Thursday, October 28, 2010

USIMWAMINI RAFIKI KUPITA KIASI, (KIKULACHO KI NGUONI MWAKO)

Napenda niwakumbushe wadada wenzangu, jamani, hata ukiwa na rafiki yako, ukampenda vipi, usithubutu kumueleza kila kitu kuhus wewe, wengine huthubutu kueleza hadi madhaifu ya waume zao kwa marafiki zao, hi ni mbaya sana. maana kikulacho kiko nguoni mwako, huyo rafiki yako siku mkitibuana tu! anaweza bwaga mambo yako yoote, sometimes husema hata ya uongo mradi akuchafue tu! unaweza shindwa kufanya hata kazi zako kwa kufikira maneno machafu alosema rafiki yako.

Too much of anything is harmful, unaweza kuvumilia kidogo lakini kadri yanavyozidi huwezi kuvumilia tena na kujikuta mnaaibishana kama hivi, sasa yote haya ya nini? sijamaanisha ni marafiki woote, but kati ya marafiki 100, wanaoweza kukaa kunyamaza zikitokea miss understanding ni watatu tu! wengine hakuna kitu, ni aibu tupu

unaweza kusikia maneno ambayo ukiyatafakari unapoteza furaha kabisa, unatamani kulia kila ukimuona, but you cant change the situation hata ufanyaje, mbaya zaidi umpate rafiki ANEBORESHA TAARIFA LO! Utajuta kuzaliwa, maana hata usiyoyajua, anakutupia wewe,  (inakera sana hii, zamani mimi nilikuwaga najua mtu akisoma, basi hata behaviour yake inabadilika, kama alikuwa mmbea basi ataapunguza au kuacha kabisa, kama muongo, basi atadanganya kidogo, but i was wrong, hakuna cha msomi wala nini, (kuweni makini jamani,  mashosti hawafai hata kidogo,


Rafiki anaweza kupata ujasiri hata wa kuweza kuwagombanisha wewe na mumeo, kwa maneno ya uongo, kwa taarifa TATA, mradi tu mkose amani ndani ya ndoa, mbaya zaidi mumeo ayapate, lo! aibu mno, unaweza pata hasira ukatamani kutoa nywele kichwani, ukahisi miguu yote inatetemeka, meno yanajisugua kwa hasira, kila ukimuona unapata hasira kali sana, (marafiki msiwaamini sana jamani, wanatesa )

sio wote, but hata hao unaoona kwao ndio umefika, hakuna atakaewagombanisha, mh!
mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, msikubali kuwa wapumbavu, MUWE MAKINI WEPENDWA, NAWAPENDA SANAAA
6 comments:

 1. unachosema ni cha kweli kabisa violet, maana imeshanitokea mim, kuna mtu nilimwamini kupita kias, nikisafiri, familia yangu inakuwa mikononi mwake, kila mahari tupo wote, lakini alivyokuja kunigeuka, huwezi kuamini hapa juzi alifiwa na mkwewe, hata msibani sikuenda, amenisingizia maneno makubwa sana ambay menging hata siyajui, imeniuma sana na sitamsamehe hadi nakufa

  ReplyDelete
 2. HAHAHAAAAA, YANI UMENICHEKESHA KWELI HII MADA YA LEO, VIPI SHOST YALISHAKUKUTA NINI? MAANA ASILIMIA 100 YA ULIYOANDIKA NI KWELI TUPU, POLE MLIOCHELEWA KUJUA KUWA RAFIKI HAFAI, RAFIKI WA KWELI MOYO WAKO TU!

  ReplyDelete
 3. dada hayo uliyosema yote ya kweli kabisa ,mimi nilikuwa na rafiki yangu ambaye nilikuwa nampa kila kitu, kuanzia kulala hadi mavazi yake yote yalikuwa juu yangu, lakini alichonifanya siwezi hata kusema na muachia Mungu tu ndio mlipaji wa yote. maana amenichafua na bado anaendelea kunichafua kwa watu mpaka kune simu yaani mpaka wakati mwingine nachanganyikiwa kabisa. lakini nimeamua kukaa kimnya na kushukuru kwa mungu tu.

  ReplyDelete
 4. wanawake wambe sana, hakuna cha elimu wala nini

  ReplyDelete
 5. lakini da violet, mimi nafikir mtu akielimika basi na umbea unapungua, inakuwaje hapa? mimi mwenzenu maisha yangu ni ya peke yangu, watu wamesemaaaaa weee, anaringa, anajiona yeye ndio yeye, sijui ninini, lakini wapi? sijaacha nafasi hata ya nukta, staki shobo, staki kero, hakuna rafiki wa kweli kabisa, haswa kwa sisi ngozi nyeusi

  ReplyDelete
 6. Mie nimeishi uzunguni na nimeona wazungu wa kike kazini mashoga wanapendana sana, watoto wao wanavaa nguo zinazo fanana, upikiana, uendeshana, ufanya sherehe na familia zao ukutana. Sie wengine tukaona wengine wanabahati ya kuwa ktk urafiki nzuri.Baada ya mwaka kupita, naona wanavunjiana vioo vya magari, na kupasuliana nguo. Bosi akapiga sim polisi wakaenda kumalizia huko. Mmoja wao akaamua ahache kazi, yaani hata bosi hakuweza kuwapatanisha, sijui walibiana wanaume, lakini wote waliolewa na wanawatoto.

  ReplyDelete