Friday, September 9, 2011

MTOTO WA MUME WANGU ANANIFANYA NITAMANI KUIKIMBIA NYUMBA YANGU- NISAIDIENI

Mimi ni mama niliolewa miaka mingi iliyopita, nilimkuta mume wangu ana mtoto mmoja ambae ni mdogo sana, mama yake alikuwa amefariki ndio nikaolewa mimi,
Nilimlea Yule mtoto kama wa kwangu mwenyewe, nilimuhudumia na kumpa mapenzi yote ya mama, nami mungu akanijalia nikapata mtoto mmoja wa kiume,

tatizo ni kwamba huyu mtoto wa mume wanguameshakuwa  yuko form four sasa hivi,lakini nilianza kumlea toka akiwa na miaka mitano,
Juzijuzi hapa nilihisi ni mjamzito, nikampima nikakuta ni kweli, iliniuma sana kwakuwa bado ni bint mdogo istoshe hata shule bado hajamaliza, nilimsema sana, cha ajabu baba yake toka kipindi hicho hadi leo hii hajasema chochote na binti yake kuhusu huo ujauzito, mbaya zaidi anamtetea kwa kila kitu kias kwamba Yule mtoto anaweza kunijibu vile anavyotaka, nikijaribu kumuonya anakuja juu sana, na baba yake anamtetea,

Natamani hata kuikimbia nyumba yangu, maana sielewi itakuwa hivi hadi lini, mtoto amekuwa mjeuri kupita maelezo, tena anasema kwanini wewe unifatilie fatilie wakati baba yangu anajua na hajasema lolote juu ya hili, wewe ndio una uchungu sana???
Sasa jamani mimi kama mimi sijui nifanye nini kabisa, tunaishi kama mtu na mke mwenzie yani ukikuta ananijibisha as if ni mdogo wake, naombeni  ushauri, nifanye nini mwenzenu??



9 comments:

  1. samahani kwa ninachokiandika.na mungu apishie mbali,isije ikawa aliempa mimba ni huyo baba mtu.inashangaza mtoto wako awe na mimba huyo baba asiseme kitu.malezi gani hayo?jaribu kuchunguza

    ReplyDelete
  2. dada ulieleta hiii huu mkasa pole sana mimi kitu ninachokushauri kwanza mtangulize mungu mimi sijui wewe ni dini gani omba sana kwa muumba wako ailinde ndoa yako hayo ndio yanaitwa majaribu najua roho inakuuma sana haswa ukizingati ukianza kumlelea tangu akiwa mdogo nakumpa mapenzi yote kama mzazi wake sasa usimchukie tena kwa hali aliyokuwanaye mimba sio mchezo anawezakukutukana lakini wale wewe usimchukulie hasira kuwa mpole naye maana kama nimimba ndiyo hivyo ameshapata wewe kaanaye kwa upole huku ukimwombea mungu ajifungue salama usimseme sana akaja akaamua kujiua maana usinajua hasira za mimba usimwongeleshe tena kuhusu mimba yake maana kama baba mtu hasemi kitu wewe unaangaika ya nini labda baba yake anaona akimsema sana anweza akamsababishia makubwa mtu mwenye mimba uwezikumgombeza au kumsema unatakiwa uende naye taratibu hata kama amefanya kosa wewe siulibeba mimba uajua jinsi ilivyo huyu binti mwache na mimba yake kwani amechezea bahati yake amepata bahati yakwenda secondary yeye anaichezea wengine wanatafuta hiyobahati hawaipati pole dada na matatizo usiachekumwomba mungu kwani yeye hashindwi na jambo lolote

    ReplyDelete
  3. iasije kuwa miba ni ya baba yake au umeshachunguza mimba ni ya nani.

