Thursday, April 8, 2010

MUME WANGU ANATABIA YAKUTEMBEA NA MAHOUSEGIRL WANGU- JE NIWE NAWAWEKA WAZI JUU YA TABIA YAKE KABLA??

Anayo tabia hiyo, mimi binafsi imeniumieza sana na kunifanya naiona hali ya kawaida tu,

Maana kila anaekuja anaondoka kwa sababu hizo hizo, mwanzoni sikuwa nilikuwa naumisa sana, nikawa naondoka moja kwa moja kwetu, ananifata narudi, kwa ajili ya watoto wangu tu!,

Kuna kipindi alimpa mimba housegirl wangu huyo alikuwa ni watano, nililia sana, maana kuna jirani yangu yeye ni nesi, ndio alieniambia kwamba nimchunguze, mimi kutwa nipo kazini, narudi usiku na watoto wanakuwa wamelala

Yeye huwa anawahi kurudi, basi kumbe ule mchezo wanaufanya kipindi ambacho sipo, basi nilipoanza kumchunguza kweli nikaona maziwa yanamjaa na anapendeza sana, ila kazi anafanya kama kawaida, sema alikuwa ananidharau kupita kiasi, mimi sina tabia ya kuongea ongea, ni mvivu sana kusema sema, lakini ilifika kipindi msichana ndio akawa kama mama,

Siku ya siku ilifika nikambananisha sana, nikiwa na Yule nesi jirani yangu, akampima, akakutwa na mimba, tukaanza kumuuliza ni yanani, alikataa kusema, baada ya kuamua kumfukuza ndio akasema ‘’ ntaenda wapi wakati muhusika ni baba’’ nilitaka kurukwa na akili kabisa

Mume wangu nilipomuuliza mara ya kwanza alikataa, nililia sana, nilipombana sana ndio akakubali na kuniomba msamaha,

Kusema kweli niliamua kurudi kwetu rasmi, nikamuelezea mama hali halisi, mama akaniambia nipumzike nyumbani kwanza, maana matatizo yalikuwa yamefuruliza sana,

Lakini nilipigiwa simu na kuambiwa mwanangu amelazwa, anaumwa sana, maana nikitaka kuondoka na watoto ananikatalia, hivyo niliondoka peke yangu, kwa ajili ya mwanangu nilirudi nikafikia kwa Yule nesi, rafiki yangu, nikawa namuuguza mwanangu, sasa kuna siku alinifata usiku yeye na ndugu zake na kunitaka nirudi nyumbani tukayaongee, niliwaheshimu sana, name nilimpigia simu mama yangu, akaja, tukayaongea huku Yule msichana arudishwe kwao, sasa sielewi, kabla yule msichana hajaondoka, tukiwa katika maandalizi ya kumsafirisha, nahisi kuna mchezo ulifanyika, maana baada ya miezi mitatu, Yule binti mimba ilitoka, akuwa anaumwa, nahisi alikunyw vidonge ili itoke, au mume wangu alimshawishi aitoe, kusema kweli niliamua kumrudisha kwao, mume wangu alisemwa sana na ndugu zake, na akaomba msamaha kutorudia,

Nilipoletewa mwingine tena, akamtongoza, huyu wa sasa alikuwa mwaminifu, akaniambia mama, baba kasema nilale nae atakuwa ananipa mshahara mkubwa na kuwajengea nyumba wazazi wangu, nilimsema sana, nilimuuliza mimi tatizo langu ni nini hadi utake kunifanyia wasichana wangu? Kwanini unanidharirisha hivyo? Hakujibu, isipokuwa alimchukia sana Yule binti, na kuna kipindi nilisafiri kikazi nikakuta amemfukuza nyumbani kamleta mdogo wake,


Sasa nahitaji ushauri wenu, niwe nawaweka wazi wasichana ninaowapata juu ya tabia ya mume wangu? Au nitakuwa namdharirisha? Ila hali hii imenifanya nijishushe thamani sana, kwanini asifanye nje huko? Kuna wazuri wangapi hadi ang’ng’ane na wasichana wangu?

4 comments:

 1. mumeo atakuwa na mapepo sio bure,
  muombee tu

  ReplyDelete
 2. usiwe unawaambia, utakuwa unamdhalilisha mumeo, kaa na mumeo, muulize tatizo lake hasa nini hadi afanye uchafu huo? inauma sana, lazima atakubali kusema tatizo lake kama utamuuliza kwa upendo, pole dada yangu, waume wa siku hizi kama wamerogwa inakera sana, usimwache, ongea nae tu, pia uwe mkali kidogo juu ya mahousegilrwako, angalia mavazi yao wanayovaa, kama hayastahili kemea, pengine ndio yanafanya mumeo aningie vishawishini,
  imeniuma dada pole

  ReplyDelete
 3. Jamani wanaume wengine balaa, hadi wanatufanya watu tusiwe na house girl. Mie hapa nina kimimba inanipa tabu sana hadi nataka kuweka house girl. Kama mambo yenyewe ndio haya nimehairisha hata kuweka msichana.
  Mdada pole sana ila muhimu mkalishe mumeo na umuulizie tatizo lake haswa ni nini hadi anachukua HG?

  Vile vile na wewe jiangalie upande wako labda upo busy mno hadi unakosa muda wa kukaa na mume. Hebu angalia kazi unazowaruhusu hao wasichana kufanya, maana kama unawaruhusu hadi kufua chupi za mumeo na kutandika kitanda chenu kuwa makini.Ujue kuna baadhi ya kazi tunatakiwa kufanya sisi wamama na si kuwaachia wasichana. Jitahidi kumuweka msichana wa kazi asiwe close sana na mumeo.

  ReplyDelete
 4. hapo kuna mawili, yawezekana wewe mwenyewe ni sababu, kwa vipi?
  1. yawezekana wewe uko busy sana kiasi cha kushindwa kutimiza majukumu kama mama
  2. yawezekana kazi za housegirl wako zimevuka mipaka, anatandika chumbani, anampatia baba chakula hata kama wewe upo,
  3. anajali watoto kuliko wewe
  4. dada anaweka maji ya baba ya kuoga,
  5. kama alivyosema mdau hapo juu kwamba yawezekana wasichana wako wan uhuru mkubwa kuliko wewe, tazama mavazi yao, muda mwingine msichana anavaa suruali imembana sana yawezekana hata chupi ikawa inaonekana, au sehemu za kiuononi, halafu anakatisha katisha mbele ya mumeo, unategemea nini? wasichana wenyewe siku hizi macho mia mia, hawaeleweki kabisa, pole dada
  pia tu kumbuka kumuombea, atakuwa na pepo la uzinzi

  ReplyDelete