Tuesday, April 13, 2010

MAMA MKWE ANANIFANYA NITAMANI KUIVUNJA NDOA YANGU- NISAIDIENI

jamani wapendwa wangu, kuna huyu mwenzetu,anahitaji ushauri wetu sana, kusema kweli story yake imenihuzunisha sana, nindefu kidogo, nimejaribu kuiedit kiasi, but tuisome tuilewe ndio tumshauri

Pole na shughuri mdogo wangu, shida yangu ambayo kwakweli nahitaji msaada wenu, ni kwamba, mimi naishi hapa dar es salaam, huku kigamboni, nimeolewa na nina mtoto mmoja wa miaka 3,nilichelewa kuzaa 


Toka nilipoolewa niligundua mama mkwe hanipendi, upande wa mume wangu wamezaliwa wawili tu, yeye na dada yake, ambae anamatatizo ya akili, ana miaka kumi na nne sasa, yani kilema chake hawezi kufanya lolote lile, ni udenda tu unaomtoka masaa yote,
Wakati tunafunga ndoa tulikuwa tumepanga vyumba viwili, mama mkwe wangu akija alikuwa akilala kwenye chumba kingine ambacho nilikifanya kama sebule, anakaa hata miezi mitatu ndio anaondoka, ila ndani ya hiyo miezi mitatu, yani mimi nilikuwa napungua hata mwili, ni mkorofi sana, mwanzoni mume wangu alikuwa upande wangu, alikuwa akinitetea kwa mama, lakini sasa hivi wote wamenigeuka, tangu mume wangu alipokuwa rikizo akaenda kwao, mimi sikwenda kwa ajili ya kazi, basi alikaa mwezi mzima, aliporudi tu! Mambo yakawa mabovu kupitiliza,


Ni kama mtego aliporudi alikuja na huyo dada yake mwenye mtindio wa ubongo, ili niishi nae na kusema maisha ya kijijini na umri wa mama umeenda hawezi kumlea hy bintie , nimeletewa huyo wifi, ni wa kumbeba, hachuchumai kujisadia, wala kupiga mswaki wala nini, akitaka kunya anayaachia tu, mimi nikirudi nafuwa, mahousegilr zaidi ya watano wameondoka wanasema hawawezi kukaa kwa ajili ya ile kero,


Mama mkwe huwa anakuja mara moja moja, na akifika tu! Anaanza vijembe, mara mwanangu ameisha sana, hali vizuri, mambo mengi sana, niliwahi kuongea na mume wangu, nikamwambia huyu jesca kwanini tusimpeleke kule wanakolea watoto wenye hali kama hii? Akakataa, akasema wanapelekwa wasio na ndugu, nimlee tu, na kama sitaweza niondoke mimi. Inaniuma sanahii, na nikiondoka nani atamsadiia


Mume wangu ni muislam, na mimi ni mkristo, kunasiku wote tulikuwa kazini, Yule binti mlemavu wa akili(wifi yangu) alipata kama kifafa vile, akaanguka na kutapatapa, housegirl wangu alikimbia kwenye nyumba ya jirani yetu(mlokole) wakaja kumfanyia maombi, alitulia, niliporudi ndio nikapewa taarifa ile, basi mimi nilimuhadithia mume wangu aliporudi kwania njema tu, violet nilipigwa mimi na housegilr wangu, tulipigwa sana, kesho yake msichana wangu aliondoka kurudi kwao, nikaachwa na mtoto wangu tu! Akaagizwa mama mkwe akaja, waliweka kikao walinisema sana

Nilimwambia mume wangu basi tuwe na wasichana wawili, wa kumlea huyu mdogo wako, na wakumlea mwanangu wote wawili nitawalipa mimi, lakini alikataa nakusema kuwa najifanya nina pesa, ataniachisha kazi, sasa jamani hadi sasa hvi mimi sijui cha kufanya, nilimshauri basi tumpeleke mtoto boding alikataa, sasa niambieni wanandoa wenzangu, nifanye nini? Hamna amani nyumbani, kila siku ugomvi, kipigo, mama mkwe anakazana tu kuwa nina roho mbaya, dini yao inaruhusu mimi kuachwa au kuolewa mke mwenza, na mume wangu anasema kama nimechoka kumuhudumia dada yke basi nikubali aoe mke mwingine wa kumuhudumia jesca, nawaza niondoke na mtoto wangu, au niendelee kukaaa? Au nifanyaje jamani? maana sometimes huwa nahisi kama vile wao ndio walimuharibu akili, kwanini hawataki apate msaada wa maombi





