Thursday, July 22, 2010

MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI - (BINADAMU HATUNA HURUMA HATA KIDOGO)

Imenisikitisha sana hii, lakini ndio hivyo tena, hawa wenzetu wakikukamata wala hawakuachi na wala hawana huruma.
hii imetokea huko gongolamboto, usiku wa kuamkia leo, mwizi huyu ameuwawa kwa kuchomwa moto, lo!
 story nilizopata jujuu ni kwamba, watu walikuwa wakikimbiza mwizi, mwingine tu! bahat mbaya yule mwizi aliwachenga  na kukimbilia sehemu zingine, (akawapotea) sasa wakat wale watu wamekata tamaa wanarudi, wakasikia kelele mtu analia, anaomba msaada, kama mtu anaekabwa hivi, wakafata kelele zilipo wakamkuta huyu (kwenye picha) akimkaba dereva wa piki piki na wamekuta amemchoma bisi bisi, ila huyo dereva nae alikuwa na ubavu kidgogo, basi walichokifanya waliwahi kumkamata mwizi huyu na hasira za yule mwizi wao wa kwanza zikaishia kwake,
inasemekana baada ya hapo walimwambia aseme ametumwa na nani, (kabla hawajamkaanga) akasema bosi wao anaishi bagamoyo, akawapa na namba za simu, basi wale watu wa hasira kali, walimkamata, wakampa kichapo, haikutosha wakaamua kumkaanga Binadamu mwenzao kama kama hivyo,
nimeona asubuhi hii, du! jamaa kaiva ile mbaya, (binadamu sio kitu jamani lo!) ila ndio waache jamani mbona hawajifunzi??????? ss sijui nae tuseme akalale pema wapi ah!
lakini sasa, kuua kwa kujichukulia sheri mkononi hakufai, kwanza ni dhambi, ss kama walipata namba za huyo tajiri si ni bora wangembananisha awapeleke ili wakamjuwe anaefanya hivyo? inasikitisha sana,
yani mtu unamwagia mwenzio mafuta, unachukuwa kiberiti, unamuwasha, da! mi naona bora wangemtandika mbakora za kufa mtu, wamjeruhi tu! ili yale maumivu yamfundishe, kuliko kuua,No comments:

Post a Comment