Saturday, April 9, 2011

MWILI WANGU UNATOA HARUFU KALI SANA , NINANUKA MASAA YOTE, NAOMBENI USHAURI WENU NITUMIE NINI

Mambo Dada, please usirushe email yangu,
Mimi niko hapa dar, nina miaka 25, tatizo langu ni kwamba ninatoa harufu kali sana, mwili wote, jasho langu lina nunuka sana, kwapa, hata sehemu za siri nanuka pia,  hhali hii inaniumiza sana, inanitesa na kuninyima raha, nakosa kujiamini,

Niliwahi kwenda hospitali, wakafanyia check-up, wakasema nikazane usafi tu, ndio maumbile yangu, lakini sasa mbona hali hiizamani haikuwepo??? Ni miaka mitatu sasa tangu niwe hivi, unakuta hadi nikikaa na watu nahisis wananisema mimi ninavyonuka, kwenye pochi yangu hukos perfume au deodorant za aina 4, kila mara niko washroom najipulizia, hali hii ni ngumu, kwa usafi mimi ni msafi sana, sielezi ni nini hiki,
Nilikuwa na mpenzi wangu mmoja hapa hapa dar, tulidumu kwenye mahusiano miezi mitatu tu! Yeye alikuwa ni msafi sana, sasa harufu yangu ika wa inamkera, nakumbuka kuna siku aliniambia bwana nakupenda, ila harufu yako mimi mmm, hapana siwezi kuvumilia,  nililia sana, sometimes hat akitandani alikuwa akijifunika shuka lake,  finally tukaja kuachana,  alinikwepasana, nikipiga sim hapokei, mara nikasikia anataka kuoa,

Please naombeni ushauri wenu jamani, nisaidieni mwanamke mwenzenu nakosa raha kabisa, muda mwingine huwa nalia peke yangu, serious naombeni msaada wenu, maana perfume zimenichosha sasa, nimetumia manukato yote, sasa nona yamenizowea harufu iko pale pale, sometimes huwa nahisi nimerogwa, nikaa na watu nahisi wote wananisema mimi, na wengine niliwahi kuwasikia kabisa wakinitaja na jina langu, inaniuma sana, bora ingeonekana ni ugonjwa niutibu kwa gharama yeyote,

Please dada usirushe email yangu.



10 comments:

  1. hi dada mzuri usilie mpenzi wangu, hiyo hali kama hukuzaliwa nayo kuna tatizo gani? Jambo la kwanza maganda ya ndimu ni dawa sana, ukisha kamua ganda la ndimu lile ganga la ndimu usilitupe asubuhi unajisugua nalo kwapani, ndiyo deodorant yako asubuhi na jioni, na pia maji ya kuoshea mchele ukishaosha mchele, yake maji yake jioshee nayo sehemu zile zinazotoa harufu na pia nenda kwenye maombi ya kufunguliwa kama hiyo hali hukuzaliwa nayo na ni miaka miatatu tuu iliyopita ujue something is hapen usilie usihuzunike jaribu njia hizo mbili maji ya mchele na maganda ya ndimu na njia ya tatu maombi sehemu za maombi siku hizi ziko nyingi kama uko Dar nenda kwa mzee salu Buguruni ukifanikiwa njia hizo tatu lete shehuda hapo tujue mungu akubariki.

    ReplyDelete
  2. Pengine kuna organ moja mwilini mwako imevamiwa na bacteria au virus, na usababisha hiyo harusu. Kuna time ingine madokta hawawezi kutambua haraka haraka, matatizo ya binadam. Inabdi uende kwa madokta wakubwa, wenye ujuzi zaidi na zaidi. Husichoke. wapime mkojo na damu, nk. Na hata mganga wa jadi husiache kwenda hili mradi upate dawa ikuponeshe tu.

    Na kama sio tatizo la organ mwilini mwako, basi inawezekana kuna vyakula flani ukila, vinakuzuru na usababisha utoe harufu mbaya sana.


    Kwa mfano mie nikinywa maziwa na vyama najiskia nanuka sana, hata nikitumia manukato haisaidi. Hivi siku hizi sili nyama na sinywi maziwa siku za weekdays, maana kazini kutoa harufu noma.

