Friday, April 23, 2010

NAMNA YA KUWEKA NYUMBA KATIKA HALI YA USAFI







Mara nyingi tumekuwa tunajitahidi kufanya usafi kwenye nyumba zetu. Ila kuna mambo kadhaa huwa tunayafanya kwa uvivu sana ama ni mara chache sana wakati tunasafisha nyumba zetu. Hata maelekezo ya usafi kwa mahousegal/boy huwa hayalengi sana hivi vifatavyo.

1 Hakikisha unatoa nje kapeti la sebuleni unalipiga piga kuondoa vumbi na pia kusafsisha pale sakafuni kwa kuwa pia vumbi hupenye na kutuama chini. Hii ni kwa yale makapeti ya kisasa. Kutofanya hivi kumesababisha kuwa na tatizo la kudumu la kuugua mafua nyumbani bila kujua chanzo na kuona ni kama kawaida tu pale nyumbani.

2 Hakikisha unabadiri mapazia kadiri unavyoweza au kufua mara kwa mara  ili kuondoa mavumbi yanayonasa kutoka nje yarushwayo na upepo. Hii hufanya nyumba kuwa na hewa safi sana. hata kufurahi kukaa chumbani ama sebuleni hata kama ni joto. Si wajua Dar bila joto haijakuwa Dar. hahahahaha

3 Pia kumbuka sana kufuta vumbi lililopo kwenye zile nyavu za kuzuia mbu kwenye dirisha. Tena zile huzuia sana kuingia mbu ndani na hata vumbi, kwahiyo huwa na uchafu mwingi sana unaopunguza hewa safi ndani. Hewa huwa nzito sana na hata kuongeza maumivu ya kichwa. Hapa naweza sema Carbon inatengenezeka. hahaha Bios hiyo.

4 Jambo lingine ni kuhusu viatu, huwa tunavipenda sana viatu vyetu lakini hutchafulia mazingira ya ndani na kuleta taka ndani, bila kusahu harufu mbaya(Vinatema) Inashauriwa viatu viwekwe mahali karibu na mlango wa kutokea au kuingilia. Hii huzuia uchafu kuingia ndani na hata hewa ila mbaya isisumbue ndani na kusababisha makazi kuwa mazito.

5 Hii ni ya mwisho lakini sasa ngumu kiasi hasa kwenye mifumo dume. Kama kaka au baba wa nyumba ni mvuta sigara, aahakikishe ana vuta sigara zake nje kama Mita 15 kutoka eneo la nyumba. Mara nyingi moshi wa sigara hasa utokao mdomoni ndio unamatatizo sana hasa kwa watoto. Yapaswa kushauri wavutaji pale nyumbani watoke nje kwa umbali fulani kisha wamalize hamu zao kisha warudi ndani.


Chanzo cha habari hii ni  lifestyle.msn.com Decor and Organizing.








2 comments:

  1. Asante violet,
    Gide

    ReplyDelete
  2. ubarikiwe kutukumbusha maana waume zetu wanasema to much usafi

    ReplyDelete