Tuesday, November 30, 2010

MUME WANGU HANISHIRIKISHI KWENYE MAAMUZI YAKE-NIFANYAJE

Mume wangu hanishirikishi kwenye maamuzi ya familia, naona tu mabadiliko yanafanyika ndani, lakini siambiwi chochote, kazi yangu kupokea tu! Sasa nimesikia tetesi kuwa anajenga huko kwao, lakini mimi mkewe wa ndoa sijui chochote, cha ajabu mama yake mzazi ndio anajua kila kitu, na huyu ni mume wangu wa ndoa, tuna miaka nane kwenye ndoa yetu, ukimuuliza anakuwa mkali sana,  tumezaa watoto wawili mpaka sasa.
Mimi nina kazi nzuri tu na nina mshahara mkubwa Ambao naweza kufanya vitu vya maana, nilivyokwisha vifanya hadi sasa nimejenga nyumba 2, moja ndio hii tunayoishi na mume wangu, sasa mwenzangu ndio kanibadilikia sana, hata simuelewi, je namimi nianze kufanya mambo kivyangu??? Lakini naona kushare Ideas ni nzuri zaid, wadau nisaidieni naona nimetegwa  sana, na pia kwanini asinihusishe mimi mkewe?? Kajenga baa kubwa tu kwao! Lakini mimi Nimejua nilipokwenda kwenye msiba wa kaka yake,  nilipomuuliza ilikuwa ugomvi sana.na hadi sasa hata sielewi nilichomkosea


14 comments:

  1. endelea kushea ideas dada hilo nalo neno.

    ReplyDelete
  2. Sikiliza Vai, Kwanza nikushukuru kwa kutuletea hii mada tamu. Lakini pili kwa huyu mdada nimshauri kama ifuatavyo" Ndoa ili idumu inahitaji UVUMILIVU usiokuwa wa kawaida.Achana na upendo huu upendo unajitokeza siku ya kwanza pale mnapoonana tu, baada ya hapo kinachoendelea ni uvumilivu.

    Kuhusu mumeo kujenga kwao na wewe kutohabalishwa hilo lisikupe woga hata kidogo kwani mradi wewe hakunyimi haki yako ya msingi ambayo imefanya muoane na kilichofanya nyie muoane ni (unyumba) hakuna kingine. kama kipo niambie nifafanue. Na usije ukafikiri ni watoto, hapana! watoto ni wapangaji wanakuja na wataondoka. mlianza wawili na mtabaki wawili.Kama ambavyo nyie mliondoka kwa wazazi wenu ndivyo ambavyo na wao watakavyoondoka kwenu.Mvumilie mumeo ndoa itadumu. ukitaka na wewe kujibu mapigo tu, ndoa itavunjika. Kumnbuka iko siku atasema tu mke wangu twende ukaone mali yetu.........Kizito!!

    ReplyDelete
  3. Kwanza Napenda niseme Mungu wa Mbinguni akutie Nguvuili uweze kusimama na kujua haki zako.
    Nimejisikia kama mimi ndio nafanyiwa hivyo vitu,lakini jipe moyo kwani kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.
    Ushauri wangu kwako ni huu ebu mtegee mume wako siku ambayo unamuona amefurahi muulize sababu ya usiri wake ni nini?muulize kwa Upendo wala usionyeshe kwamba umekwazika atakapo kujibu ndpo utapata sehemu ya kumuelezana ikiwezekana mweleze athari ya kutoshirikishana.
    Hili pia linaweza kukusaidia fuatilia marafiki zake,na mawasiliano yake unaweza ukapata kitu kikakusidia,Nakunbuka mimi iliwahi kunitokea hali kama yako lakini kwa namna nyingine mimi mume wangu alikuwa ni mtu wa hasira kila siku lakini nilikuja kupata suluhisho baada ya kupata mawasiliano yake ya mail kumbe kuna watu wanamwambia kila siku habari zangu ambazo na za uongo na wakamwambia kuwa dawa yake ni kumfokea kila siku.Baada ya kugundua hilo ilibidi nimuombe Mungu pia na kukaa naye uwezi kuamini mpaka sasa anaogopa kuambiwa maneno na mtu kama nini.ila inahitaji uvumilivu sana na kutokujari sana maana ukisema uyabebe kila siku bp sasa hivi ni nyingi.

