umekula nini usiku huu, I wish ningekuwa karibu nawe)hii ni sms ya kawaida kweli?
Pili anapenda sana kusifia wanawake wa nje, kwenye website na sehemu zingine, mimi naumia sana, moyo unauma, hadi nimeamua kutaka ushauri, naelekea pabaya, NAMPENDA SANA, SANA TU! Nahisi siwezi kuishi bila yeye, kweli kabisa, nampenda mume wangu. Nahisi anajua ndio maana ananitesa namna hii.
Sasa nimepigiwa simu na mtu ambae mimi nayeye wote tunamfahamu, akaniuliza unayajua anayoyafanya mumeo? Njoo nikueleze, mimi nakupenda, na uthibitisho ninao. Sasa mimi najijuwa hali yangu, nahisi naweza kufa,
Roho moja inashauri nisiende, nyingine inasema niende nikayajuwe, bado nashindana na sauti hizi ndani ya moyo wangu. Pia najiuliza kama nikienda na nikayajua je kifua cha kustahimili ninacho??? SINA, lakini mbona nataka kuyajua anayofanya?????
MAPENZI YANATESA JAMANI, YASIKIE KWA MWENZIO TU USIOMBE YAKUKUTE WEWE. NIMECHANGANYIKIWA NIFANYAJE MIMI, PLEASE NAOMBA USHAURI NAONA GIZA TU, Maana huwa nikipata habari zake akili zote huhama, kama ni kazi nitavuruga toka asubuhi hadi jioni, naweza hata kula nisile, nina mwaka wa sita kwenye ndoa yangu, tena ya kanisani. ah! some times naona bora hata nisingezaliwa.

POLE SANA DADA, MUMEO ANAONEKANA AMEKUCHOKA NDIO MAANA ANAONA HATA AIBU KUSEMA AMEOA SO KIKUBWA HAPO NI KWENDA KWA HUYO MTU ILI UJUE UKWELI INGAWA UTAUMIA ZAID, NI NGUMU SANA MTU MWENYE UPENDO WA DHATI KWA MKEWE KUKANA KWAMBA HANA WATOTO NA WALA HAJAOA, HAKUKA LINALOSHINDIKANA VUMILIA ILI UWEZE KUPATA UFUMBUZI WA TATIZO HILI, KUONDOKA SIKUSHURI HATA MIMI COZ UNA WATOTO CHA MSINGI KUOMBA MUNGU ALI AKUEPUSHE NA MARADHI NA PIA AWEZE KUMBADILISHA
ReplyDeleteusijiue,usiondoke, usimfatilie, atakuumiza, wewe mdharau, fanya kama huyajui anayofanya, maisha yataenda, shauri yako,
ReplyDeletehebu fikiria ukifa wanao wataishi vipi, nani atabeba msalaba wa kulea watoto, hawa tulio wazaa tu wanatushinda, haya hao ambao hatujazaa sisi,
JUST IGNORE HIM, kama ni mfanyakazi endelea kupiga mzigo, na kama huna kazi, basi usijibweteke, tafuta cha kufanya, huo ndio ushauri wangu
pole mama, du! nimeumia sana, pole mdogo wangu, mshirikishe mungu, atakutetea, atakusaidia maana yeye ndie aliyetengeneza ndoa
ReplyDeletePOLE DADA, KAMA WALIVOSHAURI WENGINE, MSHIRIKISHE MUNGU. POLE
ReplyDeleteKWELI MSHIRIKISHE MUNGU KTK HILI, ULIWEZI PEKE YAKO. MUNGU AKUTIE NGUVU MPENDWA
ReplyDeletePole mpenzi am not married yet ila i fill sorry for you.Muache kama alivyo mumeo na wala usiumie that much fanya uchunguzi wewe mwenyewe then ndio umface ur husband umwambie nini anakifanya na the way unavyoumia because of that kuondoka si suluhu more than all ndio utampa more chance ya kujiachia.Kuhusu kutojitambulisha kua ameoa its because of that behaviour yake.Ignore him on that anaweza akajitangaza lakini asiishi kama ameoa na pia marriage come from the heart and not mouth.Na plzzzzzzzz!wanawake mcwaonyeshe waume zenu kwamba wao ndio kila kitu yani bila wao maisha ya wanawake wengi yanapotea.Be strong my love thats love but never love too too much.
