Monday, October 24, 2011

KABLA HATA SIJAMUOA AMESHAANZA KUSEMA UONGO, (AMESINGIZIA MAMA YAKE KAFA,) NIKIMUOA TUTAWEZANA KWELI??

Habari ya kazi dada, najua Mungu ameweka watu kama nyie ili mwasaidie wale wasiojua, naomba unisaidie dada angu, mimi ni kijana mwenye umri kuoa sasa, mwaka huu mwanzoni nilimpata mdada mmoja ambaye tunapendana sana na nilitaka kumuoa kabisa

Tatizo lilipoanzia ni kwamba, kuna siku alaniambia ana mimba na anaomba kuitoa mimi nikamwomba asitoe kwakuwa nilimuhakikishia kumuoa ina maana mtoto angekuwa kwenye uangalizi mzuri, akanielewa,

baada ya muda mfupi kupita  yeye akarudi kazini kwake alikuwa anafundisha, huku akisoma chuo akiwa chuon kwao siku moja akanipigia simu, akaniambia anaomba nimkopeshe rafiki yake laki mbili ana shida nazo, nikamwambia sina, mambo ni mengi sana, nikahisi amenielewa

kesho yake mchana akabeep nikampigia akapokea mvulana mmoja akasema wewe nani, na mimi nikamjibu mwenye simu yuko wapi, akaniambia mwenye simu ameanguka gafla, na wenzake wamempeleka hospitali, nikaamua  kumpigia rafiki yake nae akawa kama amepaniki akaniambia kuwa yeye(mchumba wangu) ameanguka gafla, kwa kuwa kuna mtu amemjulisha kuwa mama yake amefariki, na aliangukia tumbo mimba imetoka,

kesho yake nikaenda nyumbani kwao (msibani) bila yeye kujua nikamkuta mama yake mzima kabisa, hapo nikajua nimedanganywa, na iliniuma na kunishangaza sana.

toka pale niliamua kukata mawasiliano nae na nilimwambia kabisa kuwa simtaki tena, maana ni muongo, alilia sana na kutubu, niliamua kumsamehe, USIKU ulipofika nikamtomasa akanipa penzi ila nilimwuliza anaweza? akasema ndio,

sasa mimi ni mwanaume naomba niwaulize dada zangu jamani,  mtu akitoa mimba anaweza kufanya mapenzi baada ya siku nne? Na je huyu atafaa kuwa mke wangu kweli??? Maana ameshanistua.10 comments:

 1. Ahahahahaaaa changa la macho hilo. Demu hakuwa na mimba huyo. Kutoa mimba nafikiri ni sawa na kuzaa tu. Huwezi kufanya mapenzi ndani ya siku nne. Ila binti anampenda huyo kijana. Alikujaribu ili aone kama utamfaa au kweli una mpango mwema na yeye. Inaelekea ni mwanamke mwema tu japokuwa kafanya hivyo but nikwasababu ya mapenzi.kama una nia ya kumuoa na muoe tu.

  ReplyDelete
 2. huyo binti hakufai kaka anataka akuchune tu anatumia njia ya uongo kusudi umpatie hela mara ya kwanza amekudanganya anamimba anataka kutoa kusudi ukubaliane naye umpatie hela sasa alipoona umemwambia asitoe akaona sasa njia yake yakupata hela imebaunzi sasa akaja na njia nyingine yakusema mama yake amefariki na angali mama yake ni mzima tena huyu binti ni hatari kuliko ukimwi anawezaje kusema mama yake amefariki angali hai huyu kaanaye mbali kabisa akufaa afadhali mungu amekuonyesha mapema ukimuoa utakuja kujuta hakufai tafuta mwingine mwenye mapenzi ya kweli na wewe utampata hukuchelewa omba Mungu akuwezeshe kumpata mke mzuri kwani mke mzuri anatoka Mungu pole kaka

  ReplyDelete
 3. Hilo bomu kaka achana naye kabisa

  ReplyDelete
 4. Pole kaka.Hapo kuna kasababu kinachomfanya akudanganye. Labda haumpi pesa za matumizi akatanue na marafiki zake. heheh. Ningependa kujua ana umri gani huyo binti? Na wewe una umri gani?