    ReplyDelete
  4. pole mumy... yawezekana mimba ni ya baba yake, haiwezekani kama mzazi asikasirike wala kumsema mwanae.. any way tumwachei mungu.. Cha muhimu cha kufanya wewe usmwongeleshe... akija akikusalimia sawa, asipokusalimia sawa.. yaani namaanisha kati yenu ibaki salamu tu... yeye mwenyewe atajistukia,... na akipata tatizo atakukimbilia wewe... kashajua wanaume anajiona amekuwa. so we ni kuwa mvumilivu na kuheshimu ndoa yako na kuiweka familia yako katika hali nzuri. Dada watoto wakambo wanakera ni wachache san wanafadhila na kukumbuka mapenzi wanayopewa na mama au baba zao wakambo.. so kuwa mvumilivu wewe usiondoke kwenye ndoa yako kisa yeye... unless otherwise labda ukigundua kuwa hiyo mimba ni ya baba yake ila unatakiwa uwe makini.. ni vigumu sana kumwelewa huyo baba kwa kweli...

    ReplyDelete
  5. Kama kuna kitu kinatutesa sie wanawake ni kuwapenda watu wengine kuliko sisi wenyewe,sjui ni vile ni walezi wa dunia.Jipende mwenyewe,nafsi yako haitakukosea shukurani.Ulivyompenda huyo mtoto inatosha na ulivyomheshimu huyo baba mtu kwa kumlelea mwanae inatosha.Rudisha mapenzi kwa nafsi yako,mpende mume wako kama kawaida,mpende mwanao maana hao ndio watu wa muhimu kwako,huyo binti atashiba jeuri yake.Na kama ukimya wa baba yake ndio unamtia kiburi basi mwonyeshe ulivyomlea inatosha na wala hutomgusa labda aonae umuhimu wako kwake.Umetenda wema wako usingoje shukurani.Onyesha mapenzi kwa mwanao kuliko muda mwingine wowote,mwanao hatakukosea shukurani.Kwa hiyo mshukuru Mungu hilo limetokea mapema maana imekupa picha ya mbeleni,haya! ndio umeyagawa mapenzi kwa mwanao na yeye pasu kwa pasu halafu utu uzimani angekugeuka......jipende,endelea na maisha yako.Kujipenda ni kuthamini vile ulivyonavyo kuliko vya wengine.

    ReplyDelete
  6. Naungana na mtoa mada hapo juu. Kama tayari ana mimba kumsema kunasaidia nini? Ulipaswa kumkanya asipate hiyo mimba. Alafu umechanganya mada mbili hapa; kwanza ya mimba; pili ya nyie kuto kuelewana. Sasa uoni kama nyie hamuelewani haina maana kwa wewe kumgombeza ukizingatia si mtoto wako. Mama yake yuko wapi?

    Achana na watoto wa watu mama utaja jiletea matatizo bure maana watoto wengine hao waliodekezwa utamsema achukue vidonge anywe uishie segerea. Lea watoto wako atakukumbuka dunia ikimfunza.

    ReplyDelete
  7. Moja, mimba ndio inamfanya musielewane. Mbili, BABA yake kaona haisaidi tena kumsema sasa hivi, maana mumechelewa, na anaonabora kumsappoti tu mtoto wake,ndio kilichobaki kwa hali alionayo sio vizuri kuendeleza tu kumsema kila siku. Tatu, yawezekana labda baba yake anamuonelea huruma mtoto wake kwa vile mama yake huyo mtoto kafariki, na anakuona wewe haumsappoti kwama inavotakiwa.

    Hapo kuna sababu nyingi nazani, yawezekana pia mimba kapewa na baba yake. chunguza kwanza mama,

    ReplyDelete
  8. Kwanza pole sana, kwa swala kama hilo usifanye pupa kupanic. chunguza kwanza aliyempa mimba ni nani,

    Ni mimi
    MC CHABASA............

    ReplyDelete
  9. pole sana fanya uchunguzi mimba kampa nani isijeikawa babake mana wazazi wa siku hizi kulala na binti yake jambo la kawaida mi najua mngekaa wazazi wote mkashauriana mfanyeje halafu bint aitwe aulizwe ni nani kampa ujauzito ikiwezekana ashtakiwe kwa sababu amempa mwanafunzi mimba baba anakua mkali inahu kikulacho kiunguoni mwako

    ReplyDelete