Wednesday, September 8, 2010

NAHISI RAFIKI YANGU ANATEMBEA NA MUME WANGU - NIFANYAJE
 Habari za mapumziko Violet,
mimi ni imeolewa na nina mtoto mmoja wa kike, lakini sina furaha ya ndoa kama ilivyokuwa zamani, mume wangu ni mtu wa ugomvi sana, kitu kidogo tu! Anakibeba kinakuwa kikubwa, chuki zake kwangu hadi kwa mtoto wetu, basi nilijaribu kumuhadithia rafiki yangu mmoja, na nikamwambia kuwa ikiwezekana akaongee nae mume wangu maana naona wanaelewana, (nilitumia heshima)

Basi sikumoja nilimualika rafiki yangu aje mahali tukutane, nikamuomba ampigie sim mume wangu ili nae aje, nilimwambia atumie  namba yake maana imefika kipindi nikimpigia kwa namba yangu hapokei, basi nikampa rafiki yangu ampigie,

Alipokuja akanikuta namimi nipo alichukia na kuondoka, violet, hadi sasa sijui nilichokosea, but yeye amekuwa ni mlevi sana, akirudi wakati mwingine huwa analala na viatu na nguo kama alivyokuja hadi asubuhi, kuna baadhi ya siku huwa ananyea hadi chupi zake, ukimsema tu! Inakuwa ugomvi,

Rafiki yangu aliahidi kuongea nae, kweli baada ya siku tatu akampigia simu wakakutana kwenda kuongea, nilimwamini sana rafiki yangu na sikuhisi kama angenichukulia mume wangu, baada ya hapo rafiki yangu nae akaana kuonyesha kiburi kwangu, hanijali, wala kushauriana nami akawa hataki tena

Sasa siku moja rafiki wa mume wangu ndio akaniambia, shemeji chunguza mwenendo wa mumeo na rafiki yako nahisi si mzuri, nikamwambia sawa shemeji, ssasa kuna siku moja nikiwa naipekuwa simu ya mume wangu, nikakuta picha ya huyo rafiki yangu kwenye simu ya mume wangu, tena inaonyesha wamepiga bar, usiku, maana kulikuwa na chupa za bia, naogopa hata kuuliza,  maana kauli zake sasa hivi ni ''kama umechoka fungasha nenda kwenu, kwani ndoa kitu gani'' yani inshort hataki discusion za family

nishaurini nifanye nini?
5 comments:

 1. unaogopa nini? wawashie taa wote, akikutimua ondoka na usiishi kama mtumwa, pole sana,
  hujui kama dunia ya sasa rafiki ndio adui wako mkubwa? pole sana

  ReplyDelete
 2. Sikia Dada siku zoote malipo ni hapa hapa duniani mface rafiki yako mwambie nashukuru sana kwa yoote pia mweleze na mumeo umegundua kitu akikufukuza ondoka kaishi kwenu ila lia na mungu wako piga goti lako mungu atawaunguza tuu usisononeke wala nini as long as una kazi yako fanya kazi ndo awe mume mwachie hata kibiriti ni laan moja wapo kaa kwenu jipange na wala usilipize kwa kutafuta mtu mungu atakuletea mtu utashangaa na ipo siku huyo huyo mumeo atakuja piga goti wakati huo wewe uko mbali lia na mungu wako mweleze uliolewa uteseke,Na kma ni mume wako halali basi akupe ...Utakuja toa ushuhuda humu humu kwa dada Vai

  ReplyDelete
 3. POLE SANA DADA MARAFIKI NI WATU WABAYA SANA. UKISHAOLEWA HUTAKIWI KUWA NA RAFIKI WA KUJA NYUMBANI MARA KWA MARA MNAONANA HUKO KAZINI BASI MNAMALIZA MAONGEZI IKITOKEA KAJA NYUMBANI UNA SHEREHE UNAMUALIKA NA SIO KUJA MPAKA MUMEO AMZOEE. MIMI NDIVYO NINAVYOISHI KWASABABU MIDUME DUME HAIFUGIKI. SIJUI TUWAFANYE NINI HAWA WATU NI KUWAOMBEA TU. MAMAAA JOSE

  ReplyDelete
 4. best hapo juu uliyesema ushoga uishie oficini umenifundisha kitu mm ndio kwanza mgeni ndoani nna ndoa ya mwezi tu na nikiangalia mashoga zangu wengi ndoa zao zimevunjika tena za kanisani kwa kweli ushoga itabidi uishie kwa ofisi tu mana kaaz kweli kweli

  ReplyDelete
 5. pole sana, nimeguswa sana jamani, kweli wanawake tunateseka sana kwenye ndoa zetu, dada mpendwa una kazi ya kukuingizia kipato ?? mna watoto ?? jamani... nimesikitika sana nitakuombea mpendwa, mimi nimeolewa nina miaka zaidi ya 8 na mume wangu na leo ni birthday yake na mimi niko mbali na nyumbani (nchi nyingine ) ila nilijitahidi kukesha hadi saa sita za usiku nimuimbie...kwakweli sijaona kama yeye, namshukuru sana Mungu.

  ReplyDelete