Monday, October 31, 2011

NIMEKUTA SMS YA UTATA TOKA KWA MR. WANGU KUJA KWA HOUSEGIRL WANGU

Nimekuta sms ambayo imetumwa na mume wangu kwa bint wa kazi, sms hii imenipa wakati mgumu sana, yani hata sijui nifanyaje
Wiki iliyopita nilikuwa nyumbani, sikwenda ofisin, kwakuwa nilikua naumwa , basi ilipofika mida ya mchana nilimtuma bint wa kazi aende akanichukulie matunda ya juice sokoni, sasa sijui ilikuwaje akasahau simu yake, nikajikuta nashawishika kusoma sms zake maana simu huwa inamkeep busy sana, na huwa hataki mtu aiguse kabisa, sometimes akipigiwa simu anakimbia kwenda kupokelea nje kabisa na yuko radhi  hata aende na simu bafuni kuoga nayo,  

Sasa siku alipoisahau nikasema hapa hapa, ngoja nione kwanin huwa anaificha sana,  nimejuta jamani, nimekuta mume wangu ametuma sms  inasema hivi (leo umeandaa nini dear ??) na sms inaonyesha imetumwa masaa mawili  yaliyopita,

Ninachojiuliza, mr anajua kabisa kama mimi niko nyumbani, kwanini asinitumie mimi kumuuliza housegirl anaandaa nini? Mbaya zaidi kwanini amuite dear?? Nilipomuuliza  dada baada ya kurudi kwanini baba anakuuliza hivi, akasema sijui mwenyewe, mbona kila siku ananiuliza namuandalia nini?

Nikamuuliza anamaanisha nini anapokuuliza hivi, akasema sijui mwenyewe, (lakini hata jinsi anavyojibu, ni kwa kiburi sana, as if ana jelous na mimi,) nikapiga kwa mr. nikamuuliza kwanini usiniulize mimi, unamuuliza house gil kwan yy ndie mke, mimi si ndio nafanya kila kitu

Akanijibu kuwa napenda kujipa presha za bure kisha akakta simu, nikipiga hapokei, jioni karudi kauchuna hadi sasa hatuongei,

 mwaka umepita  sasa, alishawahi kutembea  na mschana wa kazi ambae nilimfukuzaga baada ya bint kukiri kuwa  kweli ametembea nae,  sasa nahofia na kwahuyu isije kuwa hivyo, nishaurini mwenzen3 comments:

  1. mwee yaani hawa wanaume zetu jamani,sasa dada yangu,mi mwenzio siku hizi nimejifunza subira,najua inaumaaa kupita maelezo kwakuwa wampenda mumeo ,ila ungezidi kuweka mitego zaidi ujue ukweli ,sasa hapo atajitetea na matokeo yake wewe utaonekana mbaya,upo hapo?yaani nikutokua na heshima nasisi,misikubaliani na usemi eti kila kitu wamwachia housegirl,hiyo ni big NO,mbona sisi tunajinunulia mahitaji yetu mengi na hatutembei na wauaza maduka,or tunajilipia nauli za basi na sisi basi tutembee makondakta.

    ReplyDelete
  2. Muondoe huo msichana na kama watoto ni wakubwa tafuta house boy sasa amtongoze house boy, ukipata mvulana mzuri anafanya kila kitu. hawa waume zetu hawa mweeeeeeee, jipe moyo mtoe kwa upole kabisa bila ugomvi dada yangu, na usiwe unajisahau sana na wewe kila kitu aandae house girl japo upo bize na kazi siku moja moja unapika mwenyewe ukiwepo

    ReplyDelete
  3. mahouseboy ndio wabaya zaidi, bora mume atembee na msichana wa kazi kuliko watoto kubakwa au kulawitiwa na mahouseboy, hawachagui kama kuna watoto wa kike watawabaka na kuwalawiti, kama ni watoto wa kiume watalawitiwa. ni bora udili na mwanaume wako kuhusu tabia yake kuliko kuleta maaafa makubwa ndani ya familia.bona dunia imekuwa chungu hivi jamani??/

    ReplyDelete