Monday, October 25, 2010

MCHUMBA WANGU YUKO SOUTH AFRICA- HAJISIKII KUWASILIANA NAMIMI, NAMI NAMPENDA SANA, NIFANYAJE


habari mpendwa,

mimi ni msichana wa miaka 25, naomba mnishauri maana niko njia panda,nilikuwa na boyfriend wangu ambaye anafanya kazi south africa sasa huu ni mwaka wa tano hajarudi na kila nikimuuliza anasema anakuja kesho na kesho kama unavyojua huwa haifiki,nyumbani kwao wananijua kuna siku mama yake alimuuliza anarudi lini ili aanze kufanya maandalizi ya harusi lakini akamjibu bado baada ya hapo akanipigia simu na kuanza kunilaumu kuwa nimeenda kumwambia mama yake kuwa ye hataki kurudi, yaan nimechanganyikiwa maana zamani alikuwa ananiambia mambo yake yote lakini sasa hivi hata nikituma sms inaweza ikajibiwa baada ya wiki au isijibiwe kabisa, naombeni ushauri wenu jaman maana maji yamenifika shingoni.
6 comments:

 1. my dear usome alama za nyakati ,huyo hakuitaji tena ,kisicho ridhiki shoga hakiliki huyo siyo riziki yako raha ya mwanmke nikupendwa so tafuta mwinginee

  ReplyDelete
 2. kuna wawtu mnamoyo wa KOKOTO JAMANI, AH! yani miaka 5 yooote unajihesabu bado mchumba, mh! sina hata cha kukushauri, maana umeshajishari

  ReplyDelete
 3. Mdogo wangu pole kwa yaliyokukuta nimekuonea huruma saana,ila ninachotaka kukuuliza ni je amekutolea posa au ndio ulikuwa urafiki tu,nataka kukuambia uchumba sio ndoa,naikiwa hawa kaka zetu wa kambo hata ndoa wanaacha tu wakipata kipya sembuse Uchumba?Jipe moyo bado ni mdogo sana changamka kukiwa bado mchana maana usiku unakuja.Miaka 25 bado ni mdogo bado una nafasi na muda wa kuweka mambo yako sawa,Yasije yakakupata kama yaliyonipa mimi,Mimi nilichumbiwa na kutolewa mahari nilisubiri kwa miaka minne ndipo nakuja kuambiwa kaka wa kambo ameoa na tayari mke ana mtoto.Ushauri wangu kwako ni mpigie simu muulize kama bado anakupernda,mweleze ukweli kwamba kwa jinsi inavyokwenda umekosa imani nae,hivyo akueleze ukweli kama yupo tayari kukuoa au ana mtu mwingine.
  jipe Moyo kwani kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho

  ReplyDelete
 4. Kimbia haraka, achana na habari ya kuuliza na jibu unalo, anza maisha yako, sali mlilie MUngu, mume mwema hutoka kwa Mungu, Looh! I give glory to Jesus Christ, jaman amenipa mume mwema sana. Omba omba usichoke soon utaolewa na mume mzuriiiiiiiiiiiiii hutaamn, achana na huyo asiyekupenda

  ReplyDelete
 5. Pole dada kwa yaliyokukuta ila ushauri wangu ni kuwa kwa maisha ya sasa hivi ya hawa wanaume wetu huyo si mwenzio jaribu kukaa utulie na uangalie maisha yako mengine. Mie nina shida ya kutaka kutoa topic yangu na mie inayonisumbua lakini nashindwa nifanye nini naombeni mnielekeze mwenzenu

  ReplyDelete
 6. dada hapo juu, naomba nikuelekeze jinsi ya kutuma mkasa wako,
  baada ya kuandika, tuma kwenye email yangu mimi, then mimi ndio nitaurusha, tuma kwenda
  violet.gerald@yahoo.com utanifikia bila shida,

  ReplyDelete