Wednesday, September 22, 2010

NINA TATIZO LA UZAZI, MGANGA AMESEMA NIMEROGWA, MCHUNGAJI AMESEMA NIMEFUNGWA, SASA NIFATE LIPI? NISAIDIENI

Kuna kipindi niliwahi kurusha mkasa wa huyu dada, kwamba anatatizo la kutoona siku zake, na anahofia linaweza sababisha asiweze kuzaa, sasa watu walimshauri , wengine waliahidi kumsaidia, but hakuna mafanikio, hebu naomba tusome anachokisema, na ninaomba kwa mwenye uwezo wa kumshauri/kumsaidia afanye hivyo ili nae aitwe mama jamani, kuitwa mama  kuna raha yake! tena ni sifa. tumsaidie mwenzetu!
 

Hello Dada Violeth,

Natumaini wewe ni mzima wa afya pamoja na familia, nadhani utakumbuka kuwa nilishawahi kuja kuomba msaada kwako na kupost tatizo langu na watu pia walichangia na kupata mawazo tofauti tofauti.

Inshort sijafanikiwa mpk sasa ila nataka kukujulisha yaliyojiri katika tatizo langu hili nililonalo mpk sasa na nimepata mawazo mengi sana.. Nikianza na yule aliyesema atanitumia dawa ni muongo nilijaribu kufanya mawasiliano na yeye na nikampa na anuani yangu lkn hakuna kitu matokeo yake aliingia mitini.

Dada Violeth nimejaribu kwenda hospital mbalimbali kujaribu kwa mara nyingine nilienda kwa Kairuki, Muhimbili, Sinza pale MICO kwa madaktari bingwa wa akina mama, Aga Khan bila ya mafanikio nikipewa dawa natumia na nitapata kwa mwezi mmoja lkn kwa miezi inayofuata hakuna kitu mpk madokta huwa wanabaki kunishangaa coz nikipiga ultra sound hakuna tatizo lolote linaloonekana. Basi ikabidi nijaribu tiba mbadala...

Nikaenda kwa mama mmoja anakaa Tanga aliniangalia akasema haya ni mambo ya kishirikina kwamba kuna mtu tena jirani yangu alichukua unyayo wangu na kunifunga.... Mmh ilinipa wakati mgumu sana kuamini nikapewa dawa za miti shamba na nikanywa kwa wiki kadhaa lkn mama yangu akanishauri nijaribu kwenda kanisani kumwomba mungu nilienda kwa mama yangu kitunda na nikaenda kumwona mchungaji.

Nilimuelezea mchungaji A - Z kuhusu maisha yangu tangu utoto wangu na sikumficha kitu basi nikaombewa pale na mchungaji akaniambia atafunga kwa ajili mpk aonyeshwe matatizo yangu na mwenyezi mungu. Kusema ukweli nami nikaamini hivyi wiki lililofuata nikaenda kanisani kama kawaida mwisho wa misa mchungaji akniita na kuniambia ameoteshwa kuhusu mimi kuwa kuna mtu amechungua nguo zangu na kwenda kutundika kwenye mti mkavu usiotoa maji wala majani( kwa maana mti usiozalisha) sio siri nipo njia panda hata sielewi pa kuanzia.

sielewi  chakufanya nizidi kumwomba mungu au nianze mambo ya kiswahili.... Nipo njia panda.

Ni mimi mdogo wako,


13 comments:

  1. pole dada kwa yanayokukuta, lakini njia nzuri nayoiona nio kumwomba Mungu kwasababu yeye ni muweza wa yote.. kwa mambo ya mganga nadhani huko unapotea tena sana tu. plzz muombe Mungu!

    ReplyDelete
  2. Pole sana dada, mimi nakushauri wewe mng'ang'anie mungu tu! hao waganga usiwaamini kabisa, nakuomba sana, mungu anaipima imani yako tu! aone jinsi gani unavyojisimamia? wewe mshikirie mungu tu! nami nitakukumbuka kwenye maombi yangu, kama alivyosema violet, raha sana kuitwa mama, nitakuombea mdogo wangu, ila nawe amua kubaki kwa mungu tu!

