Wednesday, December 15, 2010

MKE WANGU HAPENDI NDUGU ZANGU HATA KIDOGO- NITAMFANYAJE AACHE TABIA HII


Wanawake wengine sijui wakoje jamani, inahusu nini kuchukia ndugu wa mumeo bila sababu ya msingi, au hata kama kuna hizo ''sababu  za msingi'' watu hukaa na kuongea mkayamaliza, sasa wewe unanuna hata kutembelewa hutembelewi lo! vibaya jamani, wanawake wa tabia hii mjirekebishe, raha kupendwa na ndugu wa pande zote, kupenda kuwa kivyakovyako ni dalili za uchoyo na ubinafsi wala haifai, kaka huyu amenisikitisha kweli,  soma hiyo!!!!!!!!
Nahitaji ushauri wenu sana,
Nilioa miaka miwili katika ndoa yangu, na sikugundua kama mke wangu anatabia hii, maana tulikuwa mbalimbali, tulipojuana tu! Yeye alikwenda South Africa kusoma, namimi nilikwenda UK, baada ya kumaliza, tulikutana Dar, (ambako ndio kwenye familia zetu) tukaanza maandalizi ya ndoa, na hatimae kuona, sikuweza kumchunguza tabia zake, nadhani nilifunikwa na upendo niliokuwa nao kwake.

Shida ni kwamba, mke huyu amechange  kiasi kwamba namuogopa hata mimi, ni mtu wa hasira sana, mtu wa kususa, some times anasusa hata kupanda gari yangu mimi, yuko radhi akapande daladala, sasa mimi maisha haya sijayazowea.

 Ndugu zangu wakija ni mkorofi, anaona kama anabanwa vile, wakati nina nyumba kubwa tu! Na ina nafasi, tena asilimia ya ndugu zangu wako busy na shughuri na familia zao, ila ikifika kipindi cha December wengi hupenda kuja kwangu, kubadilisha mazingira, yani wakifika mke wangu, anachelewa kurudi kwa makusudi tu! Na anaweza kuamka na kutoka bila hata kumsalimia mama yangu na ndugu zangu, yaweza pita hata siku tatu hajawaona.

Mama ni mtu mzima, aligundua hali hii, na akasema kuwa yeye atakuwa haji, ila akinimiss itabidi niwe naenda hata weekend kumsalimia, mama ananipenda sana, maana mimi ni mtoto wa kiume pekee kwa mama yangu,  nikisaidia kwetu nikimwambia tu kwamba nimetuma hela nyumbani, anaweza nuna hata siku nne, bila kusema na mimi, sometimes huwa natuma bila yeye kujuwa.
Nashangaa ndugu zake yeye hawaishi pale kwangu, leo atakuja huyu atakwambia ni mtoto  wa uncle yuko uingereza, kesho atakuja huyu atakwambia ni mtoto wa binamu, mimi huwa sijali 
 maana huwa naamini  wageni  wanaongeza riziki katika familia.

Sasa ndugu zangu wamesusa kuja kwangu, nami nilishazowea wageni, tuna mtoto mmoja tu, ana mwaka na miezi minne, cha ajabu hata ndugu zangu walioko Dar, wakitaka kuja kumchukuwa wakashinde nao kwao mke wangu huwakatalia na husingizia anaumwa.

Naumia sana, naombeni ushauri wenu, naogopa hata kuwaambia wazazi wake maana najuwa baada ya kumsema, nitanyamaziwa hata miezi, na mimi hali hii siipendi na wala sijaizowea, maana hadi huwa naogopa kuwahi kurudi nyumbani siku ambazo amekasirika, mtoto atapigwa na kufokewa kama mtu mzima, naweza kumtandika makofi, lakini nampenda ila nachukiwa tu! tabia zake? je anaweza kubadilika kweli???
13 comments:

 1. Pole sana kaka kwa huo msalaba. Mimi nafikiri unatakiwa ukae uongee naye kuhusu hiyo tabia yake na umwambie kuwa hupendezwi nayo! Zungumza naye, ikishindikana washirikishe wazazi wake. Wageni ni baraka katika nyumba,nakushauri umshirikishe Mungu katika suala hili kwani kwa Mungu hakuna lisilowezekana! Omba bila kuchoka Mungu atainusuru ndoa yako.

