Tuesday, November 2, 2010

NINA MAKOVU SANA KWENYE MIGUU YANGU- YANANINYIMA RAHA, NIFANYE NINI?

Tunapozungumzia urembo, hatuwezi kuacha kugusia suala zima la mvuto kwanza, haswa kwa kina dada, na hasa hasa kwa upande wa ngozi, iwe nyororo, ing'are ivutie zaidi bila kujali wewe ni mweusi au mweupe, mpango mzima ni MVUTO,  sasa hebu tumsaidie mwenzetu huyu. 


mimi ni mdada mzuri na mungu kanijalia kwa kweli namshukuru mungu kwa kuniumba hivi. Lakini nina tatizo moja tu linalonisumbua...nina makovu sana miguuuni, yani mengi sana, na yananinyima raha kabisa...nimeshajaribu vitu vingi lakini wapi, hayapungui wala kuisha. nimetumia beauty cosmetics lakini yanashine tu!

naomba msaada.  lakini nilivyokuwa mdogo nilikuwa mtundu kupindukia sasa utundu unanicost na vidonda na makovu naomba msaada wako na wengine mnaosoma blog hii kama mnajua dawa naomba mnisaidie.

ASANTENI
 
 

8 comments:

 1. pole sana mrembo, umekwenda hospitali lakini? mimi naamini ukienda hospitali kwenye maspecialist wa ngozi, utapata dawa ya kuyaondoa, mimi ninayo mikoni, ah! lakini wala hayaninyimi raha, maana nimezowea kuyafunika na nguo za mikono mirefu, sasa kama unavaa kimini na yako miguuni, mwenzangu haihusu, tafuta dawa uyatoe

  ReplyDelete
 2. pole ndugu yangu unajua unapopata matatizo hakuna kulala ni kuhangaika mpaka upate ufumbuzi utundo sio issue sote tulipokua wadogo tulikua watundu kuna waliokuzidi je umeenda kcmc moshi kumuona daktari bingwa wa mambon ya ngozi hebu nenda na kama una pesa unaweza kwenda hata india wenzetu wako juu kidogo kwa suala hilo jipe moyo jiamini na utapona

  ReplyDelete
 3. pole, mimi pia naomba mnisaidie nina shida hiyo hiyo jamani,. makovu yanyima raha sana, hadi napoteza confidence kabisa

  ReplyDelete
 4. mpendwa wangu, mimi nilikuwa na tatizo lingine tu usoni( sijui nilipaka nini, nilitokewa na vipere vya ajabu, hadi nilikuwa najiogopa, upele sana hadi juu ya lips, kila siku vinaongezeka, nikawaza sanaa, badae nikashauriwa kwenda hospitali regence, nikaenda Regency, pale nikamuona Dr. Mgonda, akanitibia, ndani ya wiki mbili tu! nikapona kabisa, hadi sasa, ukiniona utasema katoto usoni, ila ana watu wengi sanaa, na clinick yake huwa ni juma nne, ss sijui kama kwa sasa imebadilishwa, nenda, atakusaidia, wahi sana kwenda, maana folen huwa ni kubwa, hadi wengine huhamishiaw siku nyingine, gharama si kubwa kiviiile,

  yeye ni specialist wa mambo ya ngozi tu! hadi wenye tatizo kama hilo lako tuliwanao kwenye folen ya kwenda kwa dr. so wewe jitahidi uje Dar, then muone atakusaidia.

  ReplyDelete
 5. POLE DADA, MWANAMKE UREMBO BWANA,
  sasa mimi naona bora ujaribu kutumia dawa kabla hujaanza kwenda hospitali,
  mimi nilikuwaga na makovu sana, kama michirizi michirizi, mikononi sehemu za juu na chini ya mapaja, kwenye maungio ya goti, aisee nilikuwa vibaya hadi nilikuwa naumia kabisa, sasa jaribu kutafuta dawa moja inaitwa BAYO OIL, ni bei kidogo, mimi nilinunua mwaka jana shilingi 40, ka tyubu kadogo tu, but nilitumia tubu moja tu nikapona hadi leo, sasa jaribu na wewe inaweza kukusaidia, ikishindikana ndio uende hospitali

  MAMA AGNES

  ReplyDelete
 6. ngoja nikwambie dada yangu mimi nilikuwa na makovu nahisi hayo yako cha mtoto, tena yale maeusi fii kama yanayowata wenye ugonjwa wa kisasa, niliangaika huku na huko lakini wapi, mwisho nilikutana na dada naye alikuwa nayo hivyovyo na yalianza kufifia, akanipa ushauri tu kuwa huwa yanaisha yenyewe cha muhimu ni usiyafiche acha yapate hewa tu kama kawa, kama unavaa vimini vaa na endelea kupaka mafuta na sabuni za kawaida tu yanaisha, mimi yamechukua muda kidogo toka 2007 hadi leo ninavyoandika yanaonekana kwa mbali mno kama vile sikuwa na makovu napaka carlolite na maji yake tu. usipake cream kali maana yanazidi kuonekana. sarah

  ReplyDelete
 7. Sikiliza Vai mbona mguu uliotuonyesha ni wamwanaume? Kama ni mwanamke upandishe mpa kwenye paja tujue makovu yako chini tu au hata mapajani! Lkn mguu huo ni wamwanaume kabisaa.

  Sasa tuje kwenye hii mada Huyu mdada mwambie anywe maziwa Fresh asubuhi kikombe kimoja ya moto mchana kikombe kimoja na jioni kikombe kimoja.Lakini asitumie mafuta kupaka yale ya maji yale mazito yenye ladha ya sukari asitumie yale nafikiri yanaitwa Greserine asiyatumie kabisa. ndani ya mwezi mmoja atakuwa soft kinoma na makovu yatatoweka............Kizito!!

  ReplyDelete
 8. dada mimi ngoja nikupe ushauri mimi nilikuwa namabaka meusi kama mtu anajichubua usoni, wakati huo naishi tabora nilikwenda hospital zote za tbr wakawa wananibadilishia tube za kila rangi. ila siku moja nilienda duka moja la madawa hukohuko tabora sokoni. nikauziwa dawa nimeisahau jina nikawa napaka usoni tu baada ya wiki mbili nimekuwa soft na madoa sina tena meusi kama unandugu tabora mwambie aende phamancy ya sokoni huyo baba anaeuza ni kabila la mjalua ni maarufu hapo mjini atakununulia inauzwa elfu tano tu!karibu na stendi ya mabasi ya NBS kwa mbele kidogo.

  ReplyDelete