Monday, December 27, 2010

MUME WANGU ANAKUNYWA POMBE HADI ANAJINYEA - NIMFANYAJE APUNGUZE AU AACHE KABISA???

Wadau nisaidieni, nimechoka maisha haya,
Mume wangu ni  ni mywaji mzuri sana wa pombe, nilimjua akiwa anakunywa hivyo kumbadilisha ilikuwa ngumu, lakini sasa hivi too much, anakunywa hadi anajinyea, wenzake wanamrudisha hoi, nimemsema mpaka nimekata tamaa, hivi atabadilika kweli?
Nimfanyaje aache pombe, maana hakuna siku anayolala bila kunywa pombe yani bora akose chai kuliko kukosa pombe, kwenye gari huwezi kukosa pombe, hadi jasho analotoa linanuka, akiingia chooni akitoka kila mtu hujua kaingia nani, siku zinavyokwenda anazidi kuchakaa,  namuonea hadi kinyaaa, kuna uwezekano wa kuacha pombe kweli?2 comments:

  1. happy new year to you.

    nakushauri mwaka huu ubadilike, weka habari mpya mara kwa mara maana mwezi unaweka taarifa moja, kweli inaniboa mi msomaji wako na napenda sana blog yako. ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  2. Hii kali lol sina mbavu jamani yaani nimeshindwa kusema mengi labda tu Muombee tu kwa Mungu na pia endelea kuulizia kama kuna dawa ya kuacha pombe.Sasa si umuulize anapata starehe gani kunywa hadi kunya? na akinya nani anamsafisha? kweli kua uyaone lol

    ReplyDelete