Wednesday, September 29, 2010

MUME WANGU AMENIACHA, NA SASA ANATAKA KUMUOA BEST FRIEND WANGU TENA KWA NDOA YA KANISANI- NIFANYAJE?

Mashost wamechachamaa jamani na waume za watu, kuweni makini nao, haya mambo ya shemeji yako huyu!, chukuwa namba yake hii!  sijui leo tunatoka twende utupe company, mh! shauri yenu,
soma hii ya huyu dada! imenigusa sana
(ni ndefu mno, but nimejitahidi kuedit na kubakisha points tu!)
Habari yako dada,


Nimepewa jina la blog hii na Arafa, anasema mlisoma nae, nahitaji sana msaada wako dada yangu, mimi nilikuwa na kijana mmoja tuliependana kupita maelezo tulikutana chuo cha ufundi, mimi nilikuwa nasoma kozi ingine na yeye ingine, baada ya kumaliza akaamua kunichukuwa na kuishi na mimi, tumeishi nae kwa muda wa miaka mitatu kama mke na mume japo mwenzangu umri wake umeenda kidogo,  tumefanikiwa kujenga nyumba mbili, baa mbili, yani hatukuwa na maisha ya shida, na nimezaanae mtoto mmoja,

Niliwahi mtambulisha rafiki yangu kwa mume wangu, hadi sasa naandika ujumbe huu ni miezi mitano nimetengana na mume wangu, alinifukuza kwake, nikamuuliza kosa langu ni nini? Akasema eti dini hazifanani yeye mkristo na mimi muislam, nikamuuliza sababu ni hiyo tu?? Hukuliona hili tokea mwanzo hadi kunichukuwa na kunizalisha? badae Nikakubali mimi kubadili dini ili niendelee kuwa nae, sikufichi violet huyu ndie mwanaume wangu wa kwanza tangu nizaliwe, wazazi walinikatalia kubadili dini, lakini mimi kama mimi nilikuwa teyari, nilijihisi kumkosa huyu ni kama kupoteza uhai wangu,

Sasa nimeshangaa kusikia baada ya yeye kuniacha, wazazi wangu waliniita kijijini kwetu, nikakaa huko miezi miitatu, siku moja akanitumia sms kuwa nimlete mwanae,(anamtaka) nikaona afadhali, ndio njia ya mimi kurudi kwake, nilikubali na kuja  tena dar, wazazi waliniambia nisifikie kwakwe niende kwa ant yangu ,  alinifata huko na kusema anamtaka mwanae ampleke mwanae machame (akalelewe na wazazi wake) pia bila aibu wala uoga, akatuambia anataka kuoa.,  hata ant yangu hakuwa akijua hili,

kumuuliza sana akasema anamuoa best friend wangu, na harusi ni mwezi wa kumi kati kati, vikao vimeshaanza. Mwenzenu natamani nijiuwe kabisa, najiona nina mkosi sana, kwanini rafiki yangu anifanyie hivyo? Kwanini itokee kwangu? Kwanini mimi tu? Amechachamaa anamtaka mwanae, sasa mimi nitabaki na nini? Kuna siku nilishika vidonge nimeze nife tu! But nikamuangalia baby wangu alikuwa amelala, nilimuhurumia sana nikaacha, but mawazo ya kujiua bado yananiandama sana jamani nisaidieni, naweza kuivuruga ndoa yao? Lakini kwa haki ipi niliyo nayo? Msaada wenu tafadhali siwezi kula wala kufanya chochote,

nina hali ngumu sana kichwani kwangu

13 comments:

 1. mimi kusema kweli nawashangaa sana wanawake wanaoweka maisha yao yoooote kwa wanaume zao? ha! kwani mwanaume ni nini? yani i swear and ill continue to swear, sitaruhusus hata siku moja mwanaume aitese nafsi yangu, achana nae, wewe kaa na wanao,kama mwanao ni mdogo una haki hata ya kumshtaki ili akuachie mwanao usimwachie mshenzi wa tabia huyo.
  usijiuwe wewe, shauri yako

  ReplyDelete
 2. Unauwezo wa kuisimamisha, kisheria ukiishi na mwanaume miezi sita anahesabika kama mume halali, tafuta kanisa wanalofungia ndoa ukamuone mchungaji/padre ili upate haki yako ya mali. Mume kama hakutaki achana nae, inauma tena sana sana lakini huwezi lazimisha mapenzi atakutesa even more. Mtot usimpe ndo faraja yako. Muache aende zake, Mungu atakupa mwingine, usijiue huyo ni shetani anakushawishi, mkemee kabisa. Utakufa mweznio atashukuru amepata uhuru, kisa cha kumfurahisha ni nini! wazazi wako na mwanao huwaonei huruma!? Let him go, he is a monster... shiiiiiiit!

