Friday, April 2, 2010

MUME WANGU NI MCHAFU SANA, ANANITIA HATA KINYAA- NISHAURINI NIFANYE NINI

Nimerudi jamani, mpanaaaaaaaaa, niliwamisi sana, thanks God nimemaliza mitihani yangu salama, nasubiri majibu tu! asante kwa mliokuwa mmenikumbuka, nami niliwakumbuka sana tu! sema mshika mawili moja au yote yaweza mponyoka, ikabidi niache kwanza huku ili nibase kwenye kitu kimoja, now im back to you dears, na nyie miliotuma sms hizi

1. umefulia wewe, huna jipya, story zako tumezichoka, unafikiri kuendesha blog ni kazi ndogo, huwezi
2. huwezi kuendesha blog wewe, unasingizia mitihani, waachie wenyewe, waTZ wote hamjui kuendesha blog, acheni  mnatukera ah!

NAPENDA kuwaambia hivi, nimewasamehe bure kwakuwa hamujui mlitendalo, pia huwa najua kuwa hakuna shamba litakalojaa mazao peke yake, lazima na magugu yawemo, basi watu wa style yenu wala haminipi shida, kuhusu blog za kitz kukukera, kwani umelazimishwa kusoma blog yangu, si usome hizo za nje? blog ziko kibao kwanini msisome hizo?? kuna wanaonufaika kupitia blog yangu, ushauri wa watu umewasaidia, wameweza kupata mwanga wa kutatua matatizo yao, ss kama wewe unaona haukufai, usiwe unaifungua blog yangu, waaachie wale wanaona inawafaa. OVER

(TURUDI KWENYE MKASA WETU WA LEO, NIMEIKUTA MINGI KIMTINDO, LAKINI TUANZE NA HUU KWANZA)]

Violet mambo vipi? mimi nina tatizo moja, na linaninipa shida sana, naomba ushauri wenu,
Nimeolewa, na mwanzoni tulikuwa tunaelewana sana na mume wangu, alikuwa na kazi, lakini baada ya muda akawa hana kazi tena, yeye ni mtu wa kukaa nyumbani tu! anasubiri mwisho wa mwezi nimgawie hela ili akalewee pombe,
shida inakuja hapa, akishalewa tu akirudi hata usiku wa manane anafikia chooni,(chumbani kwangu kuna choo) basi anachokijua yeye ni kuchamba tu! anakunya, mavi anaacha kama yalivyo, hadi ninapofanya usafi asubuhi, ndio nifrash, na hii ni tabia yake, ukimwambia anachofanya ni kosa, anafoka anasema yeye ni kichwa cha familia, hivyo tumsikilize yeye tu!,
shida ingine ni kwamba, yeye ni mtu wakurudi usiku tu, na akirudi ule usiku, anataka nimpe, sasa mimi huwa nasikia kinyaa sana, maana amelewa sana, mwili wote ananuka pombe, halafu anakuwa ananitaka, inanipa wakati mgumu sana, hii tabia ya uchafu wa chooni na hata kusex nae naona kinyaa, pia mume wangu si mtu wa kushaurika, hata umshauri vipi, hashauriki kabisa, sasa violet na wengine, naombeni mniambie nifanyaje mwenzenu, maana loh! inanikera sana mimi.

7 comments:

  1. usipoteze muda wako kuwajibu washenzi hao

    ReplyDelete
  2. kwanza dada Violeth pole na mtihani, jama watu muwe wavumilivu, siyo mnakurupuka tu nakuanza kuongea maneno machafu muacheni dada Violeth ajiendeleze na yeye huo wote ni wivu tu kama nyie yamewashinda kaeni kimya na mtabaki hivyo hivyo na midomo yenu michafu mshindwe na mlegee kabisa kukatisha watu tamaa.

