Sunday, January 15, 2012

MUME WANGU HATAKI NIFANYE KAZI YEYOTE


Mume wangu hataki ni fanye kazi, wala baishara yeyote ile,  ananihudumia kweli, lakini mimi sipendi kuwa tegemez, napenda nifatute pesa kwa jasho langu,

Yeye anataka niwe mtu wa ndani tu! Yani hataki niajiliwe wala nijiajiri, anahudumia hadi familia yangu, chochote ntakachosema napewa, lakini nawaza siku tukiachana, kwa namna yeyote ile, iwe by divorce of death, how could I leave ??? si nitapata tabu jamani3 comments:

 1. Dada, mi nikupe uzoefu wangu, mimi ni mjane sasa mume wangu alifariki mwezi wa 10/9/2009. Alikuwa mume anayejua wajibu wake kwangu na kwa watoto wetu ial alikuwa akinikataza kwenda kazini, amenikuta na kazi yangu na kuna wakati yeye akitafuta kazi kimshahara changu ndo kilitusogeza sogeza, alipopata kazi akawa kila siku ni wimbo mye niache kazi maana haoni kwanini nahangaika na kamshahara kadogo, yeye kila siku ndo ananipa nauli. Nikagoma, kwa nguvu zote nikaendela na kazi ingawa kwa masimango hivyo hivyo, ghafla siku iso na jina majambazi wakatuvamia wakampiga risasi akafa hapo hapo, mie nina kitoto cha miezi 7, usisikie nililia machozi yote nikamaliza na hayakutosha..... Nikarejea kazini, kidogo hicho hicho ndio kinanilisha leo na wanangu wawili, ningeacha kazi leo ningekuwa mgeni wa nani miye..... hatta kama angeniachia mabilioni bado yangeisha si uanjua kutoa tu bial kuingiza. Kaa chini na mumeo mueleze kwa upendo an upole madhara ya wewe kutofanya kazi, yapo mengi hilo ni mojawapo tu.
  Kado

  ReplyDelete
 2. huyu mdada amenisikitisha yaani anashida kamayangu mpaka nasoma naona kama mimi ndie niliyetuma post hii .pole mwenzangu mimi wangu nimesha mbembeleza sana mpaka kwa ndugu wote wamembembeleza hataki kusikia kabisa sijui ni lugha gani nitumie ili anielewe.

  ReplyDelete
 3. mdogo wangu kazi ni mume wa kwanza ebu jaribu kutafuta kazi jitahidi sana kutafuta kazi.

  ReplyDelete