Tuesday, November 23, 2010

MUME WANGU AMEOTA ANAFANYA MAPENZI NA MWANAMKE MWINGINE NINAEMFAHAMU- IMENICHANGANYA SANA HII, NAOMBA USHAURI WENU

Habari,
Mume wangu amenichanganya sana, siwezi hata kuwaza mambo mengine ya msingi, namuwaza yeye tu, nawaza nafika mwisho bila kupata suluhu, ndio maana ninaomba ushauri wenu
Hivi karibuni tukiwa njiani kwenda kazini, akaniambia kuwa ameota anafanya mapenzi na mwanamke mwingine, (alinitajia jina la huyo mwanamke, ni mtu ninaemfahamu vizuri sana, tena mimi na huyo mwanamke wala hatuivi, kutokana na kuwa na mdomo mchafu sana,
Sasa nashangaa na kujiuliza
1. Kwanini amuote yeye na asiniote mimi???
2. Kwanini aniambie ndoto ya kipuuzi kama hii?
3. Aliniambia ili iweje
4. Ingekuwa mimi ndio nimwambie yey enimeota nafanya mapenzi na mtu anemfahamu ingekuwaje?

Wadau naombeni ushauri wenu, ni jambo dogo bila kutafakari, ila ukilitafakari … inauma sana, ushauri please!!!!


12 comments:

 1. pole sana dadangu huyo mumeo ni mwendawazimu na anakuonyesha ni jinsi gani alivyokuchoka mwanamme yoyote mwenye akili timam hawezi fanya hivyo na inawezekana anatoka na huyo jimama jaribu kukaa nae chini umweleze ukweli ni jinsi ganiulivyojisikia na huku unafanya uchunguzi zaidi

  ReplyDelete
 2. huyo mumeo hana lolote, malaya tu!

  ReplyDelete
 3. Mi naona unacomplicate mambo tu, to me naona kawaida, sasa kama ameota afanyaje! unaweza zuia ndoto wewe! unavyoviota vyote huwa unavifanya au unavifikiria. Acheni kujipa strss za kijinga, na hao wanaocomment watakupa pressure zaid.

  Jamani, mjifunze kutake vitu easy, manalalamika ndoa ngumu kumbe wenyewe mnakuza mambo,.

  ReplyDelete
 4. ningekuwa mimi ningezua ugomvi mkubwa sana, hivyo nakusifu kwa kutoanzisha ugomvi, kwanza amekushusha heshima sana kwakukwambia ujinga huo, ni mbaya sana, na hafai hata kidogo, hii si isue kubwa, hili ni soo lililojitosheleza huu ni ujumbe wake kwako TASLIMU, muweke aseme alichomaanisha, au ndio anakutafutia sababu ya kukupa talaka??? kuwa makini na usilichukulie kirahisi
  fuatilia,

  ReplyDelete
 5. pole sana dada,mimi ninavyofikiri mumeo pia alishtuka kwanini aote anafanya mapenzi na huyo mwanamke na ndo maana akakwambia,kama wangekuwa na mahusiano sidhani kama angethubutu kukueleza,siku zote sisi wanawake tunapenda kujenga fikra chafu vichwani mwetu na kuwahisi vibaya waume zetu,sioni sababu ya wewe kuendelea kuumia,kama unaona inazidi kukutesa hebu muulize mumeo kwanini alikwambia kaota hiyo ndoto?atakachokujibu utajua kama kuna lingine ama ni ndoto tu!mwisho nakushauri usiwe unajenga fikra mbaya juu ya mumeo,shukuru Mungu amekwambia wewe mkeo kuliko angeenda kumwambia huyo mwanamke kuwa amemuota!

  ReplyDelete
 6. mh hizi presha zingine za kujitakiwa jamani...
  achana nae awe alisema kwa nia mbaya au snzuri atajiju,.....songa mbele bwana achana na stress za kijinga

  ReplyDelete
 7. Kama ange ota na angetaka kufanya nae mapenzi in real life angeuchuna tu na kumfuatilia akafaidi uroda wa ndoto in real life hehe. Naona mumeo yupo matatizoni na ndio maana kakushirikisha. Mwambie yule mama mchawi, anawangia ndoa yenu muachane. Nendeni kanisani mukaombe

  ReplyDelete
 8. ila jamani..kwanini amuambie ? angenyamaza tu..nyie mnaongea tu ila yangewakuta mmh

  ReplyDelete
 9. Naomba niungane na wengi hapo juu kuwa usichukulie kwa mtazamo mbaya mapema hata kuijpa stress ambazo hazipo.

