Friday, November 12, 2010

SHEMEJI ANANITAKA, NAOGOPA KUMWAMBIA DADA, NI MKOROFI NA PIA HATANIAMINI

Dada, nakupongeza sana kwa kuwa na blog nzuri, inatusaidia sana, mungu akubariki, mimi nina shida, ninaishi na dada yangu ambae tumechangia baba, ila mama zetu ni tofauti, baba yetu alikufa, ndugu wakamuomba dada anichukuwe anisomeshe kozi yoyote ile,

Nikahamia kwa dada , sasa toka nimefika hapa, shemeji yangu ananifata sana, ananitaka kimapenzi, kwa nguvu na kunitishia kuwa anaenisomesha ni yeye na sio dada yangu, hivyo nimkubalie tufanye siri, Ananifata hadi chuoni, ananinyima raha kabisa, mchana ananifata anitoe luch, yani ah! ananisumbuwa sana na namshangaa amekuwa na wivu hata kwangu, hataki nipigiwe simu na mwanaume, anapekuwa simu yangu, sana, nimejitahidi kumkwepa lakini wapi

Dada yangu ana asili ya kiburi sana, ni mkali kias kwamba hata mama yake anamuogopa, na yeye ndie ameolewa na mwenye uwezo kidogo, hivyo wote wanamtegemea yeye, sasa naogopa kumwambia tabia za mumewe,  maana najua kabisa hatoniamini, na atanifukuza nitashindwa kusoma,,

Ninawaza niwaambie watu wazima wamwambie dada, lakini nina uhakika 100% dada hatoniamini, maana hupenda kusemasema kuwa, akiskia mtu yuko na mumewe, yeye hatadili na mumewe atadili na yule anaemchukulia mumewe, sasa mimi nahofia kukosa masomo yangu, maan shemeji mwenyewe anamjua mkewe alivyo, na kuna siku aliniambia unafikiri ukimwambia dada yako ndio atanifanya nini? Acha ujinga wewe, hutamani maisha ya dada yako, wewe nipe uone ntakavyokupa maisha mazuri,
nakosa raha kabisa, nisaidieni kwa ushauri wadau

nifanye nini mimi??? Dada usiirushe email yangu please!!!

8 comments:

 1. mimi ni msichana kama wewe nakupenda ndiyo sababu nakupa ukweli. Kwanza kabisa wewe si mtu mwema kwa mujibu wa maelezo yako haiwezekani kama kweli dada yako unampenda ukamchambua katika aya ya tatu uliyoindika. Kilichotakiwa kama kweli ulikuwa hutamani kuwa na shemeji yako kimapenzi ungeeleza tu matatizo anayokuletea shemeji yako ndiyo tukupe ushauri. Kwa habari ya dada yako haina maana kumchambua mtoto wa mwanamke mwenzako kwani kila binadamu ana mapungufu sawa yeye ana kiburi wewe una nini? Kutembea au kutombea na shemeji yako amua wewe kwasababu dada yako anakiburi

  ReplyDelete
 2. Du, hapo pa kali. Hapo dada umekwama sana. Kwa lolote utakalo lifanya litaaribu masomo yako, na uhusiano na dada ako. Ukimkubali shemeji yako, jua tu dada ako atajua tu, haiwezi kufichika kama mumewe anavofikiria. Hapo utakosa vyote, uhusiano mzuri na dada ako na masomo. Ukimuambia dada ako, kama ulivo sema hatokuamini. Mie nazani nenda kawambie mama yako, shangazi yako kama upo ktk hali ngumu. Unaogopa kuaribu ndoa ya watu, na kuaribu masomo yako, na kuaribu uhusiano na dada ako. Wazee watakusaidia kuongea na dada ako ili wakuamishie sehem ingine ukasome. Sio lazma wamuambie kama mume wake anakufuatilia kimapenzi, maana ataumia pia,,,, pole dada.

  ReplyDelete
 3. jamani mimi nimpezi wa hii glob sana haipiti siku bila kuisoma mungu akubariki sana kwakuwa watu wanapata ushauri mzuri kupitia hii glob yako.Nawengi inawasaidi,sas mimi nina swali moja natakakuelewa.Hivi kuna maandiko yanayokataza haswa mwanamke kuolewa na bwana aliye chini ya umri wake yaani ninamaana mwanamke awemkubwa kuliko bwana ktk maandiko yeyote iwe ya kislam au kikristo naomba mnijuze wapendwa anayejua mstari hasa ktk biblia maana mimi ni mkiristo

  ReplyDelete
 4. Better keep quite, mashangazi wengi wambea sana, vumilia umalize shule

  ReplyDelete
 5. pole dada ndo dunia, nenda kwa wazee na uongee ukweli wao watashauri cha kufanya,ila wasimwambia dada yako hata kidogo kama mumewe anakutaka maana amani itatoweka,hata kama utahama basi kuwe na sababu nyingine,na huyo shemeji nae hana haya wala aibu!yaani hapo ndo nachoka na wanaume sijui wakoje!

  Emmy

  ReplyDelete
 6. Du!! mitihani tu ya mungu iyo wee usjidanganye shetani akakutia mashakani kutembea na shemeji yako..utatengwa mpka na ndugu zako wa baba mmoja na mama mmoja.Jaribu kutafuta mzee mmoja akupe ushauri jinsi ya kumueleza dada yako.
  yellow!!!

  ReplyDelete
 7. mimi ninachokushauri ni ujitahidi uhame hapo kwa dada yako,il i umkwepe huyo shemeji yako ,halafu kuhusu kumwambia mtu,umwambie tu mama yako maana watu wengine ni wachonganishi na pia dada hakiambiwa mtaGOMBANA ,we make any story ili uweze kuhama ,pole sana dada

  ReplyDelete
 8. Sikiliza kama Shemeji anakutaka ina maana amekuona wewe ni mkubwa! unafaa kutunza siri. hilo neno Dada ndio mwenye uwezo kidogo sio neno zuri ndilo linalokukosesha Amani, maana unajua mwenye uwezo kidogo akisikia atakufukuza. Wewe cha kufanya kwanza hama hapo nyumbani mwambie Dada yako kuwa unataka kuhama ili akili ikue(yaani isiwe tegemezi) ukihama hapo nyumbani Mungu atakufungulia njia nyingine. usimtamani Shemeji yako mbona wanaume wapo wengi.Na Dada ako usimwambie hii habari atakutimua kabla siku uliopanga haijafika. Na ukilala na njaa siku mbili akili itacheza utapata cha kukufaa..........Kizito!!

  ReplyDelete