Sunday, September 11, 2011

MZAZI, MUDA GANI UNAKAA NA WATOTO WAKO NYUMBANI??
Swali hili ni la msingi sana kwa mzazi anaejali mtoto wake, wazazi tumekuwa busy mno, kiasi kwamba tunawasahau watoto wetu kabisa, kuna kipindi kiliwahi kunikuta mimi nikitoka saa 12 naenda kazini naacha wamelala, nikitoka kazini naenda chuo, narudi home saa mbili na nusu au saa tatu nakuta wamelala, yani ilinipa wakati mgumu sana,sasa naamini hii inatokea na kwa wengine pia kutokana na shughuri tulizonazo, muda umekuwa upo pale pale ila majukumu ndio yametuzidi


Nawakumbusha tu! Wazazi wenzangu siku tunazokuwa na muda, lets say ni weekend, tukumbuke kuwa karibu nao sana, tuwadadisi kiundani sana kujua mawazo yao, michezo yao na hata mahusiano nao na dada zao (mahousegilr) tuangalie homework zao, tukague madaftari yao, kwa kufanya hivi tutagundua vitu vingi sana, ambavyo wamejitahidi, au wanahitaji msaada zaidi


 nilichogundua kwao hasa kwa hiki kipindi ambacho niko rikizo ni kwamba wanapenda sana kila kitu niwafanyie mimi, mfano wakiamka tu! wanakuja chumbani kwangu moja kwa moja, na kunitaka mimi niwaandae, na sio dada tena, so namwambia dada endela na kazi zingine, ngoja niwahudumie mimi. basi wanafurahi sana, nikimaliza kuwapa chai, wananiambia mama utupeleke hadi shuleni kwetu, kwakuwa sio mbali na nyumbani, basi nawasindikiza wananipa mabegi yao niwabee, yani wanaenjoy kupita kiasi, hata kwa kuwa namimi kwa dakika chache tu!


Tusiwaamini sana wadada wa kazi, coz wao sio wazazi, ni wachache sana wanaofanya exactly like mother, but mmmmm… bado kama mzazi especially mama, unahitaji kuwa karibu na mtoto sana, ukiwa na mtoto ambae sio muoga atakufanya ujue vitu vingi vinavyojiri nyumbani wakati haupo, mfano tracy wangu, kila kinachojiri nyumbani hasahau,  ukirudi tu! Kama akiwa macho anakuelezea, naanza kumfanya rafiki yangu tangu akiwa mdogo, ili asiniogope bali aniheshimu  na awe wazi kwangu, maana kumkaripia sana kunampotezea confidence kabisa, anahisi kila atakachofanya atafokewa, so nivizur sana kusoma tabia za watoto wetu INAPOBIDI KUWA MKALI, KASIRIKA NA MTOTO AJUE NIMEMUUDHI MAMA AMEKASIRIKA, LAKINI ISIWE NONGWA, KILA SAA UNAKASIRIKA MTOTO ATAKUCHUKIA


Weekend hii nimekumbuka kugusia watoto, naona limekuwa ni tatizo kwa baadhi ya wamama,  siku ukipata nafasi, andaa chakula cha watoto wako wewe mama, dada nae apumzike, angalia walipohifadhiwa nguo zao za kushindia, angaliwa walipolala kila siku, kagua kabla hujalala,  je vyandarua vyao ni salama? Kagua kucha zao kila weekend, kata ziwe fupi, yani atleast uwe na hata nusu siku kwa ajili yao,Kweli nawaambia mtoto hujiskia fahari sana anapokuwa na wazazi wake, baba au mama au wote, japo watoto wengi wameegemea sana kwa mama, hawataki utoke, ukitembea nao wanajiskia raha sana,

 
KWENU WAZAZI NATAMBUWA MNAFAHAMU WAJIBU WENU KWA WATOTO,  BUT WENGI WENU MNAJISAHAU SANA KUTOKANA NA SHUGHURI ZA KILA SIKU, NAJARIBU KUWAKUMBUSHA TU,  JINSI TUNAVYOLEA WATOTO WETU, NDIVYO WATAKAVYOKUWA KUWA,

KIKUBWA NA CHA MSINGI, PAMOJA NA UBUSY TULIONAO TUSISAHAU KUWAOMBEA KILA SIKU, ILI MUNGU AENDELEE KUWALINDA KWA KILA KITU

4 comments:

 1. watoto ni wako? aisee hongera sana

  ReplyDelete
 2. waooooo, taifa la kesho, watoto wazuri kabisa, wamependeza sana, ila trace anaonekana charming kama mama yake, nawapenda sana watotot mapacha, niombee namimi nipate

  ReplyDelete
 3. mh! huyo trace alivyo bishooo, mh! haya mama, hongera kwa kukuza

  ReplyDelete
 4. kweli kabis, tumekuwa busy sana na kazi, tuwakumbuke watoto
  asante kwa kutukumbusha violet, nakupenda sana

  ReplyDelete