Habari ya kazi Voiet. Mimi ni kijana wa kiume, i have 18yrs, hadi
sasa naishi Zanzibar katika wilaya ya Mjini. Nilikua nikitembelea kwa
siku nyingi katika blogi zako zinazohusiana na suala zima la MAPENZI, katika utafiti wangu juu ya suala hilo, nimefaidika na mambo mengi sana yanayohusu MAPENZI, kwa
mfano, jinsi ya kumpata mwanamke akupendae, pia vipi utaweza kuishi
kuishi nae, na vipi munaweza kuboresha na kudumisha mapenzi yenu na
mengineyo. Nashkuru sana nimefaidika kwa kiasi kikubwa sana kupitia BLOG
zakoAnt Voilet.
Ila lakini, pamoja na yote hayo,
niliyoyapata kupitia BLOG zako bado mimi nina tatizo moja tu ambalo
linanikwaza katika MAPENZI yote kwa ujumla, kwa kutumia TAALUMA ambayo
nimeipata kupitia BLOG zako, nahisi nikitu MUHIMU sana katika MAPENZI
pia inaweza ikapelekea kuachana na MPENZI wangu na ni kitu ambacho mimi
sijakipanga maishani mwangu kumsaliti yeye kwani NAMPENDA.
Tatizo langu Ant Voilet ni kwamba mimi hadi sasa bado sijajua jinsi
gani ya KUMBEMBELEZA MPENZI wangu, kwani yeye kila siku ananmbia
NIMBEMBELEZE wakati wa usku asa na mimi sijui kwa sababu mimi nilitaka
kuyajua MAPENZI kabla ya kumpata MPENZI,aidha naliyasoma kwanza yakoje
halafu ndo nikaingia,bali yeye anambia nimwambie MANENO MAZURI YA MAPENZI YENYE KUMLIWAZA WAKATI WA USIKU ANAPOTAKA KULALA, husema
yeye hapati usingizi na mimi pia nimeshachoka kumdanganya, kwaiyo
nakuomba Ant Voilet kwa ROHO YA UNYONGE na nainamisha kichwa changu
chini na napinda magoti yangu chini na nainua mikono yangu juu kupokea
MSAADA wako kwani nakuomba unisadie juu ya hilo kwani NAMPENDA ZAIDI YA
ANAVYOFIKRIA na sitaki nimpoteze. Pia nimeshamuahidi Mungu ikiwa
hatochukua roho ztu nitakuja kufunga nae NDOA.
Ni matumaini yangu yakua ombi limefanikiwa na litajibiwa.
Ant Voilet ndio tumaini langu la pekee.
INASIKITISHA NDUGU YANGU KUUDHIHIRISHIA UMMA KWAMBA SASA UNAVUNJA AMRI YA SITTA HADHARANI. SI UFAKHARI.MUDA MUAFAKA UKIFIKA UTAJUA NAMNA YA KUM'BEMBELEZA MWANDANI WA UKWELI NA SI HUYU '''FAKE''' ULIYENAYE KWANI KESHAKUONA KWAMBA U MWANAFUNZI KATIKA FANNI NDIO MAANA ANAKUPELEKESHA PUTA KWA KUKUTAKA UM'BEMBELEZE.
ReplyDeleteKijana mbona bado wewe ni mdogo sana kuhangaika na mambo hayo katika hali hiyo?Vipi shule umemaliza masomo?Naona kama unataka kujipatia vidonda vya tumbo kwa kwa kuparamia mapenzi kihivyo.Jambo la kubembeleza mapenzi halina ujuzi wala elimu yoyote.Ni jinsi tu unavyoweza kujituma mwenyewe.Unapata shida ya jambo hilo kwa sababu wewe bado ni mdogo sana licha ya kuwa na umri wa 18 ambayo wengi hujidanganya kuwa wamkuwa watu wazima.Usikonde kwa mambo kama hayo.
ReplyDeletempe nyama ya ulimi
ReplyDeletemimi ni msichana mwenye miaka 32,nimezaliwa kilimanjaro.nina elimu ya chuo kikuu.nimeajiriwa serikalini.umbo langu ni mfupi, mweupe,si mnene wala c mwembamba.natafuta mume mwenye mapezi ya dhat atakayenipenda jinsi nilivyo,mwaminifu,mcha mungu na muumin wa kikristo.mpenda maendeleo na asiyetumia pombe.wasiliana nami kwa ndeku1981@hotmail.com
ReplyDeleteMmmhhh
ReplyDelete