    ReplyDelete
  3. jamani pole sana dada hapo kwa matatizo ya mumeo, najua wanaume wengi ni wabishi sana,lkn inategemea na wewe unaongea nae vipi kama unaongea kwa kumpandishia hapo ndio wanakuwa wabishi anaona kama sasa wewe ndio unataka kuwa mkubwa wa nyumba, wewe mtafutie mda akiwa mzima ongea nae kwa upole,mimi nimejifunza hilo kwa mchumba wangu ukiongea nae kwa sauiti ya juu mtagombana, lkn nilijufunza kuongea kwa ukarimu na kumuomba vitu vingi alivyokuwa anafanya na sivipendi ameviacha alikuwa anavuta sigara anakunywa pombe, akivua nguo atapoiacha ndio hapo hapo utaikuta,lkn ameacha vyote hivyo, so tujifunze sana kuongea vizuri na waume au wachumba zetu,watatuelewa tu na hepuka maneno yatakayo sababisha ugomvi, hata akifoka wewe nyamaza usianze kujibizana nae,yeye mwenyewe atakaa chinni na kutafakari nini anafanya,ok nakutakia kila laheri.

    ReplyDelete
  4. Kwanza, dada violet, pole sana kwa maneno ya kukatisha tamaa wanayokutumia watu, lakini nataka ujuwe, ukiishajiunga ktk shuguri za kijamii, basi uwe teyari kwa yote, utatukanwa, utasemwa, lakini wewe wala usijali, tia masikio yako pamba, fanya unaloona linakufaa wewe, wala wasikutishe na maneno yao ya kipumbavu wapuuzi hao, kwanza usikute wao hawajasoma, ndio maana hawawezi kujua umuhimu wakuwa busy na masomo hasa kipindi cha mitihani,
    Nakuja kwenye mada yetu, kwanza kabisa nampa pole huyo dada, maana najua tabu anazozipata, niliwahi kupitia shida hizo, mume wangu alikua ni mchafu kupita kiasi, yani hata niumwe mimi basi yeye hata chupi hafui, kuna kipindi nilifanyiwa operation nikalawa mwezi mzima, aisee nilikuta chupi zingine zina mavi kabisa, yani hazitamaniki, na yeye alikuwa anaendelea kuzivaa kama kawaida, haoni hata haya, hewa ilikuwa nzito sana chumbani,
    nilichokifanya, nilimwambia kwa upole na upendo, akaniona bwege, nikamuwekea mikakati, kwamba bwana usipooga nahama chumbani naenda kulala kwa watoto, alikuwa anapitisha hata siku tatu hajaoga, kweli nilihama three times nikawa nalala na watoto wangu, ile ilimuuma, nikamwambia kuanzia leo sikufulii chupi tena, akavaaachafu, hadi alipopata fungas wa huku chini, akadungwa misindino kibao, ndio akili ilimkaa sawa, hata pmapenzi sikuwa nampa, alijirekebisha na ss ni msafi zaidi yangu

    ReplyDelete
  5. Jamani pole mama,

    mi nakushauri hivi,

    Fanya kazi kwa uvumilivu, anavyorudi tu na akishafanya mambo zake kule chooni, ingia flash mwogeshe mfute mpulizie manukato nawe nawa kidogo na maji ya uvuguvugu, fanya hivyo kwa kila anavyorudi mara tatu ataacha, hawa wanatakiwa kufundishwa kwa matendo na sio kwa maneno dada utaona tu hali imeisha.

    jitahidi kumwambia maneno mazuri ya upendo. Pia kumbuka wewe ni mlinzi wake, je umesimamaje mbele za Mungu kumwombea ili asifanyike kikwazo kwako? mwombee ili hali hiyo iondoke. Mungu amewafanya kuwa kitu kimoja

    ReplyDelete
  6. wanawake mnavumilia mengi Mungu awabariki. nafikiri ni kumfundisha kwa matendo ikibidi ingia flash kama alivyosema hapo juu ata chupi fua. ni mumeo usipofanya hayo utajiletea magonjwa km UTI na mifungus sungu. muombee sana. ana pepo la uchafu. Violet usijali soma tena kwa bidii blog ipo utaikuta, kwanza ukiconcetrate na masomo ata umu utakuja na maanalitical thoughts zaidi awahelewi kipaper hao. Mungu akubariki

    ReplyDelete
  7. pole sana dada huyo mtu haelewi maana ya shule unapofanikiwa lazima watu walete maneno mabaya, muombe Mungu ufike pale unapopataka na atakusaidia.

    catheline

    ReplyDelete