 

7 comments:

  1. pole sana dada yangu, nataka nikwambie hivi, usiruhusu mtu mwingine aivunje ndoa yako, inaelekea mkwe wako ana nafasi kubwa sana kwa mwanae kuliko wewe, inakera sana kuona unakosa furaha kwa ajili ya mkwe, mama ana nafasi yake, but na wewe mke ndio una nafasi kubwa kuliko yeye,KUMBUKA MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE, Usikubali kuwa mpumbavu kiasi hicho, huyo wifi yako ni jaribu lako, na nialzima litakuwa na mlango wa kutokea tu! lishinde, lisikushinde, jiulize, kama sio jaribu kwanini hawataki ulete housegirl wake peke yake, kwanini hawataki akalelewe kule wanakolelewa wenye tatizo kama lake, kwanini hawataki akae na mama yake, hivyo ni vimbinu vidogodogo tu! ambavyo nyuma yake kuna kitu, sio bure, mume wako anakosea sana kukunyima haki yako, kuhusu mkweo kukuchukia jaribu kuongea nae, tena kwa upendo na heshima kama mama, muulize tatizo lako nn na akueleze, pengine kuna mambo unafanya yeye hayapendi,pia mume wako, usikute keshatafutiwa huyo bi mdogo ss wanatafuta sababu tu!, kwanza mnamyima haki mtoto wenu, je hakuna wakubwa wengine upande wa mumeo unaoelewana nao ukawaambia juu ya suala hili wakusaidie? kama wapo ita ndugu zako na zake, muongee ueleze tabu unazokutana nazo, pia waeleze hujashindwa kuhudumia ila muda ndio huna, sio aletwe housegilr hapo, bali apelekwe kule kwa wenye shida hizo apate msaada vizuri, kingine kumbuka kumuomba Mungu aikumbuke ndoa yako, yawezekana kabisa kuwa ni kijaribio chenye jibu jepesi tu! ila kwakuwa umekata tamaa, basi hata hicho kijibu chepesi utakikosa, NO KUACHA NYUMBA YAKO HADI MWISHO, KUWA JASIRI, JIAMINI KUWA WEWE NI MAMA, UKIWA LEGE LEGE, NYUMBA ITAKUSHINDA KWELI, BUT UKIWA MKAKAMAVU, wala haitakushinda.pole mpenzi wangu,

    ReplyDelete
  2. nina mkwe mkorofi lkn yako ni too much pole sana kutoka moyoni kama ni msalaba nakiri nicngeweza kubeba nimepata relief kusoma habari yako mkwe wangu ni changamoto haswaaa lkn ckuipa nafac ya kujadili jambo ili kuepusha shari na huongea mbele ya mwanae inapobidi mana ni mgeuza maneno cjapata kuona na hakuna dalili kwamba ataondoka kesho au keshokutwaaa wanawake tuna kero kulea wakwe i wish misaada ingepelekwa huko waliko ili ndoa ziwe na amani...

    ReplyDelete
  3. dada pole sana jamani yani mimi kwakweli sijaolewa ila ndio niko mbioni kuolewa kisa hiki kimenisikitisha na kunivunja moyo jamani hawa wamama wanaowatesa watoto wa wenzao je huyo wifi yake angekua yuko sawa angeolewa akatendwa ivo angefurahi huyo mama??pole sana kwa hayo ila mimi nachooona hapo huyo mumeo washamtia maneno sanaa huko kwao na ivo mmetofautiana dini ndo chanzo kikubwa hapoo muhimu ni kua jasiri kaa chini na mumeo myajadili haya na kama dada violet alivyosema basi heri uwafate wakubwa uwaeleze hayo matatizo pengine mkapata ufumbuzi ila usikimbie ndoa yako muwazie mtoto ambae hatopata mapenzi ya baba mkiondoka hapo nyumbani