ReplyDeleteTrust me that man hajakuchoka kama anaondoka na kurudi nyumbani he is still yours.Just ignore him and try to make follow up on him by your self bila kumshirikisha mtu.Ukigundua ni kweli then tell him the truth kama hakubali mpe vithibitisho kama hataki wafate wakubwa zake.huko imeshindikama amua mwenyewe bila kushauriwa na mtu kuondoka au kukaa nae na uvumilie milele.
ReplyDeleteUsijiuwe wewe kwanza kapime afya yako iko safi, la pili ushinde moyo wako kayajue ile ujue unaanzia wapi mbona sisi waume zetu hatukutegemea kama wangeweza kufanya uchafu jirani tuu na nyumbani kuna gest kumbe ana kitoto huko nilipogundua nilitaka kufa ndoa yangu miaka 9 sijawahi muona hata siku moja pili ni bishoo sana na ana dharau mno wa wanawake maana mimi nilikuwa ni unique nilipogundua tulichuana vibaya mno japo nilikonda mno kama mgonjwa nikachakaa na siku moja nipogundua yupo bar fulani na huo demu nikamlazimisha kurudi nyumbani tukagombana katika simu akaniambia leo utakoma akaenda kulala huko huko aliporudi kesho yake sikwenda kazini niliomba ruhusa tuligombana mno mwisho tukaenda kwa washenga, tukayasort na kitoto chetu cha kiume nikadogo tuu nikamwambia ongea na baba yako mimi nimechoka au unataka mimi niondoke aje mama mwingine akasema hapana kikamwambia baba yako akamwambia unamuona mama baba hali usiku analia kila siku, mpka na mimi nalia akamwambia mimi sitaki mama mwingine nataka kukaa na mama yangu akanyamaza kimya, ilifika hatua akanionea huruma akatafuta rafiki zake wawili wakaja tukaa kikao akaniomba msamaha mwenyewe kwa kusema jamani namuonea huruma mke wangu alivyo konda nitamuuwa sasa, kwa kiwewe akanipa cheap yake ya simu akanunua nyingine, yle dada alikuwa antuma mgs kwa siku hata inshirini analalamika mimi namjibu sikutaki sasahivi niko na mke wangu akipiga sipokei mpka kachoak siku hizi anatuma mgs anajidai kapotea no anatuma ktk hiyo cheap ya mume wangu ambayo ninayo kwa hiyo bwana mtumaini mungu pia na maombi kwani shetani mwizi na mharibifu,
ReplyDeleteWewe tatizo lako dada unampenda sana mumeo. Kumpenda mume si tatizo na ni tatizo. Ni tatizo pale mtu anapogundua umemfia wakati yeye hana mapenzi nawe kihivyo au alikuwa nayo ila yako yamezidi na yamegeuka kero. Nakushauri usihache kumpedna mumeo ila usimwonyeshe namna hiyo. Maana kuna wamama tunadiriki kuwambia wenzi wetu ukinihacha ntakufa. Mimi mume wangu nilikuwa nadhani ni malaika, yaani ni tofauti na wanaume wengine. Lakini tulipofika miaka sita kwenye ndoa, alianza uhusiano nje kipindi mimii ni mjamzito. Nilimwambia ntajiua na nitawaua watoto (nilikuwa namtisha tu) wacha achanganyikiwe, piga simu kwao na kwetu. Kwa kifupi cha moto alikiona. Nilijua fika alicheat kwa kuwa nilikuwa nina mimba na mimba ilinifanya niwe mbali nae. Lakini nilimwambia I will make sure your life wont be the same kwani najiua na watoto uanze upya na huyo malaya wako asije nitesea watoto. Na huyo kimada nilichomfanyia hatakaa atembee na wame za watu (maana nae alikuwa si mzoefu kwa utafiti wangu alikuwa anajifunza) Sometimes fighting pays. Dada alikoma mpaka akiniona town anatafuta uchochoro. Na mume wangu hakumtetea wakati namfundisha adabu (sikumpiga lakini) ndo nikajua wakati mwengine wanaume wanatoka nje si kwamba hawatupendi ila kuna wadada wako strategic kuiba wame za watu.
