Saturday, October 16, 2010

ANAPENDA KUFANYA MAPENZI NA MIMI NIKIWA KWENYE PERIOD, SIKU ZA KAWAIDA HAISIMAMI, NIFANYAJE NISAIDIENI.

(Wewe unaweza kuwa na tatizo, ukaliona lakwako ni kuuubwa saaana, kumbe kuna wengine wanayo zaidi ya kwako,hebu soma hii ya huyu dada, kisha mshauri wewe unaona afanyaje maana mh! )
Hi dada Violet
Ninatatizo na naitaji msaada wenu. Hapa najiona nipo njia panda sijui pa kuelekea. Nimeolewa juzi juzi tu, ila kinacho nichanganya mume wangu tunapo jamiiana huwacha kusimamisha uume wake katikati ya tendo la ndoa, hii ndo tabia yake kila siku. Wakati mwingine hasimamishi kabisa hata wiki, na akisimamisha basi haichukuwi dakika moja inalala tena,, Hii inanikera sana na kuniumiza. Na sasa imesababisha nisijiskie tena kujamiana nae, ingawa nampenda sana na sitaki kumsaliti.

TATIZO KUU:
Tukienda kulala ananijia na kuanza kunishika shika na anasimamisha sana, ila akisema aingize tu, kitu kinagoma. Hii inanichanganya sana na naumia sana ingawa simwambii. Maana nampenda mno.
Nikimuliza, anasema yeye pia anaumia kwa hili,. Hata yeye anashangaa, maana haijawai kumgomea hivi kwa wanawake wengine wa mwanzoni. Ananiomba nimvumilie, anasema hili tatizo ni la mda mfupi, litaisha. anachosisitiza ni kuwa ananipenda na nisimkimbie

Sasa najiuliza au mie simrizishi, hajiski chochote tunapojamiana na anaogopa kusema anachopenda.
cha ajabu kila tukienda kwa wazazi wake, tukirudi tu, siku hiyo atafanya kazi tam sana kitandani, sote mimi na yeye tutajiskia raha hadi basi. Ikitoka hapo basi,,hasimamishi, hadi nikiwa ktk period ataniganda kama luba, anataka ajamiane na mimi hivo hivo kila siku, sipumui. Hata kama mie naumia anasema pole mke wangu, anapenda zaidi nikiwa ktk hali hiyo. akimaliza ananicheka na kunibusu na kunikumbatia hadi asubuhi, yaani anaonesha upendo zaidi. Na period ikimalizika yeye hanitamani tena, anageukia huko.au husubiria kipindi ambacho sijiski kufanya tendo la ndoa, ndio husimamisha usiku wote kama chizi wa mapenzi. Hajui mie nateseka moyoni ingawa sisemi. Alafu naona kama vile mie ninapo umia yeye anapata raha na kuridhika.

Natumaini kupitia blog hii ya Violet, nitashauriwa,, mie nimejingiza tu ktk ndoa sijui A wala Z. Mie na mume wangu tunaumri sawa, tumefikisha miana 30, sio watoto tena sasa.

Naombeni mnishauri jamani. ASANTENI
11 comments:

 1. huyo atakuwa ni mchawi huyo, jiulize, kwanini apende damu? nenda kamshtaki kwa yesu

  ReplyDelete
 2. Yawezekana mmoja wenu ana pepo halitaki mpeane raha, anza maombi ya nguvu kuliondoa pepo.pole sana, mbona mateso hayoo.mana ukiwa kwenye period ni kinyaa kitupu wala mwanaume haipendezi ajue.Sa yeye ana enjoy nini hapi damu mh! makubwa

  ReplyDelete
 3. pole sana na kweli hilo ni tatizo kubwa jamani, lo! yani kuna mambo mengine unaweza waza usiku kucha usipate majawabu, kwanini mumeo awe hivyo, wakti wanaume wengine wakishajua uko kwenye period hata ukipika chakula hali, anaona kinyaa, yeye anataka akufanye huku una damu, lo! kuna kitu hapo, sio bure, kimbilia kwa yesu dada, muombee huyo atakuwa na pepo, tena la uchafu
  KUHUSU KWAO
  kutokana na maelezo yako hapo, ni wazi kuwa wana kiuchawi fulani hivi kwaenye familia yao, kuwa makini sana, yawezekana hata wazazi wake wanalijua hilo, kwanini asimamishe aktioka kwao tu! lazima kuna kitu wanakifanya, pole sana, dawa yake ni YESU KRISTO WA NAZARETH, YEYE hashindwi kitu hicho ni kidogo sana kwake