    ReplyDelete
  3. mm! wewe nawe sasa unataka kuyakoroga wewe, kwa mganga umefata nini? acha kabisa, au amua kitu kimoja, kuwa moto au baridi, kama kwa mganga zamia huko, usimshirikishe mungu, maana nuru na giza kamwe havikai pamoja,
    BWANA ACHA MAMBO YA WAGANGA, TULIA KWAMUNGU TU

    ReplyDelete
  4. mie mama yangu alipoolewa alikaa mwaka mzima bila kuzaa akaanza kuhangaika kwa waganga kahngaika sana na mwisho akampata mganga wa kweli akampa dawa na akashika mimba ndo mie nikazaliwa mtoto wa kirang...lkn alipewa sharti akijifungua anipeleke huko kwa mganga sema mpaka leo mama hajanipeleka...wakat huo mama yangu alikua anakunywa pombe yy pamoja na mume wake yan baba yangu hawakua wnajal din japo wote ni waislam.

    na baada ya kunizaa mie sasa muda wa kuzaa mtoto mwingine umefika tena matatizo yakaanza hapat mtoto akahangaika sana hospital wapi..akaenda kwa wagangaa wapi..ila yule mganga alimsahau hakurudi kwake tena ,

    mama alihangaikaa kwa miaka mingi sana mpaka mm nikamaliza shule ya msing ni sema baada ya kunizaa mm mama aliachana na pombe na akaanza kusal sala tano..so katka kuhangaika alikua anahangaika kwa waganga akachoka akarudi kusali na kufunga na kuomba ucku na mchana yan mama yangu ilifikia kipind alikua jacr sana alikua anatembea hata uku wa manane kwenda msikitin..

    baada ya miaka miwil ya kuachana na waganga na kurudi kwa mungu kusali kwa kwenda mblele hatimae mie niko 4m one akapata mimba na kujifungua mtoto lkn alikua amefia tumbon..mama alilia kupita kias mpaka akasema jaman msiende kumzika mbona bado anatoka damu huyu maana alitoka kachubuka yan km kaungua hv..niachen tu nilale naye kwan lzma kumzika? ila alizikwa

    lkn aliendelea kusal na kusal hatimae baada ya mwaka tena akajifungua watoto mapacha wakiume mmoja anaitwa hasan mwingine husen sasa wako darasa la nne..

    yan ukiingia hapo nyumban ni fujo kwenda mbele km unavojua mapacha tena.. sema mama sasa keshafunga kizaz kasema inatosha.anafuraha kila kukicha


    so ww mdada kila sehem kuna faida na hasara kwa waganga kuna faida na hasara lkn pia kwenye dn unatakiwa iman hasa siyo tu iman coz unataka mtoto lkn iman kwaa ujumla

    mie mtoto wa dawa sasa nina mtoto wa kike ama kalazmisha nimpeleke akakae na wajomba zake na coz najua mama anashida sana na watoto kuliko mie nimempata huwa naenda kumwangalia tu na kurud yan mwanangu anamwita bibi yake mama na babu yake baba kwasababu ya wale mapacha pale.

    mie namshukuru mungu cjapata tatizo hilo kabsaa na kizaz chepes balaah

    kila la her dada mungu atakusaidia.
    hlf mie nafikir ukianza kusal leo eti kwasababu tu unataka mtoto ni vigumu kujibiwa coz unasal kwasababu ya kupata mtoto na siyo sababu nyingine so inaweza kukuchukua hata miaka huko ndo upate jibu

    ReplyDelete
  5. KUSAL NDIO KWENYEWE SALI TU NDUGU YANGU MUNGU ATAKUSAIDIA IPO SIKU UTAONA MATUNDA YAKE
    MAMA JACK

    ReplyDelete
  6. Nakupa pole sana ndugu yangu kwa matatizo yalokupata. Kwa mtazamo wangu nakushauri uendelee na maombi kwani Mungu ndio muweza wa yote kwake hakuna gumu lisilowezekana. Imani yako ndio itakayokuponya, kwani hata ukienda kwenye maombi pasi wewe kuwa na imani huwezi kupokea uponyaji.

    Mrs. Lema

    ReplyDelete
  7. ngoja nikushauri mpendwa wangu, unajua hakuna kitu kizuri kama kuwa na imani, haswa ukimwamini Mungu,nakushauri wewe mng'ang'anie Mungu tu! mpe nafasi, na umwamini, usimchanganye mungu na mambo mengine, kama umeamua kumpa yeye nafasi basi mwache ashughurike, sasa wewe mara umeenda kwa mganga, mara umerudi kwa mchungaji, hivi unajua kama nuru na giza haviwezi kuwekwa pamoja? ni wazi kuwa mungu nae anakupima imani yako, mimi kwa imani yangu niliyo nayo, nakuomba mshikirie na kumwanini Mungu tu! basiiii, siwezi kukushauri kwenda kwa mganga hata kidogo, coz mimi sijawahi kwenda, na sijaweka imani yangu huko. huwa napenda sana kumwamini Mungu, tulia kwake tu, atafanya, na ninakuombea pia,
    halafu umri wako pia bado ni mdogo, ni mapema mno kukata tamaa, watu wanazaa wakiwa na miaka 40 na kuendelea sembuse wewe wa 2....? dont give up mpendwa.