  ReplyDelete
 2. Ndugu yangu yote hayo ya nini unampenda mtu anayekufanyia yote hayo!Maisha ni mafupi kaa chini ufikirie kwanini unakosa raha maishani kama hata kubali kubadilika tafuta ustaarabu mwingine kuliko uje upate ugojwa wa moyo kwa mtu uliyekutana nae na kuoana.

  ReplyDelete
 3. kina tatizo lako limenigusa sana japo sijui wewe nikabila gani wala dini gani auko peke yako haya mambo kuhusu familia hili taizo kama lako liko sana kwa baadhi ya familia kwa kaka usivunjiko moyo najua kwa kiasi gani linakukera na kukunyima raha mimi ushauri wangu huu sikushauri umwache ila waite washenga wako na wazee wakanisani km mlifunga ndoa kikristo wamkalishe chini wamkanye juu ya jambo hili usiogope kwamba ukimsemeea atakugomea hapana usipomsemea itakuwa hujatatua tatizo ukikaa kimya na utakapo fanya hivyo ninavyokuelekeza kaka yangu usiache kusali mungu nakufunga piga goti maana mungu nimwema atasikia kilio kwa mwanamke mwema anatoka kwa mungu wala usichoke kusali hakunalinalo mshinda mungu pole sana mke wako atabadilika tu usikate tamaa majaribu ni mengi kwawanadamu

  ReplyDelete
 4. eeeeeee makubwa. Hapo unakazi kaka, pole sana. Mie nazani huyo mwanamke anaogopa jamaa zako wataaribu ndoa yake. Pengine jamaa zako wanamsema sema na yeye mwenyewe kagundua. Au aliwafumania jamaa zako wanamsema. Inavo onesha hawaamini jamaa zako hata kidogo. Au pengine anaona jamaa zako hawampendi sana,ndio sababu ya vituko vyote hivo wakija. Au anaona dalili akizoeana na jamaa zako ndio ndoa yake ameitia motoni, ndio maana anawakwepa kwepa na kuwaepuka. Na pengine unae mpelekea ela ndio anae muhofia sana, ndio maana ananuna. Au pengine anaona unamnyanyasa kwa kigari chako na kinyumba chako, ndio maana anasusa na kuona bora akapande daladala. Au jamaa zako wanamnyanyasa kwa vimali vyako, au anajiskia mumemuweka chini na wewe juu. Kuna kitu tu anaogopa au hajiski vizuri. Na anaogopa akikuambia atakumiza, kwaiyo anaishia kuumia mwenyewe na kuchange tabia yake. Pengine wewe na familia yako ndio chanzo kimemfanya achange kitabia ghafla. Jaribu kufanya utafiti.Husimlaumu mtu wakati chanzo ni wewe mwenyewe na familia yako. Angalia lugha unayotumia kuzungumza nae, na angalia tabia yako pia.Na angalia lugha wanayotumia jamaa zako kuzungumza nae na tabia ya jamaa zako kwa mkeo. Pengine kuna katabia kwenye familia yako yeye haipendi. Kwani hiyo nyumba yako imekuwa holiday house or? Mwanamke unaolewa na mume mmoja tu na sio kumi na moja. je hao jamaa zako wanakaa mda gani hapo? na je kama wataamia kabisa je, maana familia za kiswaili hazieleweki.

  ReplyDelete
 5. NILIKUWA SIJAMALIZIA. HAPO JUU.
  Cha kufanya ninavo ona mie ni, kutafuta gia kule kitandani, kipindi ambacho upo katika holiday au weekend mukiwa peke yanu, siku ambayo umeiona mkeo anafuraha moyoni, muulize kwa lugha nzuri na ya busara, mfn, "unahofia nini mke wangu? alafu akikuliza kwanini? unamuambia juu ya jamaa zangu naona wamekukosea, au mie nimekukosea pia mke wangu. Nisamehe mke wangu. jifanye mjinga.. mpaka upate unacho kikusudia. Atakuambia tu

  ReplyDelete
 6. Sikiliza wewe mtoa Mada hii "Mwanamke asikusumbue OA MKE MWINGINE huyo atashika adabu" hawazi kusumbua mwanaume kiasi hicho. si umesema nyumba yako kubwa! mlete humohumo ndani mwambie mkeohuyo kwa upole sana kuwa kwa kuwa wewe hupendi ndugu zangu sasa nimemleta huyu mke mwingine ili huyu ndio aongee na ndugu zangu. Kwa vyovyote vile ata-react akifanya hivyo uamrudisha yule mke fanya kama mchezo wa kuigiza hivi atanyooka huyo kisura wako" Wanaume ni bidhaa adimu sio wa mchezo..........Kizito!!

