Wednesday, April 27, 2011

RAFIKI WA MUME WANGU ANANITAKA- NA MKEWE NI RAFIKI YANGU SANA- NIMWAMBIE?

nisaidieni jamani,  kuna baba mmoja ni jirani yetu, ni rafiki sana na mume wangu, wanashirikiana mambo mengi sana, na karibu kila weekend huwa wako pamoja, urafiki wao umefanya mimi na mkewe kuwa marafiki wakubwa, mkewe ananipenda sana,
ninachoshangaa Yule baba anakuja kwa speed ya ajabu, sms kibao, zikiingia tu! Huwa nadelete moja kwa moja, nahofia mume wangu asizione, niliwahi muuliza namba yangu kapata wapi, akasema kachukuwa kwenye simu ya mkewe, nilimfokea  sana, na nilimtishia kuwa nitamwambia mkewe, lakini hakomi  na wala haogopi, kusema kweli hadi sa sa mume wangu sijamwambia, maana mh! Patachimbika,
sasa nahofia siku Yule mama kwa bahat mbaya akipekuwa simu ya mumewe na kukuta sms anazonitumia za mapenzi itakuwaje?? Na nikimwambia kwa sasa ili kujikinga na hatari hiyo atachukuliaje,  najiuliza nimwambie mume wangu au mkewe, au niendelee kuwa kimya,
msaaadaaaa please

6 comments:

 1. WEWE USIWE MJINGA, MWAMBIE MUMEO KWANZA SIKILIZA ATAKWAMBIA NINI, BAADA YA MAJIBU YA MUMEO HAPO NDIPO UTAKAAAMUA KUMUITA MKE WA RAFIKI YAKE MUMEO NA KUMWAMBIA UKIWA WEWE NA MUME WAKO, UKINYAMAZA INAONEKANA UPO FIFTY FIFTY SO BETTER UFANYE HIVYO

  ReplyDelete
 2. Mwambie mumeo pls. Usichukulie easy kitu km hiki, itakuja kuku-cost baadae, kitu kdg kabisa kitapoeza uaminifu wako wote kwa mumeo na kwa rafiki yako pia. Tena fanya fasta mwambie mumeo kabla haijawa mbaya.. Wanaume wengine bwana ni migumegume kajisemea Hadija Kopa!

  ReplyDelete
 3. Mwambie mumeo shost! kama unavyosema mkewe anaweza kukuta msg hapo utakuwa huna la kujitetea. Unaogopa nini? kwani huyo ni ndugu wa mumeo? si just rafiki, kwanza huyo si rafiki mzuri, hana adabu hata kidogo. Mwambie mumeo shosti!

  ReplyDelete
 4. wewe ni mwanamke kuwa na msimamo, kwani huyo mwanaume unataka kumfichia siri ili nini? usipokua makini yatakupata ya kukupata na utajuta maishani ni bora umwambie mumeo mapema kabla hayajawa makubwa. labda utuambie na wewe unamtaka huyo mwanaume!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 5. Mimi naona mama unaingia kwenye mtego. Kama ni rafiki wa mumeo yawezekana wamepanga na mumeo wakutest kuona uaminifu wako. Wanaume wengine ni washenzi. Sasa unavyochelewa kumwambia mumeo basi naye ana conclude kuwa wife ni cheap na kukuona bado unatafakari ombi la rafiki yake! Maana unavyosema hana woga natia shaka huo ni mtego dear!

  ReplyDelete
 6. kama unampenda mumeo ungemuambia

  ReplyDelete