    ReplyDelete
  4. Bidada we, huyo mumeo anakufanya wewe kitega uchumi wake, akisha pata atakayo anaenda kuoa mwanamke mwingine na wewe kukuacha. Na kama si hivo basi itakuwa wewe haupendi ajiendeleze kwao, kwaiyo kaona bora hasikuambie. Pengine kaona akikushirikisha utamzuia hasiendeleze kwao. Cha kufanya, kama unaona hakushirikishi basi, lakini ela zako endeleza kwenu, jenga majumba tu na pangisha bila kumwambia mumeo, waambie jamaa zako tu, kama vile mama ako, dada zako, kaka zako nk. Akikulaumu mwambie mbona yeye anafanya hivo pia...Na hiyo nyumba pangisha bila kumwambia, wewe hamia sehem ingine na watoto, akikuliza kulikoni? mwambie mbona yeye anafanya vitu bila kukushirikisha, kwaiyo hauoni sababu ya kumshirikisha ufanyayo pia. Huyo mumeo hatari, atakumaliza

    ReplyDelete
  5. kuna kitu kinaendelea baina yako na mumeo, ni wazi kwamba hamuishi maisha ya kuelewana, kuna marumbano sanam ushauri wangu, muite mumeo kaa nae, jishushe, kuwa mjinga ili uijenge ndoa yako, yawezekana wewe unamringia kutokana na kazi yako ndio maana ameamua kufanya mambo kivyake, wanawake tukiwa juu kidogo huwa tunajisahau sana, sijui hata ni kwanini, pole lakini

    ReplyDelete
  6. Anonymous aliytoa comment mwisho nampa big up! hilo neno. Wanawake wengi mambo yao yakiwa mazuri huwa wanadharau kwa waume zao!

    ReplyDelete
  7. Ni kwa sababu dunia imetufundisha kuwa hivyo.Wanaume wengi mwisho wa siku wamekuwa wakinyanyasa wake zao kwa kuwa wategemezi kiuchumi ndani ya nyumba.Ukiangalia yapo matukio mengi ya wamama kuachiwa watoto,kutafutiwa vimada,ulevi wa kupindukia kwa sababu tu baba ndiye mwenye hela hivyo anatumia atakavyo.Wakati mwingine hata kufukuzwa au kila siku kutishiwa kufukuzwa ''nenda kwenu'',''toka hapa''.Nimeshawahi kushihudia mama mmoja akitupiwa nguo zake ingawa yeye mumewe alimwambia ahame ''chumbani kwake'' ahamie chumba kingine...yote hayo ni kwa sababu tu baba ndio mshika uchumi wa familia na mama yupo tu.Ilikuwa ni kama tu amemfukuza ndani,kibaya zaidi wana watoto ambao walikuwa wameshapevuka(miaka 16 na zaidi.Naona unaweza ukaona hata ungekuwa wewe ingekuumiza kiasi gani kuona mama yako anafanyiwa hivyo.Kwa hiyo mtoto wa kike aliyekulia mazingira hayo usitegemee akikua na Mungu akamsaidia kutoka atakuwa na mtazamo upi juu ya wanaume.Mungu atusaidie maana haukuwa mpango wake tufike hapo.Na hata ukiangalia dunia kwa ujumla watu wengi wenye pesa huwa na dharau kwa wale ambao kiuchumi ni hohehahe!kwahiyo unakuta huyu nae akipata anajua ndio wasaa wake wa kuonyesha ujuzi...WATAMKOMA!ANAENDA KUFUNGA BAA....!Kwa hiyo ni maswala ya kuyaangalia kwa upana zaidi.

    Wababa wakikupata mara ya kwanza utaona dunia yote yako,lakini wamama tusibweteke hata kama unapendwa na kudekezwa kama mtoto mdogo bado lazima ujifunge kibwebwe uwe na vyako.Kwa wasomaji wa biblia ile Mithali 31 mstari nimesahau kidogo unaelezea sifa zote za MKE MWEMA.Haijasema mke mwema ni mzembe,wala haijaruhusu uvivu utaona imeweka wazi kabisa lazima mwanamke ajishughulishe....huamka usiku haujaisha,hujifanyia mavazi ya kusokota,hulitazama shamba akalinunua kwa fedha ya mikono yake mwenyewe.Hali chakula cha uvivu,yani utaona imeandika mengi hadi kuhusu utanashati wa mumewe aketipo na wazee wa mjini.Naipenda sana ile Mithali imeainisha mambo mengi yampasayo mwanamke ili aitwe MKE MWEMA.Ingawa mwisho wa siku haijaruhusu tutukane/kudharau waume zetu.Sema tu huku duniani mivurugano mingi kiasi imeharibu mitazamo yetu wengi.Na tusipokuwa makini tunaweza kuwa pabaya zaidi,MUNGU ATUHURUMIE.Maana kwa saikolojia ya binadamu wote mara nyingi mwenye nacho ndio huwa ana kauli,kwa hiyo huwa tunaingia na hayo mambo hadi kwenye ndoa na matokeo yake kujisahau.Eeeh! Mungu Utusaidie,maana mvurugano wake ni balaa na ndio hupelekea mambo kama hayo watu ambao ni mwili mmoja hawashirishani katika mambo ya msingi kama hayo.Na mwisho wake ni kutengeneza familia zilizopasuka na hatimaye vizazi vilivyopotoka.Mungu atusaidie sana.Haikuwa mpango wake tufike huku.Nimeshawahi shuhudia familia moja baba akipata mshahara anapitia baa zikiisha ndio anarudi nyumbani.Na kama akijiskia kutoa hela ya matumizi nyumbani,basi akifika nyumbani atachukua hela kama ni noti ya tshs 10,000/= atapengea kamasi anarusha chini mkewe ndio aokote wakanunue chakula.Jamani nisiwachoshe na maneno mengi,ila ninachoweza sema wanawake tumeumizwa na aidha yaliyotukuta sisi wenyewe,au kushuhudia wazazi(mama) wetu au wanawake wenzetu wakifanyiwa na matokeo yake wengine tumekaa mkao wa kujihami tukiwaza UKIONA MWENZIO ANANYOLEWA WEWE TIA MAJI.Wengine ndio wanakuwa wababe kama hivyo n.k n.k...!