    ReplyDelete
  4. Mhh, hata, mie naona hamna suluhisho bali kuondoka!! tatizo kubwa ni mume akishatekwa akili na mama yake!! yeye ndio mwenye maamuzi, nane awe na priority, wewe mkewe au mama yake!! na akisha chukua sides na mama yake, wewe huna kitu! amethubutu kukuambia ondoka kama huwezi kaa na nduguyangu, unangoja nini!! na beleive me, hakuna mwanamke atakayeweza chukua mzigo huo!!! ilipaswa, ajadiliane na wewe kuhusu kumchukua, then uamuzi wa mwisho utoke kwako, sio mama yake kasema, ye amfungashe tuu na wewe kushtukizia huyu, kaletwa!! ondoka!!!

    ReplyDelete
  5. Pole sana dadaangu.mimi sijaolewa bado but i can feel the pain.dada kama ni mateso unayapata sana atleast ingekuwa hakuna manyanyaso mengine ikabaki kumlea wifi tu mikwa na amani na upendo.Lakin dadangu mi naona hapo raha yao wakuone una suffer am sorry to say this achana nae ukae mwenyewe japo kidogo wanawake wenye moyo kama wako ni wachache sana sidhan kama atapata wakunyanyaswa hivo.mi naamin unaweza maadam unakaz yako jaman.hivi ndo tukae kny ndoa ili mradi watu wajue tunandoa jamani?tunatafuta sifa kuwa na si tupo ndoan?hapana dada maisha yennyewe mafupi kiasi hiki mwanadamu mwenzio akutese hivi?amin dada unaweza kuwa strong muombe mungu akutie nguvu.pia mungu anamakusid ktk hilo inawezekana kuna mafunzo anakupa tubu kama umemkosea pia unahitaji kushirikisha wazee wako hata kama uliwakosea jirudi ongeza iman yako ya kikristo.

    ReplyDelete
  6. Mdogo wangu pole sana kwa yote lakini ndio ndoa hiyo. Ushauri wangu hebu jaribu kuondoka hapo na mtoto wako kaanze maisha ya peke yako na ukizingatia kikazi unacho. Au unahofu kuwa bila yeye maisha hayaendi?? wala usitetereke kwani ndoa imeingiliwa na mama mkwe si ndoa tena itakuwa ni shida kwako mpaka siku ya mwisho. Na naapa watakukumbuka sana kwa wema ulowatendea. Kwani ni vigumu mno mwanaume akachukua maamuzi ya kumleta huyo mdogo wake na hali alonayo ili wewe uje umlee. Hayo yote ni majaribu kwenye ndoa zetu za siku hizi. Huyo mdogo wake ilitakiwa alelewe na mama yake na si vinginevyo bwana labda angekuwa ametangulia mbele ya haki sawa. Kama anaweza kukufanyia wewe visa atashindwaje kumlea mtoto wake wa kumzaaa???

    ReplyDelete
  7. pole sana jaribu lako ni zito, ni Yesu pekee anaweza kukushindia, mfuate Yesu, tua miizigo yako kwake, piga maombi, am telling you hautaamini yatakayotokea, maombi ni kila kitu.mi ndoa yangu ilitetereka sana,ndugu wa mume walinichukia, mama mkwe sababu mtoto wao ambaye ni mume wangu aliugua ugonjwa usiojulikana, nikasingiziwa mimi nimemroga mume wangu.lakini nilisimama ktk maombi, mume wangu akapona, sasa wanaona aibu walisema mengi yamewashuka,walisema kwangu hawatakanyaga, mama mkwe kaumwa kakaa kwangu miezi 6, amefyata kimya hana la kusema,kwahiyo basi maombi ni silaha,mume wangu alicheat akamtia mimba mwanamke nje, mwanamke wa nje akawa ananidhihaki maana sijapata mtoto, maombi yakafanya kazi mimba ikatoka ya huyo mwanamke, sasa naonekana kama mchawi lakini kumbe ni maombi, piga goti kwa Yesu utashangaa. mama mkwe anayekuvurugia ndoa anaweza akapata kibano au hata akafa ukaishi kwa raha.

    ReplyDelete