ReplyDeleteKwa ufupi yaliisha ila toka siku hiyo nimejua wanaume si malaika. Na sitashtuka tena nikisikia ana mwanamke mwingine kwani nimekubali matokeo, ila akirudia talaka nitampa japo mimi ni mkristu. Silei maradhi nimesamehe mara moja basi next time nachukua wanagu namwachia nyumba chakufa nini na nina watoto wazuri wakiume wanaonipenda mama yao unconditionally. Wewe unasema unajiua na una mtoto. Kama mwanaume hakupendi kumbuka mwanao anakupenda zaidi ya chochote kile duniani. Kwani mwanaume ulizaliwa nae. Kama mume anipendi na mimi simpendi vile vile. Alah
CHUKUWA WANAO UONDOKE, ATAAKUUWA HUYO
ReplyDeletemh!! pole sana dada yangu ila amini hakuna kinachomshinda Mungu...piga goti bila kukoma mweleze Mungu anakusikia na anayaona unayo pitia...sikio lake si zito ata asisikie mlilie mpaka akujibu.. huyo mumeo shetani amemteka na wakumkomboa ni maombi yako ivyo ombasana bila kukoma....Mungu wetu ni mwaminifu na mwenye hekima sana alishasikia kilio chako vyakutosha..........ata yafuta machozi yako n a furaha yako itarudi mara dufu...mwamini Mungu dada yangu.
ReplyDeletePole,be strong.it is very normal katika marriage life kwa baadhi ya wanandoa,kuna kila stage katika marriage life--kama walivyosema wengine-IGNORE HIM don't show him kuwa message za wasichana wake zinakuumiza-najua inauma but you dont have choice now-zaidi ya kuignore-kama unafanya kazi be busy-if u have friends kazini-do some chatting with them-wakati yeye anapokea message kutoka kwa vimada wake-make yourself busy na simu yako pia-you can even ask you friends to call you at night be busy-this will disturb him-mapenzi yanataka wivu kwa pande zote-kama wewe unaumia anavyochat na vimada-na yeye ataumia unapopokea simu usiku na kuchat-fanya kitu tofauti-plan to go out-make friends -life is too short dont hurt yourself that much-Muweke MUNGU mbele pia katika kila unalofanya-dont cheat him but make yourself happy-he is ur husband no one can change that-but u need to show him the other side of you..be different for sometimes-kama umezoea ukiona msgg ya msichana ulalia this time give him a big smile-and make urself busy-dont ask him anything just a smile-do abnormal things-itamfanya ajiulize whats happening-ikifikia hapo-then it is time for discussion-arrange siku muyaongee-ALL the best.
ReplyDeletePole dada
ReplyDeleteIla ndio maisha so usikae kufikiria sana na anapoona ww unakonda kwa ajili yake anafurahi sana so be strong.Na km unataka kuyajua nenda kwa huyo dada akwambie kuliko kukaa na dukuduku moyoni nakwann ujie sababu ya mwanaume kwani ulizaliwa nae siku moja au yy ni muhimu sana kushinda mwanao kujiua sio suluisho la matatizo kumbuka hata arobaini aitaisha na atakuwa na hao vimada wake na kumpa tabu mtoto wako na hata km wataka kumuua mtt unataka kupata dhambi ya bure kwa mwenyezi mungu.
Wanaume ndio walivyo hata uwabebe mgongoni akitaka kutoka nje atatoka tu.Mfano wangu mie nilimkuta mume wangu na msg ya msichana na tulikuwa atuishi wote yupo mkoa kikazi so kazi imeisha amerudi hapa dar so siku amelala nikachukua simu yake na kuanza kuangalia nikakuta sms msichana akimwambia amemiss period so ni dhairi kwamba walikuwa hawatumii condom niliongea sana na kumsihi kwann ananifanyia vile ila akunijibu wala kunisonya,nilichofanya kumpigia simu kaka yake na kumwambia kila kitu coz sio mara ya kwanza kumkuta na hicho kitu na tulikaa 1wk atuongei wala nn na nikiondoka alfajiri kuja job narudi zangu home saa nne usiku or saa tano so akawa anaumia kweli anapiga simu sipokei anatuma msg simjibu so baada ya wk moja kupita akaomba samahani so sio km nao awaumii wanaumia sana ni ww tu mwanamke kuwa na msimamo sio kila utakalosikia unakimbilia kulia sio ndio kumaliza tatizo inabidi umuonyeshe kuwa hata mimi napendwa ila nakuheshimu so dada kaa ukiomba kwa munguuuuuuuuu siku zote na atabadilika tu na kingine jaribu kushirikisha familia yake km unahakika na hayo anayofanya.
Kazi wao kutusema sie vipofu wakati hata wao viziwi na vipofu kwa hao wanawake zao wa nje.
Frm Halima.