Sunday, October 31, 2010

MWANANGU ALIWAONA HOUSEGIRL NA MUME WANGU WAKIFANYA MAPENZI- WAO WANAKATAA KABISA, NIFANYAJE?


nisaidieni wapendwa,
nilikuwa safarini Arusha kikazi, kwa muda wa wiki mbili, nyumbani nilimuacha mdogo wangu ambae ni mwanafunzi wa form three,  mume wangu , housegirl wangu na mtoto wangu mwenye umri wa miaka minne na nusu.

 niliporudi safari nikakuta amani kama kawaida,  na wala sijaona mabadiliko yeyote kwa housegirl wangu, kesho yake mume wangu nae alisafikir kikazi, yeye ni dereva wa Bank Fulani hapa Dar es salaam, sasa baada ya kusafiri, usiku niliamua kulala na mwanangu,
nilishangaa  sana mtoto akaniambia mama basi ulipoondoka dada alikuwa analala  na baba huku chumbani kwakowananichukuwa na mimi, Violet, nilishtuka sana, nikamwambia unasemaje? 

Akasema kweli mama, baba alikuwa anavua nguo na dada anavua halafu wanalaliana, nikamuuliza mama mdogo alikuwa wapi? (nikimaanisha Yule mdogo wangu) akasema sijui mwenyew, basi nikaamka usiku huo huo nikamuamsha mdogo wangu nikamuuliza kama aliwahi kulala nje ya nyumbani wakati sipo, akasema ni kweli rafiki yake alifiwa, hivyo alitakiwa kuwa kwenye msiba kwa siku mbili,..........

 Mschana nimembana sana, amekataa kata kata yeye hajawahi kulala na mume wangu, mume wangu nae  amekana kabisa, sasa sielewi, huyu mtoto hata leo hii umuulize nilipoondoka baba alikuwa analala na nani, anasema na dada, niambieni nahisi kichwa changu kimeruka kabisa, nifanyaje? 15 comments:

 1. pole sana my dear mimi ninachokushauri umfukuze huyo house girl watoto huwa hawasemi uongo tena kwakitu kama hicho labda anekwambia dada amemupiga hapo kwahilo mtoto anaweza akadanganya,plz usimfuge mke mwanzako ndani,nauhuyo mumeo tafuta jinsi ya kukomesha,mtoto hasemi uongo huo niukweli kabisa

  ReplyDelete
 2. dada yangu nakushauri umkamate uyo housgirl upatie kichapo cha mbwa mwizi.halafu umfukuzie mbali yani mimi imeniuma utadhani imetokea kwangu natafuta means ya kumfundisha adabu huyo mumeo maana ni mshenzi mwenye laana toka siku aliyozaliwa ,kwali pole sana dada yangu

  ReplyDelete
 3. fanya uchunguzi, usikurupuke tu! kumfukuza housegirl, pengine huyo mtoto kaota, wanawake mnamaamuzi ya ajabu sana, yani wote mnacoment amfukuze mfanyakazi, mnahakika gani na maneno ya mtoto, je kama ametumwa aseme hivyo,
  acheni hasira za ajabu ajabu bwana. wewe chunguza kwanza,

  ReplyDelete
 4. Pole sana dada! Usichukuwa maamuzi ya haraka, kama wote wawili wamekataa endelea kuwachunguza kwani za mwizi ni arobaini kama ni kawaida yao utawagundua tu. Endelea kumtegeamea Mungu naye ataiponya ndoa yako! Muombe Mungu bila kuchoka atakusaidia!

  ReplyDelete
 5. we kaka utakuwa mwenda wa zimu kama sio kichaa kabisa, eti mtoto kaota, asiote mambo mengine anayocheza na wenzie siku nzima aote kitu kama hicho, na usikute ndio tabia yako hiyo ndio maana unataka kutetea, wewe dada, mtoe huyo housegirl haraka sana, mkimbize kabisa, hafai hata kidogo, amani maneno ya mtoto, ndio maana mahakamani akitoa ushahidi mtoto, na kuthibitisha, basi mshtakiwa umekwisha, wewe kaka ACHA KUTUPOTOSHA BWANA

  ReplyDelete
 6. dah me naamini mtoto huwa hasemi uongo, kwann aseme walikuwa wanavua nguo halafu wanalaliana? lazima kuna ukweli, cha kufanya mtoe huyo housegirl haraka iwezekananvyo then angalia cha kufanya na huyo mumeo, pole mwaya