    ReplyDelete
  8. daaah!!!!!!!!1pole sana my dada...nakushauri uende kwny maombi....km uko maeneo ya karibu na ubungo unaweza kwenda kwa mtumishi ANTHONY LUSEKELO..MZEE WA UPAKO...

    ReplyDelete
  9. pole sana dada yangu, kweli mtoto ni furaha na ni faraja kwa kila mwanadamu hasa unapofikia umri wa kuhitaji mtoto na ukampata, lakini inapotokea akakosekana inachanganya sana, inaumiza na inavunja moyo lakini naomba uendelee kumwamini Mungu naimani Mungu atakusaidia tu na muda si mrefu utapata watoto usinung'unike wala kukata tamaa ni kwamba muda wa Mungu bado haujafika hivyo endelea kumwamini Mungu naimani atakujalia tu na utapata mtoto, usijaribu kwenda kwa mganga kabisa ndugu yangu Mungu hachanganywi na kitu chochote amini kwamba Mungu hashindwi kukupa mtoto

    ReplyDelete
  10. naomba uangalie post ya www.u-turn utapata namba za watu watakaokusaidia, kuna watu walikuwa na hizo shida wanadai wamefanikiwa. nakushauri ujaribu kuwasiliana nao. kuna aina kama sita za namba za simu wametoa. nakutakiwa kila la heri

    ReplyDelete
  11. Pole,matatizo ya uzazi yapo na yanawasumbua wanawake wengi,hicho ni kitu cha kwanza unachopaswa kujua,heading ya ujumbe wako umesema mganga amesema umelogwa,mchungaji umefungwa,ndani ya ujumbe umesema umepima hospital unaoneka huna tatizo.
    Ushauri,nenda tena hospital,kuna madaktari wafuatao wanaweza kukusaidia,dr. Kapona,dr. Kamugisha-Muhimbili, Dr. Anna Purna-Regency, Dr. Shafiq-Agaghan.
    Kupima Ultra sound pekee haitoshi kujua kuwa wewe ni mzima,unapaswa kupima hormones pia,kuna hormones kuu tatu ambazo hupimwa wakati ukiwa kwenye period- nazo ni FSH,Prolactin na testerone-kwenye uzazi kuna mambo mengi sana,kama hormones hizi hazipo normal huwezi kupata mimba-haswa prolactin na FSH-(Follicl Stimulating Hormones) madaktari hao niliokueleza wanasaidia sana-pia upaswi kuwa na stress-jinsi nilivyokusoma hapo unaonekana akili na mawazo yako hayajatulia kabisa-stress zinafanya hormones kuwa juu na kusababisha ovulation kutotokea na hata periods zako kutotokea.

    Waganga sidhani kama wanasaidia,labda kama ni wachungaji au mashekh wakuombee na kukupa dawa itasaidi.

    USHAURI
    kwasasa pumzika,hakikisha huna stress,tulia kabisa ona kupata mtoto ni kitu cha kawaida,Muombe Mungu,then nenda kwa madaktari niliokutajia hapo. utafanikiwa tu.KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.Madaktari (haswa Anna Purna,Kapona na Shafiq).

    ALL THE BEST.

    ReplyDelete
  12. Umeshauriwa na wengi juu ya kumtegeme mungu kwenye matatizo yako, nami naungana nao mia kwa mia. Ila tatizo lako hata mi lilinikumba mtoto wangu wa kwanza nilimpata kwa kuhangaika sana ila ni baada ya kupata kile kipimo cha hospitali kinachicheki mirija na huyu wa pili wamepishana miaka 8. ila mimi nimehisi uzazi wangu ulikuwa mbali sana mana mpaka sasa situmii kinga yoyote.Ila tatizo hili linachangiwa sana na mawazo unapofanya tendo la ndoa unakuwa unawaza sana juu ya mimba mimba mimba jeitaingia?, na endapo hedhi intokea unakuwa huna raha kabisa, yote hii inakuletea stress ambazo zinaharibu hormones za mwili.nakushauri mlilie mungu mwambie wewe kama binadamu umeshindwa,unamwachia yeye afanye kazi yake,Nenda kwa ma dr wataalamu watakushauri hata jinsi ya kukutana na mr n.k Nawe tafuta namna ya kujisahaulisha kabisa kama uko kwenye hitaji la mimba,tafuta activities zitakazo kusahaulisha waweza hata ku adopt mtoto mdogo wa miezi 6 ukawa unamlea.mimba inaweza ikaingia bila habari pia hawa watoto wa ku adopt wanaleta sana baraka.pole sana dada

    ReplyDelete
  13. Pole dada mwenye tatizo, naomba email yako nikutumie njia ya kufuata utapata mimba. tuma sms 0755394223

    ReplyDelete