  Hata mie ni mwanamke, nakumbuka nilipokuwa kijana nilikuwa na mpenzi hasie eleweka, halikuwa hajui kumpa ela mpenzie akanunue anachotaka. Nami kumuomba mtu naona aibu, basi tabu tu. Siku moja nikamuibia pesa, na nikamdanganya eti nilikuwa na mgeni labda ndio kaiba, mwisho akagundua kuwa nimemuibia. Ndio tukachana huku tunapendana, inauma sana.

  Alipo gundua kama ilikuwa ni makosa yake mwenyewe kuto nipa mimi pesa za matumizi, akajilaumu sana ila ilikuwa to late.

  Sababu haikuchelewa mie nikaolewa na mwingine, ambae anagawana na mimi anachopata bila kumuomba.
  Ushauri wangu
  kwanza kuliko yote jaribu kutafuta sababu inayomfanya akudanganye, kuzusha vituko vya uongo kwa sababu umpe ela. Muulize sababu zilizomfanya akudanganye, ela akizotaka alitaka kufanyia nini au kama anadeni!!!!na mulize je kama anania ya kukulaghai kipesa na anatumia hizo mbinu za uongo!!!!

  Hakika ukimuliza kwa upole, na kumuakikishia kwa yote yaliotokea, atakuambia. pengine anadaiwa na rafiki yake au anataka kumpa mama yake ela nk.

  Baada ya hapo, mkabidhi hizo laki 2 kama unazo.
  Baada ya hapo. Kama haumpi ela za matumizi, jaribu kumpa mara kwa mara. Mulize maitaji yake, yaani unamuliza mwezi mara moja anaitaji kitu gani ili umpe ela akanunue au akastarehe na marafiki zake.


  Hakikisha tu hasikufirisi, na hasikuyumbishe kipesa. Mpe kile unachotaka wewe na sio anachotaka yeye maana hizo ni pesa zako sio zake. Na usimzoeshe akuombe ombe ela. ni tabia mbaya.


  Jua tu, waschana umri flani ni waongo sana, ndio wameumbwa hivo. Ndio ubaya wa kuwa na akili nyingi kichwani, wanataka wawazidi ujanja maboy friends zao.

  Kama anakupenda tu, unaweza kupuuza uwo uongo wake, na unamuambia wazi kuwa uongo wake haupendi bora akitaka kitu aseme wazi.

  ReplyDelete
 5. ACHANA NAE KIMEO HUYO, ATAKUPOTEZEA MUDA BURE, YANI HUYO NI NGULI LA UONGO,

  ReplyDelete
 6. u better run away fast, run bro runnnnnnnnnnnnnnnnn.

  ReplyDelete
 7. Mh km unamjali na unampa hela za matumizi kulungana na uwezo wako ilo chenga la macho anachotaka kutoka kwako ni hela tu kweli mtu unaweza kumdanga mpenzi wako umefiwa na mama mzazi.

  ReplyDelete
 8. WE UTOE MIMBA SIKU UFANYE TENDO LA NDOA MONGO MKUBWA HUO ACHANA NAYE KIMEO HUO ASIKUBABAISHE KABISA

  ReplyDelete
 9. anaweza akawa muongo na sio muongo wakati mwingine anafnaya hivyo akuone unamsimamo gani juu yake, je akikwambia anamimba utamwamwambia atoe au abaki nayo? hapo atapata jibu, je upande wa ndugu zake je unamsimamo gani juu ya wazazi wake? Mama amefariki je unachukuliaje kama mume mtarajiwa? ulikimbia mbio kujua je nikweli? hapo jibu kapata. Ndugu yangu akili sasa ni kwako sisi tutakushauri tu lakini akili kumkichwa wengine wanatumia hivyo kuwajua wenza wao wanamalengo gani katika mahusiano? Na wengine wanatumia hivyo kutaka kuwachuna tu. Lakini kama alikiri na kutubu ukamsamehe na mkaingia kwenye sita kwa sita alitaka akupe jibu kuwa mimba hajatoa. Akili kumkichwa. Kwa ufupi ANAKUPENDA.

  ReplyDelete
 10. mh mapenzi ni upofu hakuna mtu aliye kamilika na mpaka ukampate aliye kamili umri utakuwa umeenda cha kufanya jaribu kumuweka sawa kwanza. ikishindikana siyo riziki yako tafta mwingine.

  ReplyDelete