Tuesday, October 18, 2011

NAHIS MAMA NILIYE NAE SI MAMA YANGU MZAZI, NIKIMUULIZA JUU YA HILI NI MKALI SANA NAOMBENI USHAURI WENU

Pole dada violet kwa ujumbe mrefu, hapa nimeufupisha sana
Mimi ni mschana wa miaka 21, akili timamu ya kutambua vitu ilinikuta nikiwa nalelewa na mama tu! Kwa kuwa baba yangu alifariki, 

kwa huyu mama tuko watatu mimi nikiwa mtoto wa kwanza, kwa kuangalia ni kweli tuko tofauti sana sura, maumbile na hata rangi, wao ni weusiii na mimi ni mweupe sana, ila hiyo sio tabu maana baba yangu pia ni mweupe sana, nahisi kuna kitu nyumba ya panzi kimejificha dada v

Huyu mama hapendi maendeleo yangu, yeye pamoja na watoto wake, hadi kufikia kusema hivi ni mengi nimekutana nayo nikiwa chini ya malezi yake, amekwamisha mambo yangu mengi sana, nikimuuliza kuhusu ndugu shangazi zangu upande wa baba anasema baba yangu hana ndugu eti alizaliwa peke yake na wazazi wake (bibi na babu) walishakufa hivyo ukoo nao ulikufa. 
 
Ilitakiwa niende Nje kusoma zaidi, kuna msamalia mwema alijitolea kunisomesha na gharama zote ni juu yake, lakini mama akabana ile nafasi kaenda mdogo wangu wa pili,(mtoto wake), na  bado haikutosha, hataki mimi nifanikiwe na chochote, kuna siku nilimuuliza hivi kweli wewe ni mama yangu? huwezi amini hata kutoka huwa anatoka na huyu mdogo wangu mdogo aliebaki mimi ni kama mschana wa kazi
, naumia sana, naandika huku mahcozi yananitoka dada, kila ninachomwambia anakuwa mkali, na ninapozidi kumuuliza maswali mengi ananichukia sana

Kuna siku alikuja mama mdogo (mdogo wake yeye) na kukuta mama amenipiga hadi mkoo umevimba, nikawasikia wakiongea seblen, mama mdogo akimsema, na kumwambia, au kwavile sio mtoto wako? Hapo ndipo nilipozinguka fahamu kuwa mimi si mwanae kutokana na hivi anavyofanya,

Nisaidieni dada v, nataka kujua ukweli juu ya wazazi wangu, hata kama wote walikufa basi nijuie tu! Hata walipolala, kwanini nanyanyaswa hivi?? Niliwahi kujaribu kumuuliza kidogo tu! Ilikuwa kesi, niliitiwa hadi mjumbe, lakini moyo wangu bado una kitu! HUYU SI, MAMA YANGU.  Nataka kuprove hilo kwanza, nisaidien mdogo wenu, nina wakati mgumu sana
asante dada Violet, 
5 comments:

 1. pole mdogo wangu, nakuhurumia sana, huna ndugu yeyeote wa karibu ili akusaidie kuujua ukwel

  ReplyDelete
 2. Pole sana nimeumia sana dada yangu mpaka mimi pia machozi yakanitoka! fuatilia lazima utajua tu au jaribu kumfuata huyo mama mdogo mueleze mateso unayo pata! pole sana mdogo wangu jaribu kuuliza hata mlipo kuwa mkiishi zamani huenda wanajua juu ya hilo!

  ReplyDelete
 3. Pamoja na magumu na mizito faitik kusoma hata hapo Tz uwe na maisha yako tafuta chumba chako yule anzisha binadamu hatulingani na mungu akitaka ufanikiwe utafanikiwa tuu hata iweje, pia mshrikishe mungu sana katika hizo hali unazopitia ndugu yangu ili akuvushe iwe historia tuu

  ReplyDelete
 4. Mdogo wangu pole sana kwa yanayokukuta ushauri naokupa usiache kumuomba Mungu atakuonyesha njia ya kujua yote na kwa kuanzia huyo mama mdogo anaonekana ni mtu mwema kama aliweza kumsema dada yake kwa aliyokufanyia nakushauri kama unaweza mtafute bila huyo mama hapo kujua muombe akuambie ukweli anaweza kukusaidia

  ReplyDelete
 5. Pole nakuonelea huruma. Labda alikuiba sehem. Lakini miaka yote hiyo ulie ishi nae hata kusikia tetesi?

  Ushauri wangu wa kwanza:
  Tafuta msamalia mwema mwingine nenda nje ya nchi kajisome bibi we, kaza buti hasikuzibie riski yako, na mambo yako ya kimaendeleo fanya kisiri hasijue. Mkimbie kiivo.


  Na ukifika nje ya nchi vunja mawasiliano nae, wasiliana nae mwaka mara 2. Maana husitupe jongoo na mtu wake, labda kuna siku utamuitaji tu. Maisha haya bwana mdogo wangu.

  ukimaliza masomo, anza maisha yako, na karibu kuwa nae mbali sana na usimpe nafasi ya kujua maisha yako, maana anaweza kukuaribia.

  Alafu unaweza ukapima DNA test ambayo itaonesha kama mama ako au kama una ujamaa nae.

  Na akika ni ngumu kumuomba mukapime DNA test, na bila shaka atakukatalia. Na uadui utaanza. kuwa makini sister.

  Kama mimi ningekuwa wewe, ili upate damu yake unaweza kuwalipa pesa majambazi wamkamate na wamtoe damu tu basi, mupeleke kwa mahabara inayo test DNA.

  Ukisha jua sio mama ako, hapo sasa ndio mchokonoe huyo mama ako mdogo na muambie unajua kama dada ake sio mama ako. Na muambie akuambie tu utafanya siri ya wewe na mamdogo, akuambie wewe nani mtoto wa nani kwako wapi nk.

  Mdanganye mamaako mdogo kipesa, ili akuambie. Najua umri wako mdogo na pesa tabu. Na bila pesa tz huwezi kufanikiwa utakalo.

  kimbia nchi kwanza BIBIE, ili mawazo yapanuke. Husikose kutuletea news mpendwa

  ReplyDelete