Tuesday, November 9, 2010

NILIBADILI DINI NIKAOLEWA NA MUISLAM, BAADA YA NDOA NILIRUDI KWENYE UKRISTO, MUME WANGU AMEFARIKI, JE NATAKIWA KUKAA EDA???????


Habari ya kazi dada , mimi ni mpenzi mzuri sana wa blog yako, Dada nataka unisaidie mimi ni mkristo, nilibadili dini na kuolewa na muuislam  mwaka 2006 nina watoto 2 katika muda wote huo amani  kwenye ndoa yangu ilikuwepo

Lakini  mwaka 2008 mume wangu alianza  mahusiano na mwanamke mwingine  na kuamua kuzaa nje ya ndoa,  na hapo ndipo amani, na mapenzi vilikwisha,.

Sikuyapenda maisha yale hivyo nikaona bora nitafute njia ya kumrudisha  mume  wangu katika hali ya furaha na amani kama mwanzo,  nilirudi kwenye imani yangu ya ukristo na nilianza kwenda katika maombi kwa ajili ya kumuombea mume wangu, na kwakweli niliona mabadiliko na alianza kurekebishika

Lakini baada ya muda mume wangu alifarik. Kwa kweli niliumia sana  kumpoteza  mume wangu,  Sasa je  natakiwa kukaa eda? Hiyo eda ikoje? Au kwakuwa nilirudi kwenye ukristo haina haja tena ya kukaa eda,

Nisaidieni wadau9 comments:

 1. Pole sana kwa kufiwa na mumeo dada! Nakushauri usikae eda kwani ulisharudi kwenye ukristo na wakristo hatuna eda. Unatakiwa uwe na msimamo, usitange tange kwani dini haitakufikisha mbinguni cha msingi mkabidhi Mungu maisha yako.Pole sana endelea kumtazama Mungu atakusadia.

  ReplyDelete
 2. mimi naona kwa kuwa ulishaamua kurudi kwenye imani yako, bora uendelee huko, mambo ya eda achana nayo, maana utakuwa unajichanganya mwenyewe, upo kwenye ukristo halafu tena unafanya mambo tofauti na imani yako, ni dhambi, usifanye hivyo, wewe endelea na mungu tu, yeye ni mume wa wajane, atakutetea na kukusaidia, sawa mama?
  mama lilian tabata

  ReplyDelete
 3. pole sana dada,hiyo ni mitihani ya Mungu,tulia tu utapata jibu,ujue waislam huwa wanakaa eda ili kupumzika na kusali,pia kujitambua kama una ujauzito ama lah!ila all in all muombe Mungu sana.

  ReplyDelete
 4. dada nakuomba usika eda, haikufai wewe kwakuwa ulishaamua kurudi kwa mungu, cha msingi simama imara, magumu yote mungu atakupitisha, na atakuweka katika nafasi nzuri tu hata mume atakupatia,

  ReplyDelete
 5. kwani dada hii blog yako niyawacha mungu maana kila anaetoa maoni anajifanya nimktristu sana kwani waislam hawamuuabudu mungu nashindwa kuelewa inamaa wakristu ndo wanaomjua mungu pekeyao

  ReplyDelete
 6. mdau hapo juu, katika blog yangu hakuna sehemu yeyote niliyosema blog hii ni ya wakristo pekeyake, coz matatizo yanayowapata watu hayawapati waislam pekee wala wakristo pekee, yanawapata watu wa dini zote, so hata katika ushauri, ni mtu yeyote anaweza kuchangia, hata asie na dini, sasa hayo ya kusema blog hii ya wakristo yanatoka wapi? wewe kama ni muislamu si uchangie uone kama nitabana comment yako? nielewe, blog yangu ni ya jamii nzima.
  asante kwa kunielewa

  ReplyDelete
 7. asante kwakunielewa mimi c kuwa nania mbaya nilitaka kujua tu ok asante nakushukuru

  ReplyDelete
 8. kwanza lazima uwe na msimamo katika dini yako kama alijuwa uislam ni mgumu kwanini asingefunga ndoa yake Bomani kila mtu akawa na dini yake..sasa akipata mume mwingine muislam ata ludi tena katika uislam.ABUDU MUNGU KWA IMANI YAKO ACHA KUTANGATANGA UTAKUFA GHAFLA WATU WASIJUWE WAKUZIKE KWA DHEHEBU GANI..UNA EDA NA WALA MAANA YAKE UJUI MAANA KAMA UNAJUWA TANGU ALIVYO KUFA MUMEO TAYARI UNGEKUWA EDA USINGETAKA USHAURI..POLE KWA YALIO KUPATA NI MAMBO YA DUNIA
  yellow!

  ReplyDelete
 9. Bahati mbaya huyo Bwana ameshatutoka lakini kwa kuwa yeye ni Muisilamu imani yake inamruhusu kuoa wake wanne sasa basi kama mlikuwa wawili ina maana kuwa walibaki wawili tena ili mfikie wanne. Kwa kifupi huyo bwana kuoa tena hakuwa na kosa lolote.

  Tuje kwenye swali lako Wakristo hawana EDA hivyo kukaa EDA hakupo...........Kizito!!!

  ReplyDelete