Monday, July 12, 2010

RAFIKI YANGU ANAAMBUKIZA WATU UKIMWI KWA MAKUSUDI, NIMFANYAJE? AU NIWAAMBIE UKWELI?

Habari dada, nina rafiki yangu (msichna kama mimi) ambae tumedumu nae kwa muda mrefu sana, ni rafiki yangu wa muda mrefu, ila tunatofautiana kwenye tabia, yeye anapenda sana wanaume, na hawezi kuwa na mwanaume mmoja, hawezi kabisa, nimeongea nae hadi nimekata tamaa,

Tunaishi nae hostel, sote ni wanachuo, sasa kuna siku watu wa ushauri nasaha walikuja hostel kwetu, wakatupa semina sana, hadi tukashawishika kupima, na tukakubali kupata majibu, yangu yalikuwa safi, ila ya mwenzangu hayakuwa mazuri,

Lakini alipotoka kuchukuwa majibu yake akaniambia mazuri, kumbe alikuwa ananificha, sasa kuna siku aliamua kuniweka wazi juu ya afya yake, na kuniambia kuwa ameathirika, niliumia sana as if ni mimi, lakini niliendelea kumsihi inabidi atulie, ikiwezekana aweke akili yake kwenye kusoma zaidi aachane na mambo ya wanume, na haimaanishi kuwa nao ni kufa, mwanzoni alinisikia,

Sasa kinachonishangaza, baada ya miezi sita tabia yake ikarudia, tena naona this time imekuwa mara tano zaidi, haingii darasani, na ana wanaume wengi sana. Mbaya zaidi anasema yeye hatumiagi kinga. Na ananishangaa mimi nilie na mwanaume mmoja

Kinachoniumiza zaidi, amempata kaka mmoja tunasoma nae, na ameniambia bado hawajatembea nae, na atahakikisha anatembea nae, sasa mimi inaniuma sana, asijekumuua kaka wa watu bure, sasa hivi ni nusu ya changu doa, pombe anakunywa sana, ametoa mimba sana, na anasema yey e hataki kinga yeyote,

Nimuwahi Yule kaka nimuweke wazi juu ya hili? Na uhakika asilimia 90% kuwa hajatembea nae, maana anatabia yakunieleza kila kitu

6 comments:

 1. dada, huwezi jua nikwanini Mungu alikufanya ukalijua hilo

  Plz okoa hayo maisha ya huyo kijana,plz mwambie au hata unaweza mtumia text msg au hata kuwaambia marafiki zake wamwamibie, au hata kama ni muumini nenda msikitini au kanisani anaposali huyo kijana tafuta kiongozi mwambie ili ampe huo ujumbe huyo kijana

  naamini vyuo karibu vyote tz vina sehemu za kuambudia unaweza tumia njia hiyo pia

  ReplyDelete
 2. jamani wewe dada please muwahi huyo kaka upesi mwambie ukweli woote usimfiche mungu wangu huyu dada mbona watakufa wengi jamani kua mkweli kama dada

  ReplyDelete
 3. pls wewe dada fanya haraka hata sasa ivi nenda kamuambie ukweli uokoe maisha ya huyo kaka, Mungu amekuweka wewe uyajue hayo yote ili uokoe maisha ya wengi. usijiulize ulize mara mbili mbili chukua hatua sasa ya ujasiri ukamueleze.

  ReplyDelete
 4. aunt bora umueleze ukweli huyo kaka na pia jaribu kumuonya huyo shaga yako na umwambie asipoacha utatangaza kwa watu kuhusu tabia yake,mimi pia nilikuwa na shoga muhuni kama huyo nimeachana nae sasa hivi kwa tabia yake na pia na wasiwasi sijui kama nae hajaupata.

  ReplyDelete
 5. plz nitumie number ya huyo dogo kwa hii mail ntampigia simu nimshauri na kumwomba aachane na huyo dada, ntampa ushauri kwa utaalamu

  judycob@gmail.com

  plz fanya hivyo haraka

  ReplyDelete
 6. mfuate huyu kaka mwambie usitumie m2 maana utakuwa umevujisha siri ya rafiki yako jivishe ujasili mfuate mwambie ukweli


  sphmkumbo@gmail.com

  ReplyDelete