Tuesday, April 20, 2010

RAFIKI ZANGU WANACHUKULIANA WAUME BILA WAO KUJUA, NIKISEMA NITAKUWA MMBEA?


Kuna kitu kinanichanganya sana, hakinihusu mimi lakini kinawahusu watu muhimu sana kwangu, nina marafiki wawili, na ni wamama wenye familia zao na nimajirani zangu,  ss mmoja kati yako anatembea na mume wa mwenzie wakati wote wawili ni mashoga zangu, ila huyo anaeibiwa hajui kama huyu rafiki yangu mwingine anamchukuwa mumewe, na huwa anamchekea kabisa na kujifanya rafiki yake, wanaongea vizuri sana,

Nilishawahi kumuonya huyu rafiki yangu, kwanza ukizingatia sisi ni majirani, pili huyu akisha kuja kujuwa itaniweka mimi pabaya sana, naona bora hata asingeniweka wazi juu yahili maana linaniumiza sana, kwakuwa huyo mwanaume ameshanogewa na penzi la nje, ameshaanza kujisahau, anamtesa sana mkewe , anampiga sana, anatishia kumfukuza, kitu kidogo tu kwake linakuwa kubwa, huyo dada huwa akipigwa na kufukuzwa anakuja kwangu, akifika kwangu anajieleza sana, na kusema nahisi mume wangu ana mwanamke mwingine,

maana mwanzo hakuwa hivi, anachowaza ni sahihi na mimi nalijuwa hilo, kinachoniuma zaidi sikumoja alipigwa sana mumewe usiku, akakimbilia kwangu, akamkuta na huyu mwizi yuko kwangu, akaanza kutueleza, nilimuhurumia sana, nikamwambia vumilia tu! lakini huy mwenzangu ambae ndie muhusika wa tukio, akawa anamshauri aondoke, aliniudhi sana na huwa namsema sana, lakini hasikii, najuta kwanini nimelijuwa hili, bora ingekuwa siri yao tu!
sasa  kumwambia kuwa chanzo ni fulani,  nashindwa maana wote ni mashoga zangu, Sasa hebu nishaurini, nimwambie tu liwalo na liwe, au nitaitwa mmbea niwaache tu mwenzie huku pembeni anajifanya anampenda, inaninyima raha sana hii.

19 comments:

 1. ukisikia umbea ndio huo
  wewe inakuhusu nini? waache watajijuwa wenyewe

  ReplyDelete
 2. pole dada ila mimi ushauri wangu ni kua mwambie huyo mwizi aachane na mume wa mtu je ingekua ni yeye angefanya nini?mtishie kua utakwenda kumwambia huyo anaeibiwa mume na akiwa hasikii kamwambie ukweli huyo anaeibiwa anapata shida huyo dada tujifikirie je ingekua ni wewe ingekuaje??

  ReplyDelete
 3. wanawake mna roho mbaya sana, huwa mnakataa tu bure, haya jiteteeni na hapa

  ReplyDelete
 4. shost hapo parefu, wala sio masikhara
  mimi nakushaui, mwambie huyo rafiki yako mwizi, kwamba utamchongea, ili akome, jamani, kwanini mtu hawezi kutulia? mbona anamtesa mwenzie? lo!

  ReplyDelete
 5. Mtishie mwambie naomba uwache kama uwachi nitamwambia. akiacha kaa kimya limepita sipoacha mwambie, na anavyomwambia aondoke wakati mwenzie ana familia ili akae yeye. sio vizuri jamani ktembea na waume wa watu eeeeeeeeee.

  ReplyDelete
 6. daah, i think bora usimwmbie directly, jribu kil njia kumuonyesha mwizi wake amjue, kwanza huyo unemuuit rfiki sion rafiki yenu, rafiki gani anaweza kuchukua mume wako na anon unateswa na bada hata hauni huruma, huo sio urafiki, ni mbinafsi na hastahili upendo wa urafiki, so better expose her indirectly,muonyeshe huyo rafiki yako anaeibiwa njia zote z kuonyesha huyo rafiki yenu mwingine ndo anamuibia mumewe, au tafuta mtu wa busara amsaidie kumueleza ukweli wa mambo. na kumbuka leo kwake kesho kwako. kaeni mbali ne huyo mwizi.

