Thursday, September 16, 2010

MUME WANGU ANAWACHUKIA SANA WATOTO WETUHabari wadau wote kwa ujumla,
Mimi nina shida moja ambayo pia hata sielewi imetokea wapi, maana zamani haikuwepo kabisa,

Mume wanguAmekuwa ni mtu mwenye hasira kila akirudi nyumbani, sijui kama na kazini kwake huwa yupo hivyo,Hanywi pombe, na kipindi cha nyuma alikuwa ni mstaarabu sana, Mungu ametujalia kuwa na watoto wawili waliopishana kidogo, lakin baba huyu amekuwa akiwachukia sana, hadi watoto wamejua kama wanachukiwa, yani akirudi watoto hata kama walikuwa wanacheza wanakaa kama wamemwagiwa maji, nikijaribu kumuuliza ni ugomvi, anasema acheke cheke amekuwa mgonjwa wa akili?, yani ana majibu ya karaha sana, hadi tunaona bora awe anakaa kazini muda woote
Hata kutoka nao siku hizi hafanyi kama alivyokuwa akifanya zamani, kwa mwezi mara mbili, anawapeleka beach, au sehemu nzuri nzur za kupumzika, lakini siku hizi, mh! Hataki hata umgusie suala hilo, sasa mimi linanishangaza sana, na pia naona kabisa linavyotesa watoto, hivi violet, ni hii ni hali ya kawaida kweli? Yani mzazi mzima ukachukie watoto wako mwenyewe? Maana ile ni damu yake,

Nishaurini kwa wale yaliyowatokea kama mimi, au hata kama mna idea zozote mnishauri ili nijuwe cha kufanya kitakachorudisha furaha ya zamani
5 comments:

 1. hilo ni pepo kabisa, kazana kumuombea, haiwezekani achukie watoto gafla tu, from no where, piga goti omba, mungu atamnyoosha tu!

  ReplyDelete
 2. mhh sitaki kukutisha ,ila ANA NYUMBA NDOGO HUYO,CHUNGUZA ...

  ReplyDelete
 3. labda ana matatizo kazini,au kitu kinamsumbua anahitaji utulivu wa akili,so linapokuja swala la kurudi nyumbani,watoto wanasumbua,anakua na hasira nao.jaribu kumshirikisha Mungu kwenye swala lako.kua na Imani

  ReplyDelete
 4. dada ulietaka ushauri, kitu ambacho mimi nahisi kuwa kinaweza kuchangia haya kutokea, ni mahusiano mliyonayo kati yako wewe na baba watoto wako? je upendo upo kati yenu? mnaheshimiana? una hakika hakuna vikwazo vyovyote vinavyomdisappoint huyo baba?? coz ninavyohisi mimi, kama ninyi mtakuwa hamuelewani, ni wazi kuwa kila mmoja wenu hatokuwa na hamu na mwenzie, labda akirudi home wewe kama mama humpatii huduma zinazotosha kama baba, huwajibiki ipasavyo, thats why hata majibu yake yanakuwa dry, you know, wanaume ni kama watoto vile, japo nao some times wanabore, but wewe kama mama unafanaya majukumu yako ipasavyo? suala la kusema yawezekana ana bi mdogo nje, mmmmmmmmmm sina hakika nalo sana, na sitaki wala sikushauri uamini hilo, but hebu cheza na tabia zako kwanza, jiangalie kama uko fresh katika angle zoote, naamini kuna mapungufu, na wote wawili hamtaki kushuka, kama yapo basi wewe jishushe, then uone kama hali itaendelea, ningekushauri mengi, but let us wait for other opinions,
  gud day.

  ReplyDelete
 5. pole sana, yawezekana Mumeo anongozwa na pepo baada ya kuopoa bibi mwengie, hawa wanaume bwn huwa hawajui, wakishapata nyumba ndogo wanalishwa vya kulishwa.maana bi mdg anataka apalilie kwake, siamini kama ni uchovu,umesema hapo nyuma mpk beach alikuwa anawapeleka sasa ki ubinaadamu lazima ingefika maali awaonee huruma watoto na mkewe, huyo hana ufahamu kesha lishwa,mtoe huko kwa maombi, kazana sana kumwombea aliyolisha yote yatoke

  ReplyDelete