  Fundisho kwa nyie mnaojifanya mnawapenda sana mashosti kila siku karibu home, mara tutoke na Mr. mkomeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

  ReplyDelete
 3. usiwe mjinga wewe mtoto, yani ujiuwe sababu gani mwanaume kwani ulizaliwa nae

  ReplyDelete
 4. njoo mimi nitakuoa mwaya, mie mwenyewe muislamu mwenzio, achana nae huyo hakupendi ila alikutamani tu!

  ReplyDelete
 5. Pole mpendwa najua inauma tena inauma sana, lakini jipe moyo muombe mungu wako akutie nguvu na ujasiri ili usimame imara ondoa hayo mawazo ya kujiua kwenye akili yako na usifikirie kujiua hata siku moja kwa ajili ya mwanaume. aliyekwambia maisha bila yeye hayataenda ni nani kwani ulikua ukijua kwamba yeye ndiye atakuwa mume wako basi tulia muombe mungu mume wako alikua bado hajaandaliwa na mwenyezi mungu. hayo ni moja ya mapito, achana nae muombe mungu utapata mume mwema na mwenye mapenzi ya dhati na machungu yote utayasahau.usiache kula kwa ajili ya huyo mshenzi kula vizuri upate afya utakavyo acha kula na kujiweka na mawazo ndio utazidi kumpa kichwa na utachakaa nayeye atazidi kukuona huna samani unatakiwa upendeze zaidi ya ulivyokua ili ajutie kukuacha. kuhusu mtoto usimpe huyo ndio faraja yako na mwambie wewe unahaki ya kumlea mwanao mpaka atimize miaka 18. sheria ipo kama hataki nenda mahakamani.FUTA MACHOZI,SIMAMA IMARA, JIPE MOYO UTASHINDA. Eva from Tata

  ReplyDelete
 6. jamani wapendwa mbona wakali?! mdogo wangu pole sana nakuomba usijiue mwangalie Mungu tu atakufanyia njia, pia ukumbuke utamuacha mtoto wako mdogo halafu utampa mwanya huyo baba mtoto wako wa kuoa, nakushauri fuata sheria. kweli mashoshisto mmmmhhh!!!!

  ReplyDelete
 7. JIUWE MWAYA ''UFE''

  ReplyDelete
 8. WANAUME WA SIKU HIZI WAMEOTA MIGUU VICHWANI, SIJUI TUWAROGE WAWE WEHU, YANI MIE HATA SIJUI NIFANYAJE, MIMI NILIVISHWA NA PETE, LAKINI NIKASHANGAA KUMBE ALIVISHA PETE KWINGINE TENA, NA KULE NDIKO ALIKOOA, SIKUOGOOPA WALA KUTETEREKA WALA NINI, SASA HVI NINA MCHUMBA NA NIKO STANDBY KAMA NAE ATANITEMA HAYA, AKIOA HAYA, YANI WALA HATA SISHITUKI, WANUME ARE LIKE WANYAMAA HAWANA UBINADAMU HATA KIDOGO

  ReplyDelete
 9. Msikimbilie kuvaa pete jamani, Pete uvae mkianza vikao, mi nilivaa pete na mahari juu na hakukua na ndoa, lakini namshukuru Mungu nimepata mume mwema hasa, nashangaa nilikua nasubiri nini kwa huyo kibwengo. Mume anapatikana kwa maombi tu, hili nawashuhudia kwa kuwa limenipata mwenyewe.
  Ombeni mlilieni Mungu, ndoa utaipata kirahisi wala hutakua na haja ya kujibembeleza kwa mtu, atakutreat kama malkia