  ReplyDelete
 7. Unaweza kununua video camera au recoder, alafu kila ukiondoka unaiwasha na unaificha chumbani mnapo lala wewe na mumeo. Itawarecodi tu, na utakuwa ushaidi nzuri. Hao ni wapenzi wa siku nyingi sana dada. Ila 40 yao imefika, ndugu yako alipo ondoka walipata uhuru mkubwa, na hawakufikiria kama mtoto wa miaka 4 anaweza kusema kwa bahati mbaya. Vizuri umejua mama.Husiamue vitu haraka haraka bila kuthibitisha mwenyewe dada. Mfano, unaweza kujifanya unaondoka kikazi, kwa wiki mbili, lakini unaenda kulala gesti siku moja, na siku ya pili unarudi saa tisa za usiku, na fimbo au gongo kubwa. Ukiwafumania,unampika mumeo mukisaidiana na mdogo wako, hehe. Hato fuata tena mahousegirls wako.

  Maana ukimpiga house girl na kumfukuza, haito saidia, utasababisha mumeo amurumie hausegal, sababu ni kosa lake kamlaghai mtoto wa watu. Na atamfuta tu kumuomba samahani, na kumtimizia ahadi alio muaidi. Na ndo hapo hapo housegal kwa maasira yake anaweza kuendelea kimapenzi na mumeo ili akulipishie ushenzi. Utabaki unalia tu mama, mumeo atampangia chumba uko na kumfanya mke wa pili, bila wewe kujua.

  Unamkunguta na unawwambie housegal kuwa analaghaiwa kimapenzi na huyo bwana. Nafikri hausegal ataondoka zake mwenyewe na hato mtaka tena, hehe. Na ilo dume litashika adabu yake, na atajiona mpumbavu maana umemgutukia mawazo yake

  ReplyDelete
 8. Chukua simu ya housegirl nenda nayo ofcn, au danganya unasafiri, lala gesti siku ya kwanza ya pili ibuka usiku home

  ReplyDelete
 9. aga tena una safari uondoke na mdogo wako,...halafu urudi ghafla utajua ukweli..heeh yukoje huyo mumeo ..hausgal ?? loooh nadhan ningekua mimi ningempa kipigo ..na angeenda kulala polisi wiki nzima !!

  ReplyDelete
 10. mmhh wadada mnaniogopesha, yaani wote mmekimbilia kusema housegirl apigwe , unahakika gani ni yeye? pengine aliletwa mdada mwingine? halafu ni mwanaume gani mwenye akili timamu atafanya ushenzi huo mbele ya mtoto ambae ameshajua kuongea? jamani fikirieni mara mbili, mimi naunga nahuyo aliesema ufanye uchunguzi kwa siri halafu ukishapata ukweli chukua hatua, na kama tatizo liko kwa huyo baba ina maana huyu mama atakua akifukuza house girls kila siku. mchunguze mumeo kama ndio tabia yake basi amua cha kufanya

  ReplyDelete
 11. we anonymous wa 1:10 hapo juu utakuwa mgonjwa wa akili kama sio punguani, mtoto huyo mdogo kiasi gani hadi asimtambue dada yake anaishi nae kila siku, tatizo letu watanzania hatupendi kuukubali ukweli na kuuamini hadi tudanganywe, mtoto ni kama malaika, na kwanini aisisingizie kitu kingine, kwamba labda mama ulipoondoka baba alikula na dada, yeye anasema walilaliana na dada, lo! NI UKWELI MTUPU, UCHUNGUZE ILI IWEJE, we zubaa uletewe mtoto wa housegirl hapo, mtoe fasta sana kisha ndio udeal na mumeo, wanaume kwani wana akili sawa, mie huwa naona kama punguani vile, pengine walihis mtoto kalala, wakaleta ushenzi, watoto wajanja, anawezajifanya kafumba macho kumbe anachapo, mimi naamini maneno ya mtoto asili 1000% TIMUA HUYO MSCHANA