  ReplyDelete
 7. mmh! huyo anayesema umbea hapo juu hayajakufika au ndio tabia yako na wewe, hivi siyo vizuri kabisa tena rafiki yako kweli kikulacho ki nguoni mwako ni ngekuwa mimi wewe ningemuonya huyo mwizi asiposikia, ningefanya kadinner party nawaalika wote na waume zao sasa hapo ndio ningetoa duku duku langu na hata kama urafiki ufe sitojali,lkn siwezi kumuona mwanamke mwenzangu anateseka tena anayemtesa tunacheka nae, loooooooooooooo! wasichana, wanake mbona tunakuwa na roho za kikatili namna hii? mtu unamume wako bado tu au kama hauna basi katafute wako hii inatia kinyaaa kabisa, tena ukute huyo mwizi kajipeleka, na sisi wanawake hata kama ndio ushoga tukome kusimulia mambo yetu ya ndoa kwa marafiki ndio unamfanya mwenzio amtamani mumeo, wewe dada kweli mwambie mwenzio asije akavunja ndoa yake kisa huyo hata sijui nimuitaje, mwambie tu, lah! yani nasikia hasira utadhani yamenifika mimi.

  ReplyDelete
 8. huo ni umbea dada, hao wanaosema umwambie, utaanzaje? wangekuwa wao wangemwambia, mimi niligundua kabisa baba yangu anatembea na rafiki yake mama kipenzi, lakini wala sikusema, za mwizi 40, mama aliwanasa yeye mwenyewe live, sasa wewe unaweza kujitia kimbelembele kumsemea mwenzio, you never know, wenzio wanaweza kukugeuka na wakawa marafiki wakubwa, ukapoteza hata amani, yatakushuka shu!!!!!!!!!!!! haikuhusu hiyo, mradi hachukuliwei mumeo, achana nao dada wewe endelea na shugur yako, cha msingi mshauri huyo dada asiondoke kwake avumilie tu
  lo!

  ReplyDelete
 9. pole shost kwa kweli upo katika hatari kubwa sana, ukisema umwambie mwenye mume unaweza kuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya watu, wewe cha kufanya kata mawasiliano na huyo mwizi tena ikibidi umpige marufuku kuja hapo kwako maana mwenye mume akijua atajua mko njama moja na mnamsanifu, na usitake nae mazoea tena, muachie mwenye mume ajue kwa njia nyingine ili wewe uwe safe side......ni mtihani mkubwa sana huo

  ReplyDelete
 10. Kwa kweli wewe pia una tabia mbaya sana kwa nini unaendekeza tabia mbaya kama hiyo kwa nini usiwakutanishe na kuwambia tabia zao mbaya au na wewe unachukuwa mume wa mtu.

  Mfano ndo wewe unafanyiwa hivyo ungejisikiaje kama huyo mwizi hakuelewi achana naye na vunja uhusiano naye.

  ReplyDelete
 11. Ukweli ni kwamba mwizi ni mwizi tu kama mpango wa kumuiba mume wa shoga wako ukifeli hujue atakuibia wewe wizi ni tabia kama anayo lazima atakudhuru wewe sasa nakushauri ndugu huyo mkatae vunja ushoga nae atakuumiza na wewe

  ReplyDelete
 12. Mpendwa, kwani una deni kubwa na huyo 'mwizi' kiasi kwamba huwezi kuachana naye? unless hiyo tabia haikukeri. Cha msingi achana naye tena mpige marufuku kuja kwako na sababu ya kufanya hivyo uiweke wazi kabisa. Kwa sababu mateso ya ndoa sio madogo, sasa sembuse hayo ambayo chanzo chake kinajulikana, na yanafanyika kwa mtu wako wa karibu, hebu act now bwana umpe ahueni rafiki yako!

  ReplyDelete
 13. hapo sasa, na huyu dada anaeteseka sasa hivi mara ghafla akija kujua na anakumbuka alikuwa anaenda kwa huyo vk kumlalamikia na vk anajua kinachoendelea sema ni kumpooza"vumilia"...vumilia wakati unajua kinachomla/mmaliza?...bwana wanawake tuna mambo magumu mno....sasa akijua ndio utaanza kumwambia ooh rafiki yangu cjui pole cjui sorry nilishindwa kukuelezea coz kimepanda kimeshuka....ctakuelewa mana ni full" unafiki" na nitahic nawe ulikuwa unafurahia mateso yangu, haki ya nani wacheni tu, unacheka nao na wabaya ni hao hao.