  ReplyDelete
 4. Du! pole sana mpenzi, tatizo lako ni kuubwa sana kibinadamu, lakini mbele za Mungu, ni dogo sana, ninachokushauri mimi ni kwamba piga magoti Omba, usiishie kulalamika tu, hii pekee haitoshi, omba, ikiwezekana shirikisha hata watumishi wa Mungu muombe kwa pamoja, huyu mumeo ana kitu kinachomsumbua, na analitambua hilo isipokuwa amekuficha, wala sio tatizo la kwenda hospitali hilo (jinsi nionavyo mimi) so the only thing i can advice to you ni Kuomba tu!
  pia mumeo anakuharibu kisaikolojia bila yeye kujua, na wewe unaumia taratiiibu na inaweza fika kipindi ukawa hutamani tena kufanya tendo hilo, kutokana na kufanywa wakati usio stahili, wakati tendo lile lahitaji wote wawili kukubaliana, sasa km yeye anaenjoy ukiwa na damu unadhani ni nini?? hilo ni pepo lililopo ndani yake linamsumbua, unakosea sana kukubali kufanya tendo hilo ukiwa kwenye period, unakosea sana mpendwa wangu, anakukosea sana, hata kama unampenda vipi, you have to be strong,Vitu vingine sio vya kubembelezana bwana, ni kwamba HAIWEZEKANI, basi HAIWEZEKANI, sikupi nikiwa ktk perion OVER. SS wewe umemzoesha hivyo, but hujachelewa bado,
  Kingine nakushauri, shirikisha wazazi wake, ni ngumu kwenda Direct kwao but waweza tumia wazee wenye hekima zao au hata mshenga wenu, ili afikishe hilo mlizungumze, but stopisha kumpa wakat wa period, anakudharirisha sana bila wewe kujua,
  POLE, TUNAKUOMBEA.

  ReplyDelete
 5. Pole sana kwa yaliyo kukuta dada, nimeumia as if ni mimi. nakuombea sana na ninakuonea sana huruma mpendwa wangu, ila kitu kimoja ambacho ninakushauri ni kwamba, nenda kwa wazazi kashtaki, huyo ni mpuuzi, na wewe inaonyesha ni mpole sana, huyo atakuwa ana nguvu za shetani huyo, anahitaji maombi, pia wazazi wake watakuwa wanajua kila kitu, wamekuficha tu! wewe nyamazam utakuja kutolewa kafara, shauri yako. SIMAMA KWA MIGUU YAKO, CHUKUWA HATUA, UTAUMIA AT THE END OF THE DAY,

  ReplyDelete
 6. pole sana dada, nakuhurumia sana kwa hali hiyo, Mungu akutee sana, ninachoona mimi ni kama alichosema dada violet, kwamba mumeo kuna kitu ndani yake, na anakijua, ni kama amefanya maagano navyo, cha msingi hapa mlilie mungu kwa bidii maana yeye hufanya njia mahali pasipo na njia, jitahidi sana kuomba mdogo wangu,
  MSISITIZO
  jiapize moyoni mwako kuwa huta fanya tena mapenzi ukiwa katika period, dada hii inakuharibu, inakupotezea amani, furaha, na kukufanya uwe kama mgonjwa, dada itakusumbua sana hii, usiintertain kabisa, kataa tena kuwa mkali, mweleze madhara yake, tena anaweza pata fungus yeye mwenyewe, kibiblia tukisema tutumie agano la kale, ilitakiwa wewe ulale chini na usishirikiane nae kwa lolote, it amazing my self so much, kuona mnafanya mapenzi na damu, lo! wewe dada, ZINDUKAAAA, kama alivyosema violet, UNADHARIRISHWA SANA wewe hujui tu hilo

  ReplyDelete
 7. NJONI KWANGU NINYI NYOOTE MSUMBUKAO NA KULEMEWA NA MIZIGO, NAMI NITAWAPUMZISHA,

  UNATAKA NINI TENA?? NENDA KWA YESU DADA, UTAPUMZIKA

  ReplyDelete
 8. Hi dada, pole sana na tatizo ulilonalo kwa sasa. Kama alivyokueleza mwenzako, hilo tatizo ni la muda, ki ushauri ni kuwa huyo anayependa kufanya mapenzi nawe wakati uko kwenye period ni kuwa wanaume huwa wanaathirika na tendo hilo kama atakuwa amefanya bila kutumia kinga. ukweli ni kuwa ule uchafu utakao na damu huwa na madhara kwa wanaume na dhara kubwa ni kupata mchango tumboni ambako anakuwa tumbo linanguruma sana. Huu ugonjwa unatibika kwa njia zote kiasili na mahospitalini.
  Mwanaume akiwa na aina hii ya mchango nguvu zake za kiume hupotea mara tu anatapotaka kuingiza uume wake. Hili liko wazi kwa wanaume wengi wanalijua ama limewatokea na wengine hawajui sababu yake ni nini! Hakuna dawa za nguvu za kiume zaidi ya hizo za kutoa mchango huo na kukufanya uwe na uwezo wa kusimama tena.
  Kibaya kwenye hilo ni kuwa mara nyingi athari za kushindwa kufanya mapenzi kwa wanaume hujijenga kwenye akili yake na akisha patwa na athari hii basi huchukua muda kurujea kwenye uwezo wake wa kujiamini kama anaweza tena. Na ndio maana ukiwa kwenye periods anataka kufanya mapenzi kwa vile huko ndiko alikokupatia athari hiyo! Mpeleke atibiwe hilo. Mtafute Dr atakuelezea na kama hilo tatizo mtafute mganga wa asili sio wa kienyeji watakusaidia. Maelezo haya mimi niliyapata kwa mganga wa asili Dr. Kifimbo. sina number yake ila nafikiri kuna watu watakuwa wanamjua na wanaweza kuwasaidia from there!

  Pole sana Dada!

  ReplyDelete
 9. NASHUKURU KWA USHAURI WENU. NITAJARIBU KUYAFANYIA KAZI. HOPE TO SURVIVE THIS...

  ReplyDelete
 10. si umeambiwa uende kwa YESU dada! sasa unangoja nini? nenda ukawekwe huru.

  ReplyDelete
 11. Hilo ni tatizo la kiRoho kwa sababu huyu aliyo kwa mumeo ni Jini mpenda hedhi!!

  ReplyDelete