Monday, October 3, 2011

KILA NIKILALA, NAOTA NINAMUUA MUME WANGU,
Habari ya kazi dada v, pole, 
mimi nina shida moja ambayo inanisumbua kwa kipindi kirefu sasa, kila nikilala huwa naota nimemuua mume wangu, yani nakuja kushtuka pale aliponyooka na kukata roho, ndio huwa napiga kelele sana na kuamka, nikiamka hujikuta mwili wote unatetemeka, jasho jingi linanitoka, 
mume wangu huniuliza tatizo ni nini? naogopa kumwambia nilichoota, hivyo humdanganya ndogo ingine tu!, huwa anainuka anipa maji ya kunywa kisha nalala, 
imejirudia takriban mwezi sasa, hadi nakosa hata amani, ukizingatia wala sijagombana na mume wangu na wala hata simuwazii kufa, 

yeye mume wangu alinishauri niwe naweka bible kichwani, nalaria, lakini hali hii wala haistop, na mida ya ile ndogo iko pale pale, sasa huwa naweka alarm kwenye simu ikifika mida ile tu! nainuka na kuanza kusikiliza radio, kipindi cha maombi, lakini hujikuta nimepitiwa na usingizi mzito, na nikija kustuka tu! najikuta nimeshaota, na jasho linanitoka,

nampenda mume wangu, naombeni ushauri wenu jamani, pole dada vai kwa kukusumbua, ila naomba usilitaje jina langu, wala email yangu3 comments:

 1. pole dada mimi nakushauri kama wew ni mkirsto uwe unaenda ktk maombi uombewe hiyo ndoto ya mauti ikutoke na wewe unapoota ndoto hiyo ukishtuka upige magoti na kusali maana hiyo i roho ya mauti nenda kanisani uwaambie tatizo lako wakuombee nafikiri shida yako itaiisha usali sana ni hayo tu pole

  ReplyDelete
 2. Pole sana, mie pia nakushauri kama Huyo Anonymous wa kwanza alivyokushauri. kama wewe ni mkristo au hata kama sio mkristo inabidi upate ushauri wa kiroho na uombewe ili hiyo hali iondoke kabisa na isijirudie tena. Kabla ya kulala omba sana hata kwa machozi ikatae hiyo hali na jikabidhi kwa mungu. Unajua nini, hiyo kitu kama haitakutokea wewe hapo baadaye basi itatokea kwa ndugu, jamaa na hata wazazi wako, wewe unaonyeshwa ili uchukue hatua ambayo itasaidia kuiokoa hiyo roho inayotakakudhulumiwa. chukua hatua sasa dadangu.

  ReplyDelete
 3. usijali wewe ni dhehebu gani, kimbilia haraka kwenye maombi, kwa kina mama rwakatale au kwa mchungaji salu pale buguruni, nenda watakuombe utapona, hilo ni pepo mauti linataka kuingia kwa mtu wa karibu yako, na atakaekuuma sana, hapo kimani na kimaono zaidi ni kwamba Mungu anakukumbusha kuamka na kuomba kukemea roho ya mauti, sasa ukiendelea kuwa kimya, itakucost, ni heri uchukuwe hatua,
  MUNGU AKUBARIKI SANA NA AKUHURUMIE, MIMI PIA NITAKUKUMBUKA KWENYE MAOMBI YANGU,

  ReplyDelete