    ReplyDelete
  8. Shika ushauri wa anony 5.43, huyo ana ndoa imara, hao wanaokwambia achana mara pangisha hawajaolewa hao, hawajui ndoa ni nini.

    Si kila mwanamke akiwa na hela/elimu ni jeuri, hayo ni maneno ya wakosaji, achana nao.
    La mwisho, mtegemee Mungu katika kila jambo, simama katk maombi kila unapopata msukosuko ktk ndoa. Usishee na walimwengu hawakawii kukuongezea machungu.

    wanaume wengi/si wote ni selfish sana, ndoa nyingi zinapata tatizo kama lako. Mlilie MUNGU ALIYEKUPA HIYO NDOA AIREKEBISHE.

    Mwisho nakupongeza kwa kupata mume, wengi wanalilia hiyo nafasi hawapati, mshike usimuachie....

    ReplyDelete
  9. wewe wa hapo juu wala, nimeolewa na kwa taarifa ako, mie mume wangu hafanyi ujinga kama uwo. Sababu anajua kabisa mie nipo muazi na nataka awe muazi kwangu pia. Na akifanya jambo bila kuniambia nikaskia kwa watu, anaipata. Punda haendi bila mchapo. Kuwa peke yako kwenye ndoa za kijinga.Ila usishauri wengine waishi na machungu daima, kisa mungu. Kama mume hakuambi mambo makubwa kama hayo, jua hakuthamini,nakudharau, haufai kwake, anakuona mjinga. Na ukimuachia, ataendeleza kukufanyia hivo hivo mpaka muingie kabulini. Poleni wanawake mlio ktk ndoa za namna hiyo, mimi nazani munayataka wenyewe. Samaki mkunje angali mbichi.

    ReplyDelete
  10. Kuishi ktk ndoa kama hiyo, bora kuto olewa. Hao wanao lilia ndoa, hawana hadhi ya kuolewa. Kama unayo hadhi basi hata ukiachika utaolewa tena.

    ReplyDelete
  11. kuvumilia? eh eh, juzi kati shangazi wa mume wangu kafariki sababu ya kuvumilia ktk ndoa. Akishauriwa hivo hivo, vumilia mwana, mwanamke vumilia, vumilia mama wanaume ndio walivo. Leo wote walio mshauri avumilie wanajuta. Maana wamemuingiza mwenzao ktkt moto, sasa jupo kaburini. Mungu amlaze mahari pema. Huyo jamaa mumewe anadunda tu kwa raha zake na kuendeleza kuambukiza wanawake wajinga. siku hizi mtu inabidi unangalia nafsi yako tu, basi kama wanaume ni selfish kazi kwao, ila wasitese wenzao kwa uselfish wao

    ReplyDelete
  12. pole sana dadangu hebu niambie huyo mumeo hizo tabia ameanza lini mana kama ni toka mlipoowana ni msiri basi ndiyo tabia yake huwezi kumbadilisha lakini kama ameanza siku za karibuni huyo ana lake jambo kuwa makini mpenzi usibweteke ni wanaume wachache wanaoweza kuwaeleza wake zao mambo yao wanayofanya hata kama ni ya maendeleo mimi mume wangu nimeishi naye twelve iyers lakini mambo yake mengi huwa haniambii yani anaweza kununua gari nashtukia tu liko hom ndio anakumbia nimenunua namuuliza mbona hata hujanishirikisha anajibu kwani tatizo liko wapi kwa kweli hiyo tabia inanikera sana sijui nifanyeje nimeongea nae sana lakini habadiliki namwambia kuna leo na kesho hatuna maagano na mungu ukifa gafla huoni ni tatizo anakaaa kimya kwa hiyo nshamzowea tunaishi vivyo hivyo akijisikia kunambia poa asiponiam bia poa

    ReplyDelete
  13. Na madeni yake ya siri yote akifa atakuachia wewe.

    ReplyDelete
  14. utapata ukimwi ukiendelea na huyo.mpende akupendaye huyo hakupendi

    ReplyDelete