    Na nina rafiki yangu mmoja, akila vitunguu, au mayai, ananuka kama kaoza, anasemaga na akila vitu hivo ujifungia ndani siku 2, maana mmm.

    Jaribu kufanya utafiti kipi ninakuzuru, mfano, unaweza kula chakula kimoja tu kwa siku 2, ili uone kama utatoa harufu mbaya, alafu unaenda next food. usichanganye vyakula.

    Pengine hapo zamani ulikuwa hauli vyakula mchanganyiko. Na watu wanaoishi mijini na nchi zilizo endelea kama ulaya wananuka zaidi maana wanakula vyakula mchanyanyiko, na vingine vya makopo. Ndio maana wazungu unuka kwa sababu vyakula wanayokula vya kuchanganya changanya mno. Nakutakia masharibu mema

    ReplyDelete
  3. pole sana mdogo wangu kwahayo yanayokusibu kila jambo lina sababu yake sisemi umelogwa la hasha kitu chakufanya mtangulize Mungu kwa haya matatizo kwani hakuna linalomshinda yeye piga magoti mlilie Mungu wako kwani anaona unavyotaabika na kukosa raha ya maisha kwa ajili ya hali hiyo hakika atakusikia na hali hiyo itakwisha kwa uwezo wake kwani hakuna linalomshinda yeye ni hayo tu wala usisononeke sana na usikate tamaa yuko yeye atakusikia kilio chako na matatizo yataisha bora tu umwamini na kumtegemea na kuomba kwa bidii

    ReplyDelete
  4. jaribu ku google.kuangalia ufumbuzi.nasikia kuna ugonjwa fulani unaitwa fish,jina la pili nimelisahau.unakuwa unanuka hata upulize nini,harufu haiondoki.ila nahisi ipo dawa ya hilo tatizo.au huenda tatizo lipo ndani ya mwili wako na sio nje.pole sana inasikitisha kwa kukosa raha kwenye tatizo ambalo hujui ufumbuzi wake

    ReplyDelete
  5. jaribu dada kwenye website ya www.jamiiforums.com,kwenye jf doctor,kule kuna wataalam watakusaidia kimawazo

    ReplyDelete
  6. Nimesoma email yako kwakweli imenisikitisha!So, i found this article which i hope will be helpful for you, jamani pole sana!The link is http://www.healthblurbs.com/cause-for-abnormal-strong-fishy-body-odor-and-trimethylaminuria-diet-plus-natural-smell-remedy/

    ReplyDelete
  7. pole sana dada labda nijaribu kukushauri jaribu kuwa unajisugulia ndimu mwili mzima kabla ya kukoga asubuhi na pia kuwaunafanya hivo mara mbili asubuhi na usiku kabla ya kulala mwili mzima kipande cha ndimu bila ya kumenya ganda na sehemu za siri jaribu kuona dactari pengine unaugongwa ambao unaweza kupata kwa njia ya kujamiiyana pole sana jaribu hiyo ya ndimu inawasaidia sana watu wenye kikwapa utapona kama utafatilia bila kuona uvivu mungu atakusaidia dada yangu utapona

    ReplyDelete
  8. Inawezekana umelogwa maana kama haukuwa hivyo zamani nina mashaka. Je umeshawahi tembea na mume wa mtu? Maana wanawake wengine hawakawii kukuendea kwa mganga unuke mumewe akutose. Anyway, tafuta mchungaji akuomee na wewe mwenyewe omba sana. Mimi nina imani umelogwa kwa sababu kunuka jasho hakuji ukubwani

    ReplyDelete
  9. chunguza vyakula unavyokula huwa baadhi vinawasababisha jasho kunuka husun vumba kama unakunywa sana supu ya samaki,vitunguu thom,mayai,maziwa nyama na spices zikiwa nyingi pia husababisha jasho kunuka

    ReplyDelete
  10. Naona mwone docta wa alergy, labda kuna vyakula vinavyokudhuru we bila kujua, pili tumia maji yalitokana na ukoko wa ugali uogee waweza ukawa dawa. songa ugali uungue kidogo sufuria jaza maji then ule ukoko ukishabanduka wote weka vyote menye ndoo nenda kaogee

    ReplyDelete