  ReplyDelete
 10. pole best, lakini katika vitu ambavyo huwa siviwazii na sitavipa nafasi katika maisha yangu ni kuwaza kujiua,yani hata iweje siwazi hivyo, kifupi huyo mzazi mwenzio wa la hajaumbwa kwa ajili yako, na mambo mengine ni yakumshukuru mungu tu! coz tumeambiwa tushukuru kwa kila jambo, you never know pengine mungu amekuandalia mume mzuri atakaekupenda kwa dhati, wewe huyo wanini bwana, ah! achana nae, tena nikwambie mwanaume akigundua unamzimikia atakupelekesha wewe kama mlevi, atakupa maisha ya shida sana, bora kumuignore tu! cha msingi jali maisha ya baby wako tu! ona kama vile unaweza ishi bila yeye, kwani wewe ulizaliwa nae huyo?? ah! natamani nikuone nikuona tuongee vizuri. ah! usijiuwe bwana,

  ReplyDelete
 11. pole sana mdogo wangu. hayo ni mapito tu hapa duniani na wanaume ndivyo walivyo na hata huyo anayetaka kufunga naye ndoa naye itafika siku atamuona hafai atahangaika na wengine. La muhimu, jitahidi kumtoa katika kichwa chako japo itachukua muda. Mtoto usimpe kwani bado yuko chini ya himaya yako utakachokula wewe mpe na mwanao atakuwa tuu huyo. Nenda mahakamani kadai haki yako mliyochuma pamoja na nina imani sheria itachukua mkondo. Mbona yalishatutokea hayo yako cha mtoto? kaza buti tafuta pesa na zidisha maombi Mungu yupo kwa ajili yetu mpz. POLE SANA MPZ.

  ReplyDelete
 12. mapenzi ni ya pande mbili, kama upande mmoja haukupendi basi usilazimishe, kwani hata kama utaweza kutumia sheria kuzuia hio ndoa yao bado sheria haiweze kukupa upendo. mimi nashauri sheria itumike ili uweze kupata haki zako na muachane kwa amani, nasema muachane kwa amani kwani huyo ni mzazi mwenzio, huyo mtoto wenu hatakua na mzazi mwingine(biological parents) zaidi yenu, na kwabahati mbaya hatujui kilichomsibu huyo baba, kwani kwenye maswala ya mapenzi nguvu za giza pia hutumika, kama wewe ni mchunguzi utagundua siku hizi wadada wengi wamejiingiza kwenye ushirikina kwa ajili ya kujipatia wakaka/wababa wenye maisha mazuri, na mwisho narudi kwako wewe mwenyewe, hawa mnaowaita mashosti au shoga si wote wenye nia nzuri na wewe, nakushauri uwe na mipaka katika mambo yako. si kila kitu cha kumwambia shosti/shoga

  ReplyDelete
 13. SIMAMA MAMA IMARA MAMA MWOMBE MUNGU UMSAHAU KABISA, HIVYO NI VISA VYA MAPENZI HAMNA MTU AMBAYE HAJAVIPITIA CHINI YA JUA, KILA MTU ANA KISA CHAKE JUU YA MAPENZI. WAZAZI WAKO WAMEKULEA MPAKA UMEKUWA IWE KWA SHIDA AU KWA RAHA UJE UFE KWA AJILI YA MWANAUME!!! HEBU WAONEE HURUMA WAZAZI WAKO,MTOTO WAKO N.K HAO WANAKUHITAJI SANA KULIKO HUYO MWANAUME MWACHE AOE WEWE UNAFIKIRI KAMA KAKUACHA WEWE NA KAMPENDA HUYO RAFIKI YAKO UNA FIKIRI ANA MAANA HUYO? NAE ATAMWACHA TU SO WEWE NI MREMBO SANA TENA SANA JAPO SIJAKUONA, SIMAMA SONGA MBELE YUPO MUME MWEMA KWA AJILI YAKO. MIMI MWENYEWE YALINIKUTA HAYO NIKAZAA HALAFU NIKAACHWA, HIVI SASA NINAVYOKUANDIKIA UJUMBE HUU NIMEOLEWA NA MUME MZURI TENA MSOMI KABISA NA NDOA KANISANI UPO HAPO. SO STOP KILLING YOUR SELF, MUNGU NI MWEMA.USIJIUE MUNGU HAPENDI.

  ReplyDelete