  ReplyDelete
 14. yaani wanawake jamani tuna kuwaga na vijimamabo vya ajabu sana, sasa wewe umeolewa unamharibia mwenzio nyumba yake na zaidi unamshauri aondoke cjui kitu gani,sasa akiondoka na yeye ataacha ndoa yake aingie kwenye hiyo aliyoiharibu? hapo ndio ninapochoka unafiki wa "kike"...napendaga sana kuwashauri wanawake wenzangu kwenye ndoa zao wakipata purukushani waangalie ni nani na nani wa kumweleza, yaani ni kutafutiana uhasama tu huku, mie cjui hata nielezeje mana ingekuwa ni me cku nikijua lawama ni kwenu wote wa3...mume wangu, huyo mwizi wangu na wewe vkeisy mana wote mnani enjoy....sasa ni bora wewe vk ujitenge na huyo mharibifu mapema.

  ReplyDelete
 15. ukweli n kwamba mungu amekuteua ww uwe mtetezi wa huyo anayeibiwa , lakini kwa kutolitambua hilo unajikuta unakuwa mtetezi wa mwizi,maana yake na wewe ni mwizi kwa nini mwenzio anaibiwa halafu unatulia tu kwa kwel ww ni mnafiki,usituchezee akili, mimi nina shaka pengine hata wewe umetembea na huyo bwana ndio sababu hutaki kumtaja huyo mwenzio kwa kuwa na yeye atakutaja .LA KAMA NI MKWELI NA UNAMUOGOPA MUNGU WEKA MAMBO HADHARANI SEMA UKWELI UNAOUJUA VINGINEVYO DHAMBI YA HUYO MWIZI NAWE ITAKUTAFUNA HAKUNA WA KUWATETEA WANAWAKE KAMA WENYEWE HAMKUA WAWAZI NA KUONEANA HURUMA MIMI NAITWA BOAZY UKINICHUKIA POA AKIMWAGA UGALI WE MWAGA MBOGA NA JIKO TIA MAJI

  ReplyDelete
 16. dada yangu, hunijuwi wala mimi sikujuwi, watu wanakurupuka tu! kukwambia umwambie live, utafikir wao wangeweza,
  mimi ilishanitokea, nilijitia mmbea nikasema, we! nilikiona kilichomtoa nyoka pangoni na kukimbilia porini, nilipakwa mie, nilionekana mmbaya kuliko wote, na mapenzi yao yakanoga, yaniteremka shuuuuuuuuuuuuuu
  cha msingi wewe mstopishe huyo mwizi asikushirikishe chochote

  ReplyDelete
 17. nyie mnaosema asimwambie hayajawakuta, mimi kama mimi acha niitwe mbea, kwanza umbea maana yake nini? maaana huyo dada yeye hakutoka kwenda kumchunguza huyo mwizi labda mimi sijui vizuri maana ya umbea, kweli kumuona mwanamke mwenzangu anateseka tena best na anayemtesa nae ndio shost wetu looo! utaoneka mbaya kama ukimwita huyo mwenye mume ukaongea nae peke yake, wewe waite wote ongea nao waambie nyie watu wazima, magonjwa haya watu hata hatusikii jamani, kama unaona ugumu basi fanya kama walivyosema wengine mwambie huyo mwizi akukome huo wizi wake asikuhusishe, mimi ningesema mi sioni kigumu hapo na kama urafiki na uishe tu.

  ReplyDelete
 18. tafuta line mpya mwandikie message huyo rafiki yako ukweli wote kwamba mume wako anaibiwa na fulani, au kama kuna siku unajua watakutana na shosti wako, muandikie message ili aende awafumanie, tumia line mpya kable mwisho wa kusajili line haujaishi mwezi wa sita, atawafumania na mwenyewe atajua cha kufanya.

  ReplyDelete
 19. Duh. Hii kali. wewe dada uliyefahamu kuwa babako ana tembea na mwanamke nje ukashindwa kumweleza mamako una walakini. Malipo ni hapa hapa duniani. Itakutoa the same thing na bintiyo atakuchunia. story ya huyu dada ni sawa na kujua kuwa best yako anakaribia kuanza uhusiano wa kingono na muathirika unanyamaza eti ajue mwenyewe. Si utakuwa muuaji na wewe? Nadhani huyu shost mwenye siri atafute namna ya kumfikishia habari mume wa mwanamke mwizi (asimwambie mwenyewe ila atumie hata marafiki wa huyo baba. Achunguze amfume mkewe mwenyewe na ndo patakuwa patamu

  ReplyDelete