  ReplyDelete
 12. POLE DADA KWA YALIOTOKEA. ILA MIMI NAKUPA KWA UFUPI KUNA JIRANI YETU YALIMTOKEA MATATIZO KAMA YAKO NA MDOGO WAKE NDIE ALIYE GUNDUWA KAMA SHEMEJI YAKE ANATEMBEA NA MSICHANA WA KAZI.NA ALIPO MWAMBIA DADA YAKE DADA YAKE AKAMWAMBIA SHOGA YAKE ILI AMPE USHAURI NA SHOGA ALIMSHAURI KUWA ASIPANIKI ACHUNGUZE KWANZA LABDA MDOGO WAKO APATANI NA MSICHANA WAKO WA KAZI NDIO MAANA KAMZULIA.NA KAMA YEYE MSICHANA WA KAZI NA MUMEO WA MEKANA TENA KWA KUAPA.TULIA CHUNGUZA...BASI SHOGA IYO CHUNGUZA JAMAA ALIENDELEA KULA MZIGO NA MIMBA SASA JUU..SASA NA WEWE POTEZA MUDA KWA KUCHUNGUZA NDIPO ATAPOKUWA VIZURI MKE MWENZIO NA MIMBA JUU. MTOTO ADANGANYI ATA SIKUMOJA NA WALA YEYE AJUI ALICHOKWAMBIA WEWE KINAUMUHIMU KIASI GANI...UKICHELEWA KUMTIMUWA MIMBA ITAKUJA!!!!yellow

  ReplyDelete
 13. Hata sie wanawake akili zetu hazipo sahihi vilevile. Mie nawashangaa sana nyie wanawake munao kimbilia kusema hamukumu housegal, na adili na mume wake. Mwanamke mwenye mawazo timamu hawezi kudili na mshenzi. Huyo mwanamme ni mshenzi anakulaghai wewe pamoja na housegal wako dada. Na kama haukumstopisha mumeo tabia yake chafu, mwisho atalala mpaka na ndugu zako, na mpaka watoto mutao wazaa. Mwisho utafukuza ndugu zako mpaka watoto wako. Sababu anajua hauto mfanya lolote, na atakuona mjinga wa mawazo

  ReplyDelete
 14. Pole kwa yaliokukuta naelewa maumivu ya mapenzi, baada ya kuipitia hiyo sms yako inaonekanwa uwezekano wa mumeo kufanya hicho kitendo cha kinyama na cha kishenzi ni mkubwa kwanini nakiita cha kinyama inawekana wanaume wengi wanafanya mapenzi nje ya ndoa lakini si kwa house girl kwani ni sawa na mwanao inaonekanwa hata mwanawe anaweza kumuingilia isitoshe kwenye kitanda mahsus ambacho no specially kwa wewe na yey.

  USHAURI: kwa vyovyote huyo house girl ni lazima aondoke lakini usimuondoe kinyama mtu yeyote akifanya kazi hizo huwa ana shida naomba endelea kumsaidia kwa vile kosa si lake pengine mumeo kamtisha pengine katumia udhaifu wake wa umaskini kwa kumpa fedha vyovyote itakavyokua mumeo ndio mwenye makosa hivyo muondoe namsaidie na MUNGU ATAKULIPA hapa hapa duniani jengine kama unaweza kazi zako mwenyewe hakuna sababu ya kutafuta house girl mwengine because mumeo anaonekanwa si muaminifu, utata unakuja kwa huyo ndugu yako ya kike kama hakuna sababu za msingi za kuwepo ningekushauri ukamuondoa kwani mumeo anaonekanwa ana sexuel harissment so utakapo safari anaweza kutumia mbinu yeyote na huyo ampe na hapo ndio utakua uhasama mkubwa kwenye familia yenu jengine si vyema kuvunja ndoa kwa maana hiyo sikushauri kuvunja ndoa ila mueleze ukweli ikiwezekana mbele ya wazee wake na wako na mtake awache tabia hizo la ziada mtishe huyo mtoto kabla kuondoka kwa sisi waislamu huwa tunatishia aseme au utamsomea albadir sasa yeye mtishe kwa njia zozote au tumia njia za kirafiki tumia pesa almradi wewe una akili jaribu ukishindwa basi uamuzi na huo nilikupa mwanzo suala la ndoa usivunje muachie MUNGU yeye ndie hakimu wa haki and i promise atalipa hapa hapa duniani

  ReplyDelete
 15. pole sana dada ushauri wangu huyo beki tatu muondoe haraka sana watoto huwa hawasemi uongo tena usimwambie mumeo kama unamwondoa fanya kumshtukiza huyo dada alfajiri fungasha virago uondoke itakuwa vizuri kama mumeo akiwa safarini halafu kaa na mumeo umseme sio vizuri anavyofanya ajirekebishe magonjwa mengi siku hizi

  ReplyDelete