  Inategemea na mumeo ni mtu wa aina gani.Kama mumeo amekuwa na kawaida ya tabia hatarishi katika ndoa yenu kweli unaweza kumwazia hivyo.Lakini me nashauri kama mumeo ni mtu mcha Mungu au tu ni mtu mpole ambaye muda mwingi mnashirikiana na mko pamoja huna haja ya kuogopa.Naamini atakuwa amekwambia kwa wema na huenda anajua uadui uliopo kati ya wewe na huyo mwanamke.Kama nyote ni wakristo salini maana huenda shetani amenuia kuiharibi ndoa yenu kupitia huyo mwanamke.Kwa hiyo kuwa makini,usije ukawaza vibaya sana hata kuchukua hatua zisizo nzuri dhidi ya mumeo halafu ukakosa mwana na maji ya moto.Nadhani unajua akili za wababa,au hata wewe mwenyewe mtu akuhisie vibaya wakati wewe hauko hivyo utajiskiaje.

  Ni kweli dunia imetuzoeza kuwa wababa/wanaume wamekuwa watu wa ajabu linapokuja swala la mahusiano ya kimapenzi hadi kwenye ndoa.Lakini kuwa makini si wanaume wote wakorofi.Na huwa inawaumiza kama yeye hayuko hivyo halafu ukamuhukumu kwa mazoea tuliyofundishwa na dunia,na ndio hapo unapoweza kumchokoza.Kwa hiyo kuwa makini,ndoa ni yenu na ule upendo uliokuwa nao kwanza na mumeo endelea nao huku ukiangalia nini cha kufanya.

  ReplyDelete
 10. Sikiliza wewe Binti unajifanya mfalme njozi.
  TAfsiri ya ndoto ni hii" NDOTO NI OPPOSITE YA MAMBO ULIYOYAFANYA MCHANA AU UTAKAYOYAFANYA MCHANA" Kinyume chake ndio ndoto.
  Sasa basi kama ameota hivyo basi wewe inakupasa kufurahi kwa kuwa kinyume chake atatembea na wewe! si ndio opposite yaani wewe ni opposite ya huyo rafiki yako? sasa unachosikitika ni nini? Hapo ndio anakuandaa wewe cha kufanya kanunue maua utampa mtakapokuwa mnarudi jioni mbusu na kisha mwambie nakupenda acha hasira za kijingajinga!
  Ndoto haina maana nyingine yopyote zaidi ya hiyo niliyokuambia.........Kizito!!

  ReplyDelete
 11. Na wewe siku moja mwambie umeota una do na rafiki yake tena kupitia tigo, uone atakavyo react!

  ReplyDelete
 12. Mamii pole sana kwa ndoto hiyo..kwanza shukuru Mungu kuwa ameamua kukushirikisha kuhusu hiyo ndoto ina maana anakuamini kwa kiasi kikubwa ndio maana akakuambia na akajua kuwa you will take it as a mature person angeweza kunyamaza kimya na wala usijue..mimi naamini kwa dhati kabisa kuwa ndoto si ndoto tu hivi ni viashiria au mawasiliano ambayo tunayaopata kwa njia ya kiroho ili kutuandaa in real life situations...kumbuka katika agano la kale Yusufu aliota, Ibrahimu aliota, Jacob aliota na wengine weengi tu na ndoto zote hizo zilikuwa na maana..sasa kiroho kama wewe ni mkristo kuota unafanya mapenzi na mtu ni kitu ambaco ni kweli kuwa unakuwa unafanya mapenzi na mapepo/(spiritual husbands/wives)yaani katima maana nyingine ni kuwa kuna maroho mabaya ambayo huingilia binadamu wakiwa wamelala na mara nyingi hawa huleta mifarakano katika ndoa na kuvuruga ndoa kwani baada ya muda hili likiendelea bila kufanyiwa maombezi huwafanya wahusika kutopenda kushirikiana kimwili na wenza wao katika ndoa...ingia katika maombia ya kumsaidia mumeo kuvunja hiyo roho ili isiendelee kumfuata mumeo na kufanya naye mapenzi.hebu ingia katika google halafu search hiki (40 common dreams--wahat they mean and what to do about them)kitabu kipo for free na kinasaidia katika kukuongoza jinsi ya kufanya maombi ya kuvunja laana mbalimbali zinazotokana na ndoto hizo.tusidharau ndoto wadau ni muhimuhuwa zinaashiria jambo, zinatuonya kuhusu tukio fulani,etc.

  ReplyDelete