  ReplyDelete
 7. kwikwikwi mdau hapo juu umenifurahisha sana, hiyo dawa nzuri sana mbona atakoma hatanuna tena teh the teh

  ReplyDelete
 8. Hahahahahh!! Kizito
  umenivunja mbavu...Mwenzangu usilete maigizo katika mapenzi patatoka kivumbi apo.Sema uyu kaka ana mapenzi sana.Naanaependwa habari apati Inahuuu
  Yellow

  ReplyDelete
 9. kuwa makini kaka ufanyajo, usije ukauwasha moto ukashindwa kuuzima. Kama haumtaki huyo mwanamke oa mwingine. Jifanye mbabe tu kama unavoshauriwa. Pengine ukamkosa na mke mwenyewe. Je ukija na mwanamke mwingine, na yeye akifunga vitu vyake na kuondoka, utafanyaje? Na pengine utakapo ingia patakuwa pagumu zaidi kuliko hata hapa

  ReplyDelete
 10. I HAVE NEVER COMMENTED ON THIS BLOG BUT TODAY NA COMMENT COS NIMEUMIA SANA UR WIFE IS SO STUPID HAJUI MAISHA HUYO NA KINACHOKUJA NI MCHOYO SO ALICHOSEMA KIZITO YUKO RIGHT MSHIKISHE ADABU THEN UKIBADILIKA NDIO WANAKUWA WA KWANZA KUNYWA SUMU MUME KABADILIKA HUYO KAZOEA ILE MIJIUME MISHENZI AMA KWELI PENYE MITI HAPANA WAJENZI BUT KAMA KWELI UNAMPENDA MVUMILIE NA JARIBU KUTUMIA NJIA ZA KIZITO ILI AONE TABIA YAKO INACHANGE MAY BE ATABADILIKA HATA SIKU MOJA LALA HOTELINI MWAMBIE NIMEPATA SAFARI YA GHAFLA THEN ZIMA SIM ZOTE HUYO ANAHITAJI KUJAZWA MAPENZI NAMAPENZI UNAMJAZA MWANAMKE KWAKUMFANYA AWE NA WIVU AJUE ANYTIME U CAN GET ANOTHER MAY BE IT WILL WORK KANIKERA ALL N ALL VERY SORRY HII DUNIA INA MAMBO MENGI SANA

  ASMAR

  ReplyDelete
 11. bro asikuzingue ukawa unaumiza kichwa.mwanamke wako ni mchoyo ndo mana anaroho iyo.ndugu zako ni muhimu kuliko chochote.upatapo na shida ndugu ni wakwanza na marafiki.mtoto uwe unampeleka kwa ndugu asiige tabia ya mama yake.akinuna na wewe nuna usimsemeshe.dawa ya jeuri kiburi zaidi yake.inaonekana yupo anae mpa kiburi.mwite msimamizi wa ndoa yenu aongee nae.ukishindwa kabisa mwambie mama yake.kama bado jeuri.amua wewe kuongoza nyumba kwakuwa wewe ndio kichwa cha nyumba.ila usisahau kumtanguliza mungu mbele ambadilishe.

  ReplyDelete
 12. pole sana kaka kwa mtikhani ulionao naomba nikuulize swali kwani wewe ni dini gani kama wewe ni mwislamu asikuchanganye sana muolee mke wa pili halafu akinuna hamia kwa mke mdogo mbona atabadilika tu huyo

  ReplyDelete
 13. huyo mwanamke kwa kifupi ni mchoyo, pili inaonekana wewe unahela sn so anahofia kama ndugu zako wakija wanachunguza kitu fulani. na anaonekana hana mapenzi ya dhati bali ni mali na ukija kuishiwa humuoni tena hy. hakupendi kaka yangu anapenda pesa hana lolote ulafi wa mali unamsumbua.

  ReplyDelete