Sunday, December 5, 2010

TULIACHANA NA MUME WANGU, AMENINYANG'ANYA WATOTO NA HATAKI HATA NIONGEE NAO-NISAIDIENI


Hello dada yangu violet,
nahitahiji ushauri wako na wadau pia, mimi niliolewa na mume ambae sikumpenda in 2001 and I was 17 years old, ila nililazimishwa na wazazi. Tukafunga ndoa, ndugu zake hawakufika sababu walikuwa hawanipendi, sikujali sana sababu yeye aliiahidi familia yangu ya kwamba atanilinda

tuzaa watoto 3, ila mda ulivyokwenda nae alianza kubadilika, akaanza kunipiga, anarudi usiku sana, Siku zingine harudi kabisa, ilibidi nimshirikishe sheikh mkuu matatizo yetu,  sheikh alimuita lakini hakwenda.

maisha ya ndoa yalinishinda, nikaamua kurudi kwetu mwaka 2008, alininyima talaka, niliamua kuondoka kwa lazima pamoja na wanangu, alhamdulillah nilipata kazi nzuri nawasomesha vizuri

Baada ya muda nikapata safari kwenda UK ndipo nilipo hadi sasa,  watoto nikawaacha nyumbani kwetu, sasa yule bwana alienda nyumbani akawachukua watoto 2. Na toka awachukue, amekata mawasiliano na mimi, hata kuwasiliana na wanangu siwezi.

Nawaombeni wadau na  dada violet mnisaidie, nipeni mbinu zozote, sababu sijui lakufanya kabisa, nimesha tuma watu wakaongee nae aniache niongee  na wanangu, lakini kawakatalia  cha ajabu anasema atawapiga hata hao ndugu zangu  kama wakirudi kwake tena.plz help me sister, I miss my babies so much5 comments:

 1. Sasa wewe si ulisha waacha ukaenda zako UK. Na kama unataka kuongea nao bora uende huko huko kwa x wako ukaonge nao. Haki ya kukukataza na kukuzuia wewe husionge na watoto ulio watoa tumboni mwako hana. Nazani akikuona kwa macho yake, hatokukatalia, ataona aibu. Kwanza unajua watoto wako wanaishi vipi huko kwa baba yao? kama wanateseka je? na mama wa kambo? Wanawake wengine jamani, wanafikiria maisha yao tu, bila kujari watoto wao wanaishije. Mwisho munakosa watoto kwa maji ya moto. Ukisha teseka na huaribiwa huko, inakuwa mijambazi, inavuta mabaki wanakuwa hawana msimamo wa maisha, akina mama munapata hasara, mulibeba mimba bila faida

  ReplyDelete
 2. pole sana mdogo wangu,
  ni kwamba, huyo mumeo hana maana hata kidogo, ni vile tu uko mbali, lakini haki ya kukaa na watoto unayo wewe mama, hadi watoto wako wafikishe miaka 18 ndio watachagua wa kukaa nae, watachagua wao watoto, lakini kisheria ni miaka 18 mtoto anakuwa chini ya mama yake,
  Rudi uangalie wanao wanaishije wewe, unaagizia tu, unajua wamama wa kambo walivyo? au unawasikia tu? uchungu wa mwana anaujua mama aliewakamua wakat anawazaa, wewe umekaa UK, rudi wachukuwe wanao kama ni huko UK uende nao, hurumia watoto wako dada, roho inauma as if its me!

  ReplyDelete
 3. pole dada, naungana na mdau hapo juu, rudi huku uchukuwe wanao, au hata uje uone tu! wanaishije? watoto mlezi wao ni mama jamani, rudi haraka dada

  ReplyDelete
 4. Naomba uache usumbufu, Si uliwaacha ukaenda UK sasa unataka uongee nao nini?

  Kwanza uliwachukua watoto ukaenda nao kwenu, pili ukawaacha watoto ukaenda zako UK. mimi nafikiri huyu bwana ana huruma sana maana baada ya kuona mama yao (katelekeza watoto na kuhamia UK) akaona ni bora awafuate watoto na kuanza kuwalea katika malezi ya mzazi na watoto.

  Mimi nilifikiri wewe ungefurahi sana maana kawachukua watoto Kwanza hujasema UK umefuata nini maliza ulichokifuata huko ukirudi tuambie tukujulishe cha kufanya, kuhusu huyo mumeo na hao watoto.............Kizito!!

  ReplyDelete
 5. wewe mama rudi ulee watoto wako wewe, kama ni uk, rudi uwachukuwe uende nao, watoto wa mama dear, asikudanganye mtu, rudi uwachukuwe wanao, watoto wanafanyiwa mengi na mama wa kambo, hawajui wamwambie nani? baba hajui linaloendelea, jamani dada rudi ulee wanao, inaniuma sana mimi kwakuwa ishanitokea, nilikuta wanangu wana alama za fimbo, matatizo kibao, nililia kama mtoto mdogo, inauma dada rudi

  ReplyDelete