Monday, August 30, 2010

INAHUSU, WEWE UNASAFIRI UNAMWACHA MUMEO NA HOUSEGIRL PEKE YAKE?? SOMA HIYO, NAIMANI UTAJIFUNZA KITU!

(nimerudi rasimi wapendwa wangu, nimejaa tele,  namshukuru Mungu nimerudi salama, na niko mzigoni kama kawa,  mikasa ni mingi kimtindo, but tutakwenda nayo taratiibu hadi tutaimaliza, niliwamiss sana,)

tuanze na mkasa wa huyu dada, maana umenigusa sana, coz mimi mwenyewe ni mama, na pia ndani ya story hii naimani unaweza pata kitu cha kukusaidia, 
soma hiyoMimi nina miaka kumi saba, nilikuja Dar kufanya kazi za ndani, nilifanya kwa mama mmoja polisi, na mumewe siijui kazi yake, ni watu wazima, hawakuwa na mtoto watotot wao wapo kenya wanasoma, isipokuwa walikuwa wakichelewa kurudi sana hasa mama, na mimi nikawa nawapikia na kufanya usafi, maana wao walikuwa busy,

Niliishi kwa miezi sita, nilipofika pale kwanza baba akaanza kunitaka kimapenzi, nilimueleza rafiki yake na mama, Yule rafiki yake akaenda kumwambia mama, nilipigwa sana siku hiyo, akaniambia mumewe hawezi kunitamani mimi ni mchafu sana na wala silingani nae ila nataka kumdharirisha tu mumewe,

Nikasema basi sitasema lolote, hali iliendelea vilevile, na Yule baba hakukoma kunifatilia, kuna kipindi Yule mama alisafiri alienda course, kusema ukweli Yule baba aliendelea kunifatilia sana, ilifika siku nikashawishika, nikamkubali, maana aliniahidi vitu vingi sana, baada ya kuishi hivyo kwa muda wa miezi mitatu, Yule mama alirudi, na rafiki yake  ambae ni jirani yetu akamwambia kuwa mimi natembea na mumewe, alinipiga sana na kunifukuza usiku,

Nilirudi Singida nikiwa teyari mjamzito, baada ya mama kugundua alifunga safari tukaja hadi kwa huyu baba, alituzuia na kusema nikutane nae mahali, alitufata, mama akamwamueleza hali halisi, Yule baba akatupa masharti, akasema kama nikienda kwake mkewe akijua tu! Basi hatanihudumia chochote, ila nikitulia, basi atanihudumia kwa siri,

Tukakubari kurudi Singida akanipa na laki moja ya kutumia akaninunulia na simu ili tuwe tunawasiliana ila alinipa masharit ya muda wa kumpigia, nikipata shida alikuwa ananisaidia sana hadi nilipojifungua ndio huduma zikasitishwa, tukimtafuta kwenye simu hatumpati, tukaja dar tena na mtoto akiwa na mwaka mmoja na miezi mitatu, tukaenda hadi kwake, tukaambiwa alishahama,

Nipo nyumbani hadi sasa, sina mbele wala nyuma na hata sijui nitampata wapi, maana wanasema alihamia Zanzibar na mkewe, sasa hata nikienda nitaanzia wapi na sijawahi kufika huko?

Kwa kifupi maisha yangu ni ya shida sana, mama amekuwa kipofu aliumwa macho hadi yakapofuka, haoni, baba alikwisha kufa, nimebakia mimi, ndio kila kitu. Mama ananitegemea mimi, na wadogo zangu wananiangalia mimi. namtaka huyu baba ili amsaidie mtoto maana anahali ngumu, siku zingine analala njaa, siku nikipata ndio anakula(( violet, huyu dada nimeona nitumie blog yako kumsadia, naomba kama inawezekana nikupe picha ya huyo baba, ili uirushe, ajione, aje amuone mtoto wake, anateseka sana, hata asipomchukuwa alete tu matunzo, please violet))

4 comments:

 1. nampa pole sana huyo dada,
  pia wanawake tujifunze kushughurika wenyewe, kwanini kila kitu haousegil, tena sikuhizi imekuwa kama vile fassion, mtu hana ulazima wa kuwa na housegil lakini ataforce hadi awe nae, sijui watu tukoje, ona sasa tunavyotesa viumbe wasio na hatia

  ReplyDelete
 2. pole sana mdogo wangu.
  ila kuhusu kuweka picha ya huyo baba kwenye blog sijui kama itasaidia, vinginevyo yawezamletea matatizo huyo mmiliki wa blog. la muhimu ni kumuwezesha tuu huyo dada na biashara ndogo ndogo ili aweze kujikwimu na mahitaji yake na awe mpole tuu kwani damu ni nzito kuliko maji ipo siku atajitokeza kumtafuta mwanae. So huyo bibie achakarike kwa hali na mali kukitunza hicho kiumbe kisicho na hatia. Inasikitisha sana wapendwa na haswa ukiiangalia hiyo picha na mtoto.

  ReplyDelete
 3. nampa pole sana huyo dada maskini, lakini violet wanaume cku hizi hawabebeki hata umpende vp? sasa mtu umepata nafasi ya kusoma usiende kisa kuogopa mumeo atatembea na housegal? aah nikuomba Mungu tu aingilie kati, kwani hali inatisha, maskini watu wasio na hatia wanateseka. S.K

  ReplyDelete
 4. ni kweli kabisa unavyosema S.K kwamba huwezi kuacha kusoma kisa kumlinda mumeo, but biblia inasema mwanamke atamlinda mumewe, wewe ukiamua kwenda kusoma, nenda, but usimwachie mtego mumeo kwa kumuacha na bint wakazi, isitoshe hamna hata mtoto, ningekuwa mimi namchukua bint, nampeleka kwa ndugu yany yeyote akae huko, huyo baba kama ni upuuzi wake akafanye huko na sio ndani kwangu, then nikirudi ndio namchukuwa,
  LAPILI AMBALO NAFIKIRI NI ZURI ni kwamba unapoletewa kesi na msichana wa kazi kuhusu mumeo, usikurupuke kuanzakumtukana msichana wako, unakosea, ila fanya uchunguzi taratiibu, tena ikiwezekana huyo mumeo wala humstui, itasaidia kuugundua ukweli, inaumiza sana mume akitembea na housegirl, yani najaribu kujiweka kama ndio mimi da!!! Mungu saidia.

  Alozungumzia kuweka picha hapa, nikweli haitasaidia,chamsingi dada jibidishe, utaweza tu, kuna usemi ule usemao SINA PUPA NA MAISHA KWAKUWA NAJISHUGHURISHA NAAMINI MUNGU ATANIPA KAMA SIO LEO BASI NI KESHO. Vumilia tu! mdogo wangu, one day will come dad atatoa huduma kwa mwanawe

  ReplyDelete